Ushauri Usioombwa: Andrew Chenge Muajiri Lissu Mapema

Ushauri Usioombwa: Andrew Chenge Muajiri Lissu Mapema

Mimi ningemshauri aende akapige kambi Gamboshi huko.

Ajichimbie kwa kama wiki tatu hivi.

Uzuri ni kwamba sehemu yenyewe haipo mbali na jimbo aliwakilishalo!
Nyani Ngabu, Gamboshi nzima haifui dafu kwa babu yangu yuko Tanga.

Babu ni fundi sana katika dawa zijulikanazo kama 'MVUAZA'.

Akikutengenezea hiyo kitu basi hata kama ulimchinja mtu hadharani (mchana kweupee) mbele ya mashahidi chungu tele hutaitwa mahakamani hata siku moja. Kama unabisha muulize dadaangu Sky Eclat

Mwambie kakaako Chenge anitafute. Ha ha ha.
 
chenge watanzania hatumpendi vibaya mnoooo... mamamamaaaaaaeee zake mwizi mkubwa
 
Mtanikamata ila.hamna wa kunifunga anaesema nilitoa madini bure yeye pia alitoa nyumba za serikali bure.kwa hiyo kesi zetu xinafanana...
Iam not stupid to sign a contract without security
 
Mna
Utani kweli yaani kuna wa kumfunga chenge ? Lisu huwa anakomaa na vilaza mmeona wapi.lisu akimnanga chenge ashtakiwe? Mtasubiri Sana kwa mtemi
 
Kama ningeombwa nitoe ushauri kwa aliyewahi kuwa Mwanaseria Mkuu wa Tanzania Bw. Andrew Chenge ningemwambi atafute mwanasheria ambaye anaweza kumtetea "vigorously". Na wazo la haraka haraka ni kuwa amtafute mbunge mwenzie Tundu Lissu ili itakapofika zamu yake kuitwa na kupigishwa magoti awe na mtu ambaye anaweza kumtetea kwa uwezo na upeo wake wote.

Bad boy, bad boy. They are coming after you Chenge, what u gonna do?

Au wewe ungemshauri vipi Chenge?
Kwa alivyojichafua mzee huyu sijui mwanasheria wake awe malaika kutoka mbinguni,ni suala la muda tu na tutashuhudia nae akipiga magoti kwenye sakafu na suti zake anazopeleka kuzisafisha London
 
Mna
Utani kweli yaani kuna wa kumfunga chenge ? Lisu huwa anakomaa na vilaza mmeona wapi.lisu akimnanga chenge ashtakiwe? Mtasubiri Sana kwa mtemi
Hata kwa Ruge tulisikia vivyo hivyo matokeo yake kapiga magoti sakafuni,hizi sio enzi zile ambazo matapeli waliweza kutamba waziwazi,waliweza kuua na kutoa faini ya 70,000 au ''kusema serikali nimeiweka mfukoni.''
 
Yaan mwanakijiji umefikia kutoa mada kama hizi?? Sijafikiria kama ungefika huku. Jitafakari najua unamjua vizuri tundu Lissu. Ila kuwa ccm kunakufanya ujitoe fahamu . Si jambo jema kudhalilisha nafsi yako kwa kuandika vioja huku kichwa chako Mungu alikujaliwa kuwa na hoja. Pls jitafakari!!
 
Bad boy, bad boy. They are coming after you Chenge, what u gonna do? .....hahaha ....ooooh bad boy!
 
Hata kwa Ruge tulisikia vivyo hivyo matokeo yake kapiga magoti sakafuni,hizi sio enzi zile ambazo matapeli waliweza kutamba waziwazi,waliweza kuua na kutoa faini ya 70,000 au ''kusema serikali nimeiweka mfukoni.''


Amepiga magoti ila hskufungwa na hatafungwa..... endeleni.na maigizo toka gamboshi sijui chato
 
Back
Top Bottom