Ushauri wa bure kwa BAKWATA na waislamu wenzangu wote kuhusu kususia SENSA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ushauri wa bure kwa BAKWATA na waislamu wenzangu wote kuhusu kususia SENSA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Jumakidogo, Jun 15, 2012.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #1
  Jun 15, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Nimepata tabu kwa muda ili kujaribu kufikiri na kupata sababu na jibu la maana la waislamu kususia hesabu ya watu nchini yaani sensa. Bado sijaelewa idadi ya watu, ama hesabu ya watu inahusiana vipi na imani za kidini wakati wanaohesabiwa ni watanzania wenye dini mbali mbali walionea na kusambaa nchini kwetu.

  Je! Serikali ikichakachua idadi kamili ya watu wa dini fulani na kutoa idadi tofati kutakuwa na faida gani? Je! idadi ndogo ya waumini inasababisha kupungua imani ya watu kwa dini yao? Ukiwa na imani unaweza kuwa na dini yako peke yako, au ya watu sita tu na bado ikawa dini bila ya halaiki ya watu.

  Au lengo letu ni kushindana idadi na watu wa imani nyingine? Hiyo itakuwa na faida gani kwetu.

  Ikiwa ni hivyo, ushauri wangu ni huu.

  Tuiache sensa ya serikali ifanye kazi yake, tukubali kuhesabiwa. Baada ya hapo tufanye sensa yetu ya waislamu tu. Nina hakika kila mtaa haukosi kuwa na shekhe ambaye anaweza kupita na kujua idadi ya waislamu walio katika mtaa wake, ndani ya kipindi kifupi tunaweza kupata majibu kwa kupitia sensa yetu ya uhakika. Maustadhi na mashekhe wetu mbona mengi mnayapigania na kufanikiwa? Je, sensa maalumu kwa ajili ya waislamu tu, itawashinda?

  Hakuna sababu ya kutaka kujua idadi yetu kwa kubebwa na sensa ya serikali wakati uwezo tunao watu wakihamasishwa. Huo ndio ushauri wangu, isije ikawa tunafanya mambo kinyume na demokrasia na matakwa ya jamii inayotuzunguuka.
   
 2. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #2
  Jun 15, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Kwa hoja ya kuwepo kwa mfumo kristo hiyo hesabu ya sensa ya kidini itaaminika na kukubarika???????????? Lakini kikubwa ni muhimu kujua dhamira ya kujuana idadi yetu kwa misingi ya dini ni nini?

  Israel ni nchi ndogo sana na yenye watu wachache sana duniani lakini ina nguvu kuu kuliko nchi zenye watu wengi.....je, idadi ya watu ndio kigezo cha kuwa na nguvu za kisiasa, kijeshi, kidini, na kijamii????????
   
 3. e

  eltontz JF-Expert Member

  #3
  Jun 15, 2012
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 823
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 60
  Well said.
   
 4. e

  eltontz JF-Expert Member

  #4
  Jun 15, 2012
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 823
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 60
  Itakubalika kwa sababu haina matumizi yoyote kwa serikali zaidi ya umo makanisani na misikitini mwenu.
   
 5. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #5
  Jun 15, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  kama ndivyo basi makanisa na misikiti ndio wahesabu watu/waumini wao kama dhamira ni kwa matumizi ya imani
   
 6. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #6
  Jun 15, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Kwani lengo ni kuwaonyesha wengine kuwa sisi ni wengi kuwazidi?
   
 7. iron2012

  iron2012 JF-Expert Member

  #7
  Jun 15, 2012
  Joined: Feb 16, 2012
  Messages: 358
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  naamini ktk tz hakuna sensa ya waumini wa dini fulani ambayo imefanywa na serikali bali kwa wakristu huwa ni kawaida kufanya sensa yao ili kujua active members na non active members kila mwaka sasa kwa nini na wengine wasiige mfano huo? mfano kanisa Katoliki kuna jumuiya ndogondogo ambazo hukutana kimtaa na jumla yao injulikana ukijumlisha jumuiya zote katika parokia unapata idadi kamili ya waumini ktk parokia husika, sensa kama hiyo haihitaji mpaka serikali itoe pesa hata kanisa lenyewe halitoi pesa ila ni utaratibu tu Mungu amewapa uwezo wa kufikiri akawatunikia na akili kwa nini hamvitumii? kila kitu serikali iwafanyie aibu hiyo
   
 8. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #8
  Jun 15, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Kama waumini wote wangekuwa wanakwenda kuswali msikitini na wakristo wote kwenda makanisani sensa ingekuwa nyepesi ..... naona kazi ya kwanza ya dini ni kuwarejesha waislamu na wakristo wote kwenda nyumba za ibada ili wapate sensa yao. wamrudie Mungu hesabu itakuwa rahisi wala hakutakuwa na haja ya kuisumbua serikali ambayo idadi ya waumini wa dini haina umuhimu katika kupanga maendeleo ya watu kama vile barabara, umeme, maji.
   
 9. S

  Sideeq JF-Expert Member

  #9
  Jun 15, 2012
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 2,417
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Sawa! lakini itambulike officially na Serikali.
  Na kama serikali inaweza kugharimia ufanyaji wa sensa , vilevile hawa Masheikh watakaofanya hii kazi wagharimiwe na Serikali.
   
 10. MANI

  MANI Platinum Member

  #10
  Jun 15, 2012
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,409
  Likes Received: 1,861
  Trophy Points: 280
  MamaPOROJO Huoni kuwa Jumakidogo ametoa angalizo kuwa mnaweza kujihesabu nyinyi wenyewe nakuwa na hesabu ambayo sio ya kuchakachuliwa?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 11. e

  eltontz JF-Expert Member

  #11
  Jun 15, 2012
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 823
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 60
  kwani sensa ya serikali watahesabiwa wote siku hiyo???
   
 12. Dr. Wansegamila

  Dr. Wansegamila JF-Expert Member

  #12
  Jun 15, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 1,232
  Likes Received: 817
  Trophy Points: 280
  hapo kwenye red ilitakiwa iandikwe "kukubalika"
   
 13. Kabembe

  Kabembe JF-Expert Member

  #13
  Jun 15, 2012
  Joined: Feb 11, 2009
  Messages: 2,236
  Likes Received: 928
  Trophy Points: 280
  Taabu ya hawa wenzetu hata ukiwapa uongozi wa nchi,yaani Rais,makamu,waziri mkuu na mawaziri wote,makatibu wote,wakurugenzi wa idara wote,wakuu wa mikoa,wilaya wote,wakurugenzi wa mashirika ya umma wote na kadha wa kadha bado hawa jamaa zetu wataendelea kulalamika na kudai mfumo kristo unatawala,frankly is very hard to deal with these characters,they are funny and useless!
   
 14. Dr. Wansegamila

  Dr. Wansegamila JF-Expert Member

  #14
  Jun 15, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 1,232
  Likes Received: 817
  Trophy Points: 280
  wewe unafikiri kuwa watanzania wote dini zao ni ukristo na uislamu tuu?? na unafikiri watanzania wote wana dini?? you are very very wrong
   
 15. mikonomiwili

  mikonomiwili JF-Expert Member

  #15
  Jun 15, 2012
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 274
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Nasema tena kama serikali itawasikiliza na ikaweka kipengele cha dini .Nasis wasukuma lazima tutaungana tukatae mapka kiwekwe kipengele cha ukabila ili na sisi tujue tuko wasukuma wangapi. kwani wafikiri sis ndo hatupendi kujua wasukuma ni wangapi hapa bongo ?

  Na hizo kazi zauongozi zigawie kuendana na idadi asilimia ya makabila kila kabila lenye watu wengi kue na viongozi wengi

  ala usione kimya hata sisi twapenda jua tupo wangapi :A S crown-2:
   
 16. Shinto

  Shinto JF-Expert Member

  #16
  Jun 15, 2012
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 1,781
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Juma Salaam,
  Kwanza sina shaka juu ya uislamun wako kama wengine humu JF, wanaojifanya waislamu kumbe ni makafiri wazuri.
  Kimsingi hata mimi binafsi siathiriki na sensa na matokeo yake.
  lakini unapaswa kuangalia mbali zaidi ya hoja zako hapo juu. Wakristo wanataka Waislamu wafikiri kama wewe ulivyofanya, kwa hiyo itawahakikishia dhulma bila bughdha
  1. Madai ya msingi ya Waislamu ni kuwa Wakristo kwa kuwa ndio wengi serikalini na kwenye ufanyaji maamuzi wanatumia mwanya wa kutokuwa na takwimu sahihi kuhalalisha wao kuwa wengi kila mahali.
  2. kama idadi ya watu wa dini fulani sio issue, kwa nini izungumzwe ile ya makadirio?
  3. Kama kuna haja ya kuwa na makadirio (estimates) kwanini kusiwe na real data?
  4. Pia kuna confusion inayotokana na records za nyuma, mwanzo waislamu walikuwa majority TZ, leo kwa nini wawe 35%?
  Mwisho KWA NINI TUNAOGOPA KUPIMWA? wakati tunasisitiza watu wakapimwe ukimwi! Hapa tunaogopa ukweli?
   
 17. mikonomiwili

  mikonomiwili JF-Expert Member

  #17
  Jun 15, 2012
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 274
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  ohooooo kumbe shida nikugaramiwa na serikali eeeee . Tuache uvivu yaani ukitaka kujua idadi ya watoto wako mpaka usubiri ufathili ?
  watanzania tumezoea sana kufathiliwa
   
 18. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #18
  Jun 15, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,672
  Trophy Points: 280
  Waislam wana haki kama Watanzania na wanalipa kodi ni haki yao kuhesabiwa na serikali hakuna tatizo.
   
 19. S

  Sideeq JF-Expert Member

  #19
  Jun 15, 2012
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 2,417
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Na kutambulika officially Kiserikali
   
 20. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #20
  Jun 15, 2012
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Ni kweli sensa ya makanisani, mf. katika Kanisa Katoliki huwa ni kwa ajili ya matumizi ya kanisani. lengo huwa ni kutaka kujua wingi wa waamini; na kati yao wangapi wako active na wangapi wanajikokota au wameacha imani; wangapi wamefunga ndoa na wangapi kati yao ndoa zao zimevunjika, nk. Kwa kujua idadi hii na michanganuo yake mbalimbali Kanisa huweza kuweka mikakati yake ya utume, mf. ni nguvu gani na kiasi gani zielekezwe kwa wale waliolegea katika imani, au wale ambao ndoa zao ziko kwenye crisis. Na wakati mwingine kwa kujua idadi ya waamini wote katika parokia - kama idadi hiyo imekuwa kubwa sana uongozi wa jimbo waweza kuamua kufungua parokia mpya ili kurahisisha uchungaji wa kundi la Bwana. Hii ni mifano michache yenye kuonesha matumizi ya kikanisa ya sensa iliyofanywa kikanisa.

  Kamwe sensa za kikanisa hazitumiki katika mipango ya maendeleo ya kitaifa bali ziko kwa malengo ya kidini tu au ya kiroho. Na sensa hizi zinafanywa kila mwaka kuanzia jumuiya ndogondogo mpaka jimbo zima. Ni kwa ajili ya mipango ya Kanisa tu.
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...