Ushauri wa Baba unanikosesha usingizi

bize signal

Member
Mar 22, 2021
19
75
Hi wanaJF,

Moja kwa moja niende kwenye mada ni hivi baba yangu mzazi alinipigia simu, baada ya kujuliana hali akanieleza dhumuni la kunipigia simu.

Akanieleza anatambua kuwa nimejiandaa kuishi maisha yangu Dar, hasa akizingatia nimejenga nyumba mbili Dar na na miradi yangu midogo ya kiuchumi iko dar na nyumbani mkoani mara sina japo uwanja. Akasema baada ya kunisomesha na mimi kuamua kuishia diproma tu ,yeye alinielewa hasa nilipomwambia naitaji kuwa mfanya biashara japo itanichukua muda kuwa na uchumi mkubwa.

Aliknikubalia bila shaka akizingatia yeye ni mtumishi na hadi anastaafu akiwa mtumishi mwaminifu ameishia kupata nyumba za kiswahili mbili tu nikisema za Kiswahili mnanielewa ni kama za Tandale.

Ndipo akanieleza ni kweli upo Dar ila ananishauli nitumie fulsa za nyumbani MARA KUFANYA BIASHARA. Nikauuliza una maanisha nini? Akanieleza moja ya ndoto zake ni kuona mimi kijana wake nashiriki mojawapo wa uchumi ulioko mkoani humo.

Akaniambia wewe unaelimu ya kukuwezesha kuingia popote ukizingatia najua kimombo, kwani nimesomea Kenya.

Umezaliwa mkoa wa asali na dhahabu.

Mara kuna migodi mingi na haoni kwa nini sina channel kwenye biashara ya madini japokuwa naifahamu vema kwani nilipokuwa nikisoma ndio ilikuwa ikinisomesha. Siku zote alinipa karo nikainunulia madini na kwenda kuuza nairobi. Ndio napata fedha ilioniwezesha kuishi huko na kulipia chuo.

Unaiachaje nchi ya dhahabu na kuenda kuhangaika huko? Angependa kabla sijafa aone nikishiriki uchumi huo.

Mara kuna utalii. Kwanini huna kempsite, vitaru au gari za kusafirisha watalii?

Mara kuna ziwa mbona sina hata ndoano?

Japo nina ng'ombe wa kunenepesha nje ya dar mbona siuzi ngozi nje ya nchi?. naishia kuuza mifugo tu baada ya kunenepesha?.

Unakwama wapi kijana wangu niingilie?

Anafahamu kuwa nina cash bank sio chini ya mia hamsini milioni nje ya vitega uchumi nilivyonavyo. Nimeamua nikueleze haya nikiwa hai imekuwa ni ndoto yake siku nyingi. wanaJF nishaulini nyie mungemujibu vipi? binafsi nilimwambia ninatafakari.

Akasisitizaunawezaje kiondoka katika vijiji vyenye madini na ukajisahaulisha kama hukuzaliwa kwenye ardhi ya madini?
 
Ushimen

JF-Expert Member
Oct 24, 2012
29,022
2,000
Mzee bado anamtazamo wa nyumbni ni nyumbani, mkataa kwao ni mtumwa.
Mzee anaona kama ukoo na nzao yake inapotea, ipo mbali na nyumbani na mwisho atapoteza kizazi chake.
Kimsingi mafanikio hayana formula, na hakuna popote wala yeyote aliewahi kufaham kwamba wapi penye ahadi/ameandikiwa kwamba ndipo atafanikiwa.
Kwanza mzee nafikiri hajafahamu kwamba KUSOMA ni kitu kingine na kuna tofauti na KUELIMIKA, ambapo pengine wewe kama kijana wake baada ya KUSOMA uliweza KUELIMIKA na ukatengeneza connections na mikakati ya mazingira ili uweze kuyafikia mafinikio katika mazingira yalio kuzunguka wakati tayari UMEELIMIKA.
 
toughlendon_1

JF-Expert Member
Feb 7, 2018
3,214
2,000
Jf kila mtu ni tajiri kila mtu amesoma kila mtu anaishi mjini kila mtu ana ndinga ya maana hahaha jf bana!

Mkuu inawezekana wengi wana hivyo vitu na mimi huwa sion sababu ya mtu yeyote kufanganya kama ana gari na hana hilo gari sababu hivyo vitu vyote wanavyosema vinatafutika sikuiz gari hata milion 4 unapata mkuu sa mkuu ukiamua kuitafuta hela milion nne itakushinda ??
 
Wangari Maathai

JF-Expert Member
Aug 13, 2018
35,054
2,000
Mkuu inawezekana wengi wana hivyo vitu na mimi huwa sion sababu ya mtu yeyote kufanganya kama ana gari na hana hilo gari sababu hivyo vitu vyote wanavyosema vinatafutika sikuiz gari hata milion 4 unapata mkuu sa mkuu ukiamua kuitafuta hela milion nne itakushinda ??
Mie huo msemo esp hapa jf unanishangazaga sana...hv hayo magari yanayopita barabarani watu wake wanaishi sayari ipi??? Yaani watu wan mind za giza balaa...hao waliomaliza degree zao wanaishi sayari ipi? Si humu humu?
Hizo nyumba mnazoona watu wamejenga bungalows wanaishi jupiter au?
Yaani mie nashangaaga balaa... !
Kifupi jf kuna matycoon..kuna watu wanaishi kwenye mijumba mizuri na wanatembelea ndinga kali...wapo sana tu
 
Midimay

JF-Expert Member
Apr 12, 2015
823
1,000
Wewe unafanikiwaje halafu huna miradi ya maana nyumbani? Jua kabisa kwamba kwa hali hiyo hujafuta umaskini. Huo umaskini umepotea temporarily tu. Lakn hiyo 150M ukipeleka kuwekeza nyumbani unatengeneza ajira na fursa na kufuta umaskini wa kijiji kizima.
 
dexterous

JF-Expert Member
Feb 26, 2014
1,784
2,000
Mie huo msemo esp hapa jf unanishangazaga sana...hv hayo magari yanayopita barabarani watu wake wanaishi sayari ipi??? Yaani watu wan mind za giza balaa...hao waliomaliza degree zao wanaishi sayari ipi? Si humu humu?
Hizo nyumba mnazoona watu wamejenga bungalows wanaishi jupiter au?
Yaani mie nashangaaga balaa... !
Kifupi jf kuna matycoon..kuna watu wanaishi kwenye mijumba mizuri na wanatembelea ndinga kali...wapo sana tu
Kweli kabisa mfano taycoon kidukulilo
 
Sweet16

JF-Expert Member
Mar 10, 2014
4,382
2,000
Wewe unafanikiwaje halafu huna miradi ya maana nyumbani? Jua kabisa kwamba kwa hali hiyo hujafuta umaskini. Huo umaskini umepotea temporarily tu. Lakn hiyo 150M ukipeleka kuwekeza nyumbani unatengeneza ajira na fursa na kufuta umaskini wa kijiji kizima.
Na akiamua kuwekeza asije akasema ananunua sjui gari za watalii coz ataishia kununua mbili tu used adi kuzisimamisha 150 inakata.....
Atafute tenders kwene migodi kama mzawa ni njia nzuri ya kukuza iyo 150
 
witnessj

JF-Expert Member
Mar 22, 2015
24,265
2,000
Mzee bado anamtazamo wa nyumbni ni nyumbani, mkataa kwao ni mtumwa.
Mzee anaona kama ukoo na nzao yake inapotea, ipo mbali na nyumbani na mwisho atapoteza kizazi chake.
Kimsingi mafanikio hayana formula, na hakuna popote wala yeyote aliewahi kufaham kwamba wapi penye ahadi/ameandikiwa kwamba ndipo atafanikiwa.
Kwanza mzee nafikiri hajafahamu kwamba KUSOMA ni kitu kingine na kuna tofauti na KUELIMIKA, ambapo pengine wewe kama kijana wake baada ya KUSOMA uliweza KUELIMIKA na ukatengeneza connections na mikakati ya mazingira ili uweze kuyafikia mafinikio katika mazingira yalio kuzunguka wakati tayari UMEELIMIKA.
Mzee wa kende mbili nawewe unatoa advise kwenye hii gahawa

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom