happiness win
JF-Expert Member
- Aug 30, 2011
- 2,461
- 1,394
Nimeikuta hii kwenye pm yangu. Huyu anaomba ushauri.
Niliolewa 2005 na kubahatika kupata watoto 2. Ndoa yangu ilikuwa tamu sana, tatizo mume wangu alipata ajali kazini, yeye fundi kwa kuchomelea kiwandani akaumia vibaya katika uume wake na sasa haufanyi kazi kabisa. Nimemuuguza na amepona na tunaendelea na maisha. Tatizo wivu, sina raha mwenzio inafikia hadi ananikagua akihisi nimetoka kufanywa. Hata kanisani haniruhusu kwenda nilikuwa nafanya biashara zangu Kariakoo sokoni amenizuia kwa sasa niko tu nyumbani ila biashara zinaendelea yeye anazisimamia vizuri tu. Sina raha mwenzako wivu umezidi nami ni binadamu najisikia kuwa na mtu je naweza dai talaka? najiuliza nitaanzia wapi? nisaidie ushauri tafadhali nashindwa kuwashirikisha ndugu katika hili wasije ona namnyanyapaa na kumtangazia kuwa hafanyi. au tuseme ungekuwa wewe ungefanyaje?