Ushauri: Vyuo vikuu vibaki vitano tu nchini


Hii mada kama inaukweli flani hivi!? Nyie mnaonaje jamani.
ni hoja/mada ya kipuuzi kutoka kwa mtu mwenye maono mafupi aliyevimbiwa.
 
Mzumbe sio chuo kikuu ni genge la wahuni na eti kuna watu wanaitwa maprofessor ni weupe kichwani hata kuandika research hajui. Kuna shirika Moja linaongozwa na wanaojiita maprofessor wawili wa mzumbe limeiba pesa na hawana uwezo wowote, waoga, wachawi, waongo na wafujaji wa mali za imma kupita kiasi
 
😂😂😂
Ati "incompetence products".

Mbona mwenyewe unaonesha ni kiazi tu.

BTW:Unarudia enzi za akina Mpigamsuli,Pery na ADILI SAMALU.

Na wewe ukikua utaacha tu.
 
Kumekucha, nyie mnaojiona competence, mbona ndo mnaongoza kukwapua pesa za uma,

Lakin mbona tumeona product za mda pale UDSM wakipewa vyeo hugeuka mazuzu,
Kizazi cha kipindi cha Mw Nyerere ndo kilikua na sifa muhimu kuliko hata ulizozitaja ,

Hoja yako haina mashiko
 
Mimi nafikiri vilivyopo havitoshi.Tuongeze kila Mkoa uwe na Angalau Chuo Kikuu kimoja au viwili.
 
Nilivyo iona Tumaini ya iringa tu nka kutoa akili .at least ile Tumaini ya arusha ..
 
Tunahitaji Veta nyingi sana na waalimu wa veta wengi na siyo vyuo vikuu vingi!
Veta haina ishu siku hizi. Tz tulifeli kutoa mfumo gredi na kuweka levo wakati hatuna viwanda, na tukaiingiza ktk jeneza pale tuliposema huwezi kupata diploma kutokea veta hadi uwe na D,D,D,D (4) Kutoka secondary, tulichobakiza ni kuizika tu, majengo tufugie kuku kama MR/Mpoto alivyoshauri.
 
Ati "incompetence products".

Mbona mwenyewe unaonesha ni kiazi tu.

BTW:Unarudia enzi za akina Mpigamsuli,Pery na ADILI SAMALU.

Na wewe ukikua utaacha tu.
kwa akili yako unaona hivyo lkn ni uhuru wako wa kutoa maoni.kutoa matusi ni wazi umeshindwa kujenga hoja.jenga hoja twende kwa hoja na mifano.
 
Tunahitaji vyuo vingi zaidi
wingi wa vyuo siyo suluhisho bali tunataka vyuo bora zaidi.wakati mwingine vyuo vingi ni subjective kwa maana vingi kwa idadi gani.
 
Sasa hizo certificate na diploma zilikuwa zinatolewa na vyuo vikuu? acha uboya wa kukurupuka ku comment bila kuelewa jambo....
 
Tunahitaji vyuo vingi zaidi
Kwa rate ya udahili ikifikia 2025 A level watafauli zaidi ya 200,000 ambao wakigawiwa kwenye vyuo,vyuo kama UDOM,UDSM itachukua Asilimia 40 tu, hao wengine itabidi serikali ijipanue zaid
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…