Ushauri unahitajika

miss wa kinyaru

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2012
Posts
542
Reaction score
356
Kuna rafiki yangu aliwahi kuolewa baadae akashindana na mme wake wakaachana lakini walikuwa wamebahatika kupata watoto wawili, ni miaka nane sasa tangu watengane na mme wake, alikataa kabisa kuolewa tena, japo kuna wanaume mbali mbali walitaka wamuowe alikataa, ni wanaume wengi tu walimfuata wakiwa na nia ya kumuoa alikataa.

Kati yao kuna mmoja tangu mwaka 2010 anamfuatilia alishamtukana alishamjibu majibu yote ya sitaki lakini yule baba hakuacha kusistiza kwamba wewe ndo mke wangu najua ipo siku, huyo baba nae alishaachana na mke wake mwaka ule ule aliotengana na mme wake, kwa hiyo huyo baba nae ana miaka nane sasa yuko single, na yeye ana watoto wawili pia.

Kwenye mwezi wa sita akawa kwenye relationship na baba mmoja ambae nae alikuwa anamfuatilia siku nyingi pia nae alikuwa ameshaachana na mke wake na wakakubaliana hivi wawe pamoja wasomane ili ikiwezekana mwakani mwanzoni waowane, lakini rafiki yangu akaona tabia zao haziendani akamwambia hawezi kuendelea na uhusiano huo, japo huyo baba alilalamika sana.

Mwezi wa tisa akaamua amkubalie yule baba sasa yule baba yeye kila siku alikuwa anaomba aende kwao na rafiki yangu akajitambulishe then ampeleke kwao, yule dada anakataa anamwambia subiri kwanza, kama wiki 2 zimepita yule baba kampigia simu mama yake kwamba anataka kuoa amepata mchumba kwa hiyo siku yoyote atampeleka nyumbani awatambulishe.

Yule mama kafunga safari mpaka kwa kijana, akamwambia hakuna kuoa mwanamke mwingine mrudie aliyekuwa mkeo mimi huyo ndo namtambua maana kila nikipata matatizo huwa yuko na mimi bega kwa bega siwezi kupata mkwe mwingine kama huyo.

Mtoto nae hataki anasema yule dada alikuwa malaya alishamfumania mara kibao, mama anamtetea anasema atakuwa ameshajifunza kwa mda uliomuacha.

sasa huyo baba yuko njia panda lakini anasema hawezi kurudiana na huyo mwanamke yeye lazima amuowe rafiki yangu.

Sasa rafiki yangu alikuwa anaomba ushauri je akubali kuolewa japo mama mkwe hataki au aachane na huyo mwanaume?

japo huyo mwanaume anampenda sana rafiki yangu lakini itakuwaje kwa mama mkwe?
 
Nimempenda rafiki yako kwa kubadilisha wanaume. Yani wote hao aliokuambia wameshindwana wana matatizo. Na hapo kuna ambao hajakwambia.

Namwonea huruma huyo mbaba anayetaka kuoa.

Ukimwona mpe pole zangu.
 
Yule mbaba!
Yule mbaba!
Yule mbaba! Katikati ya thired yako kuna mkanganyiko!
...
Kama shoga yako anampenda mbaba, na mbaba anampenda shosti wako mwambie tu waoane!
Mapenzi ni ya wawili!
...
Huyo mama wa mbaba, hatokosa hicho alichokua anakipata kwa huyo mkwewe!
Yap! Coz watoto wao wawili ni connection tosha ya mama wa mbaba na mkwewe!
...
Labda nikuulize:
kwani huyo aliekuwa mkewe bado anampenda/anamtaka mbaba??
 

...Je huyo Rafiki yako Yeye anataka Kuolewa?
 
...Je huyo Rafiki yako Yeye anataka Kuolewa?
Nimeongea nae anasema alikuwa ameamua aolewe tu na huyu baba, na tayari alikuwa ameshaanza kumpenda huyo baba lakini sasa shida imekuja kwa mama mkwe.
 
Reactions: Mbu


mwambie huyo rafiki yako aachane na huyo mwanaume ili huyo mwanaume arudiane na mkewe kwa sababu huyo mwanaume aliachana na mke wake kwa sababu mkewe alikuwa malaya, na rafiki yako naye ni malaya pia. Tena inawezekana ni malaya kuliko mke wa zamani wa jamaa. Asije akasababisha huyo mwanaume akafa kwa presha au akamwua maana unadhani huyo rafiki yako si malaya ilhali ni malaya kwa maelezo yako wewe mwenyewe.
 
Mbaba anamuoa mmama (rafiki yako) wote wana watoto wawili nje ya itakayokuwa ndoa yao si ndio?
Ushauri!
1.Muulize rafiki yako kama yuko tiari kuwalea watoto wa mwanamke mwenzie kama wa kwake bila kusababisha migogoro ndani ya ndoa!
2. Atampenda na kujipendekeza kwa mama mkwe kama mgoni wa mbaba anavyofanya ili kufurahiwa na mama mkwe
3. Ataacha tamaa ya wanaume kama ilivyokuwa anafanya awali maana mume aliyezaa naye + mbaba wa kati + mbaba wa sasa! namaanisha afunge brake!


Akiwa tiari kwa kila kilicho hapo juu basi aolewe tu! kama kuna kimojawapo hawezi basi atemane naye atafute mbaba mwingine!
 
Nimeongea nae anasema alikuwa ameamua aolewe tu na huyu baba, na tayari alikuwa ameshaanza kumpenda huyo baba lakini sasa shida imekuja kwa mama mkwe.

Genesis 2:24

That is why a man leaves his father and mother and is united to his wife, and they become one flesh.
 
Inabidi nimuonyeshe asome mwenyewe, maana ushauri mwingine ni vigumu mtu kumwelelezea
 
Huyo shosti wako anatafuta balaa, mwisho wa siku ataonekana ana tabia mbaya kwa kuachwa na kila mwanaume.

Hivi miaka nane bila ndoa ameshindwa kuendelea na maisha yake na watoto wake; Tena mwambie aache mtindo wa
kubadili wanaume kama nguo, atakuja kuwaacha watoto wake kwa ajili ya kutokutulia...... mpe salamu zangu.
 
Hii nayo ni style mpya ya umalaya !!
Samahani kwa kusema hivyo ila rafiki yako ni malaya
 

ingekuwa mimi ni huyo mwanaume ningemuuliza mama yangu ''hivi ni wewe unaeoa na kuishi na huyu mwanamke au ni mimi?''unataka mimi nirudiane nae kwasababu ktk matatizo yako binafsi anakupa vijisenti km sio ushauri ambao ata mimi km kijana wako naweza kukupa? mahusiano kwa upande wangu hayaitaji third party, only wawili wapendanao tu wakishakubaliana hao mtu mwingine hayamuhusu,anaweza kuishia kushauri tu na hivyo ushauri wake unaweza kukubaliwa au kukataliwa
 
Nimemuonyesha hii coment yako anasema usimlaumu kwa hilo, yeye akiwa na mtu hawezi kuwa na mtu mwingine mpaka aachane nae, hata akiingia kwenye ndoa hawezi kutoka nje ya ndoa maana yeye huwa anapenda kupita kiasi hawezi kumsaliti mme wake, hata huyo mme waliyeachana aliachana nae kwa sababu mme hakuwa mwaminifu alimvumilia akachoka, sasa huyu anaona kama historia na tabia zao zinafanana ndo maana alikuwa ameridhia kuoana nae. lakini hofu yake ni mama mkwe
 

kwa hapa sijui, lakini kwa maelezo yake mimi nimeona yule mwanamke bado anampenda mme wake ndo maana anajipendekeza kwa mama mkwe ili arudiane, si unajua wa mama na watoto wa kiume ni damu damu, anaweza mama kapewa hata rushwa ndo maana anakomaa kijana warudiane na huyo mtalaka wake. ila ningekuwa mimi ningetema mzigo aisee
 
Nimempenda rafiki yako kwa kubadilisha wanaume. Yani wote hao aliokuambia wameshindwana wana matatizo. Na hapo kuna ambao hajakwambia.

Namwonea huruma huyo mbaba anayetaka kuoa.

Ukimwona mpe pole zangu.

Na mim pia umpe pole zangu manaake huyo dada ataendelea kuwa kwenye majaribio ya kuangalia mwanaume anaemfaa hata kwenye ndoa, kwhyo ikitokea hivyo awe mpole
 
huyo rafiki yako hana msimamo na anafanya mambo kwa kubahatisha ... ndoa / mahusiano ni ya watu wawili japo yanakuja kuzungukwa na watu mbali mbali .. ukishaanza kuona kikwazo huna haja ya kulazimisha kwani utapata shida baadae
 
hata mimi nilimwambia kama umeweza kukaa miaka 8 mwenyewe ya nini ujiingize kwenye stress za ndoa tena? tabia ya kubadili wanaume hiyo amesema hana, huyu mwingine kuna mambo ambayo asingeweza kuyavumilia, kanisimlia siwezi kuyaandika hapa. anasema akiwa na mtu huwa ni mwaminifu sana, mme wake hakuwa mwaninifu alivumilia akachoka akaamua aanze maisha yake. mimi nimemwambia kila likuepukalo lina heri na wewe, achana nae huyu mwanaume endelea na maisha yako kama zamani
 
Mwambie ajitunze mwenyewe na watoto wake;
Tena atakuwa na muda mzuri wa kuwa karibu na wanae;

Kwa hilo mi sidanganyiki kabisa; Ukishashindwa ndoa ya kwanza
usijaribu ingine, utakuja aibika na kuonekana una matatizo.

..... mpe tena salamu zangu, mwambie .....a take care herself.........

 
zitafika, tena kaondoka sasa hivi maana anafanyia kazi shinyanga jana ndo alikuja akanipa hiyo story na kuniomba ushauri eti afanyeje? nimemwambia ishi uwezavyo usiishi kwa kuangalia watu wananifikiriaje? heshima ni wewe mwenyewe ulivyo na ndoa, ni wangapi wamo kwenye ndoa jina tu kwamba ni wanandoa, ndoa ni ile ile na wanaume ni wale wale.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…