Ushauri wa aina ya bunduki ya kununua

Ushauri wa aina ya bunduki ya kununua

Nyamgluu

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2006
Posts
3,160
Reaction score
1,727
Wadau baada ya kwenda na kumaliza anger management classes, najihis niko tayari kumiliki kiguu cha kuku, ukijumlisha na hali ya nchi yetu inakokwenda, tija ya uhitaji inaongezeka.

Sasa apart from hearing from rap songs sina uelewa wa bunduki na wala ni pistol gani nzuri inapatikana hapa TZ.
300px-Charter_Arms_Bulldog_2.JPG

Nzuri kwa maana, naweza beba kirahisi, haina jams, na risasi hupatikana kirahisi.
Hio hapo juu inaitwa .44 bulldog! Lil waynes pet!
Wenye uelewa naomba ushauri.
 
Anyhow ni sawa tu! Wakishajua tu kama unayo inatosha hakufuati mtu! Ningekuwa mimi naanza na gobore kwanza, halafu naanza na Kuua paka/kunguru mtaani

Hapo baasi hakufuati mtu si jambazi/kibaka wala anayewafukuzia watoto wako wa kike
 
siraha za kihami/kujilinda zipo nyingi isipokuwa inategemea na uhitaji wako.wengine wanapenda kuwa na siraha za kujilinda na kuwindia pia.wengine wanapenda siraha ndogo za kujilinda tu(pistol).sasa sijuwi wewe unataka ya namna gani.ila kwa ufupi tu ni kwamba zile siraha za kuwindia ni zile zenye mtutu wa kati(medium calibre) na kama ni siraha za kujilinda ni pistol zenye mtutu mdogo(small calibre).sasa kama unataka pistol zipo nyingi tu,ambazo nazo zinatofautiana ukubwa kulingana na uwezo wa pistol yenyewe.mfano zipo za ukubwa wa mtutu wa 0.35mm hadi 9mm.hizi za 9mm zina uwezo wa kupiga umbali mrefu hadi mita 200(centre point).umbali wa kupiga inategemea na ukubwa wa calibre ya pistol hiyo.ila kwa ushauri zaidi tembelea maduka yanayouza siraha(Tanganyika arms na pale jeshini upanga)ukienda ktk maduka hayo utapata ushauri wa bure na mzuri na pia utaziona na siraha zenyewe physically na hata ukitaka special order watakuagizia tu ili mradi ufuate taratibu zote za nchi za kumiliki siraha ila revolver hairuhusiwi kwa hapa TZ.ni kwa matumizi ya jeshi tu pamoja na silencer equipmenent.
 
Mtafute Adam Malima au Rage nadhani wana experience zaidi ya hivyo vifaa, atakushauri ni aina gani nzuri.
 
Acha kabisa kufikiria iyo kitu, historia inaonyesha watu wengi waliomiliki hiyo kitu huishia matatani either kwa kujiua wenyewe au kuua watu au kunyanganywa na watu wanaoiwinda kuifanyia uhalifu
 
Hii ndiyo silaha ninayoipenda kwa kujilinda mwenyewe. Inabeba risasi 17 za 9mm.

Glock.jpg

Kwa ulinzi wa nyumbani nakushauri ununue shotgun kama hii 20 bore

Shotgun.jpg
 
Glock 26 ni nzuri sana na bei yake sio kubwa ni kama shs 2m tatizo ni namna ya kupata leseni, usifanye masikhara na leseni ukipitanjia ya halali unaweza kuchukua hata zaidi ya mwaka
 
nafikiri hiyo 45 inafaa zaidi kwa mazingira ya kutekana kiaina aina hapa bongo maana

1287749572.jpg
 
nyie endeleeni kumpa ushauri, unajuaje yupo kwenye ile kamati yao ya..!
 
Usipate tabu hapo congo waasi wengi wa M23 wameziacha kuna RPG Rocket Propelled Gun, au M60 pia sio mbaya pia unaweza nunua hata KIFARU kama hali ya usalama inakutisha mkuu
 
Back
Top Bottom