Ushauri / Ujumbe kwa JWTZ

Ushauri / Ujumbe kwa JWTZ

itakiamo

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2014
Posts
1,071
Reaction score
1,865
NAPENDA KUWASILISHA MAPENDEKEZO KUHUSU JINSI JWTZ INAVYOWEZA KUREJESHA NA KUIMARISHA IMANI YA JAMII KUPITIA MAUDHUI YA FILAMU NA TAMTHILIA (MOVIES/SERIES).
Kwa kuzingatia nafasi kubwa ya sanaa katika kuelimisha na kuunganisha jamii, napendekeza JWTZ itengeneze series mbili hadi tatu zenye lengo la kujenga awareness, uaminifu, na uelewa wa kina kwa jamii kuhusu majukumu, maadili, na mchango wa JWTZ katika kulinda taifa.
Mapendekezo Mahususi ni kama ifuatavyo:

1. Maudhui ya Kweli (True Stories):

Movies/series zihusishe historia ya kweli na simulizi halisi za missions ngumu na za kihistoria ambazo JWTZ imewahi kushiriki — iwe ni ndani au nje ya nchi. Hii itasaidia jamii kuona uhalisia, uzalendo, na kujitoa kwa askari wetu.

2. Mtindo wa Uwasilishaji:
Maudhui yawe ya kisasa, yenye ubora wa juu, yakichanganya drama, realism, na documentary style ili kuongeza uhalisia na kugusa hisia za watazamaji.

3. Uchaguzi wa Director na Wataalamu:
Ichaguliwe Director mwenye uwezo, maono, na nidhamu ya kazi, anayeweza kuheshimu misingi ya JWTZ na wakati huohuo kuwasilisha hadithi kwa lugha inayoeleweka na kukubalika na jamii.

4. Uchaguzi wa Wasanii:
Napendekeza kuepuka kutumia wasanii maarufu wa “Sinza” wanaojulikana zaidi kwa umaarufu kuliko uhalisia wa uigizaji.
Badala yake, wachaguliwe wasanii wenye uwezo wa kuigiza kwa uhalisia mkubwa. Benroyal Pictures wana wasanii wenye nidhamu, uwezo wa kuigiza roles nzito, na wanaofaa sana kwa aina hii ya maudhui.

5. Ushirikishwaji wa JWTZ Ndani ya Production:
JWTZ iwe sehemu ya karibu katika uandishi wa script, ushauri wa kiufundi, mavazi, lugha ya kijeshi, na mazingira ya kazi ili kuhakikisha uhalisia na kulinda taswira ya jeshi.

6. Ujumbe Chanya kwa Jamii:
Movies/series zionyeshe pia upande wa kibinadamu wa askari — uzalendo, kujitolea, changamoto za kifamilia, nidhamu, na mchango wao katika amani na maendeleo ya taifa.

7. Mkakati wa Usambazaji (Distribution):
Maudhui yaonyeshwe kwenye majukwaa yanayofikika kwa urahisi kama runinga za kitaifa, majukwaa ya kidigitali, na hata shule au vyuo kama sehemu ya elimu ya uzalendo.

Kwa ujumla, naamini sana kuwa kupitia movies na series zenye uhalisia, ubora, na maudhui ya kweli, JWTZ itaweza kuimarisha uaminifu, kurejesha heshima, na kujenga upya mahusiano chanya na jamii.

Nawasilisha mapendekezo haya kwa heshima kubwa na kwa nia njema ya kuona JWTZ ikiendelea kuwa taasisi inayoheshimika na kuaminiwa na Watanzania wote.
 
Nadhani hy movie ikielezea watu walivyouawa 29, 30 na 31 October pamoja na JW kuhusika kwenye mauaji hayo wakishirikiana na wanasiasa wauaji, hiyo movie itauza sana kimataifa na kuleta watalii wengi mno kwenye hii nchi mara mbili ya watalii wanaoingia Ufaransa mana ile kazi ya mauaji ya watu wasio na hatia waliifanya vyema.

Tunasema damu ni nyekundu ila huo ni uongo, kwa walioshuhudia yale mauaji na zile maiti watakubaliana nami kuwa damu ni nyeusi.
 
NAPENDA KUWASILISHA MAPENDEKEZO KUHUSU JINSI JWTZ INAVYOWEZA KUREJESHA NA KUIMARISHA IMANI YA JAMII KUPITIA MAUDHUI YA FILAMU NA TAMTHILIA (MOVIES/SERIES).
Kwa kuzingatia nafasi kubwa ya sanaa katika kuelimisha na kuunganisha jamii, napendekeza JWTZ itengeneze series mbili hadi tatu zenye lengo la kujenga awareness, uaminifu, na uelewa wa kina kwa jamii kuhusu majukumu, maadili, na mchango wa JWTZ katika kulinda taifa.
Mapendekezo Mahususi ni kama ifuatavyo:

1. Maudhui ya Kweli (True Stories):

Movies/series zihusishe historia ya kweli na simulizi halisi za missions ngumu na za kihistoria ambazo JWTZ imewahi kushiriki — iwe ni ndani au nje ya nchi. Hii itasaidia jamii kuona uhalisia, uzalendo, na kujitoa kwa askari wetu.
2. Mtindo wa Uwasilishaji:
Maudhui yawe ya kisasa, yenye ubora wa juu, yakichanganya drama, realism, na documentary style ili kuongeza uhalisia na kugusa hisia za watazamaji.
3. Uchaguzi wa Director na Wataalamu:
Ichaguliwe Director mwenye uwezo, maono, na nidhamu ya kazi, anayeweza kuheshimu misingi ya JWTZ na wakati huohuo kuwasilisha hadithi kwa lugha inayoeleweka na kukubalika na jamii.
4. Uchaguzi wa Wasanii:
Napendekeza kuepuka kutumia wasanii maarufu wa “Sinza” wanaojulikana zaidi kwa umaarufu kuliko uhalisia wa uigizaji.
Badala yake, wachaguliwe wasanii wenye uwezo wa kuigiza kwa uhalisia mkubwa. Benroyal Pictures wana wasanii wenye nidhamu, uwezo wa kuigiza roles nzito, na wanaofaa sana kwa aina hii ya maudhui.
5. Ushirikishwaji wa JWTZ Ndani ya Production:
JWTZ iwe sehemu ya karibu katika uandishi wa script, ushauri wa kiufundi, mavazi, lugha ya kijeshi, na mazingira ya kazi ili kuhakikisha uhalisia na kulinda taswira ya jeshi.
6. Ujumbe Chanya kwa Jamii:
Movies/series zionyeshe pia upande wa kibinadamu wa askari — uzalendo, kujitolea, changamoto za kifamilia, nidhamu, na mchango wao katika amani na maendeleo ya taifa.
7. Mkakati wa Usambazaji (Distribution):
Maudhui yaonyeshwe kwenye majukwaa yanayofikika kwa urahisi kama runinga za kitaifa, majukwaa ya kidigitali, na hata shule au vyuo kama sehemu ya elimu ya uzalendo.
Kwa ujumla, naamini sana kuwa kupitia movies na series zenye uhalisia, ubora, na maudhui ya kweli, JWTZ itaweza kuimarisha uaminifu, kurejesha heshima, na kujenga upya mahusiano chanya na jamii.
Nawasilisha mapendekezo haya kwa heshima kubwa na kwa nia njema ya kuona JWTZ ikiendelea kuwa taasisi inayoheshimika na kuaminiwa na Watanzania wote.
trust is like a broken glass once broken.........????
 
Hamna kitu babu.Nidhamu jeshini ishapotea na ndio maana unasema wananchi hawana imani nao tena.Nidhamu ndio ilikuwa nguzo kuu ya JW sahivi imekuwa ni tofauti kabisa.

Sema hii mada asione yule jamaa anajiita somebody wa kinondoni utajuta
 
Jeshi halihitaji imani au kupendwa na wananchi

Ni taasisi nyingine kabisa, ina sheria zao, hospitali zao, maduka yao, mahakama zao na maisha yao

Hawahitaji imani wala kupendwa na mtu
Akili mtu wangu.Sema huko sahihi tu.Kwahiyo jeshi limeundwa la kazi gani sasa kama halihitaji kuungwa mkono na wananchi.Hivi hao military personnels huwa jeshi linawatoa wapi?(si kwa wananchi).Aya wananchi hao nao wakasema tunalisusa itakuaje?
 
Haya lisuseni halafu uone nini kitatokea

Unaweza kuwasusia labda polisi au mgambo ila siyo JWTZ

Jeshi ni nchi nyingine kabisa ndiyo maana hakuna kitu unashea nao, wana hospitali zao, maduka yao, mahakama zao na maisha yao

Hata barabarani wakipita hawatumii sheria wala kufuata sheria za barabarani kama raia wengine wa kawaida

Wewe Endelea kujiwazia una akili
 
Hapa unaongea kama mtoto mdogo jamaa yangu.Eti jeshi lina shule sijui masoko sijui blah! blah! So what?

Jeshi ni nchi nyingine?(uliambiwa na nani).Hivi unajua madhumuni ya kuanzishwa kwa jeshi la wananchi?(JWTZ).Ingekuwa jeshi linajitosheleza kwanini warudi kwa wananchi kufanya recruitment ya hao military personnels sasa?

Hivi kuna mtu kakwambia kalisusa jeshi au watu wamekosa imani na jeshi lao.JamiiForums nilijua kutakuwa na watu wana reasoning nzuri kumbe na wewe humo.Kazi kweli kweli

Yani unasema jeshi ni nchi nyingine wakati hao wanajeshi nashinda nao huku Makole?(wanatumia kila kitu wanachotumia raia wengine).Ebu punguza akili za kitoto man
 
Sasa ukishinda nao huko makole ndiyo unadhani ni wenzako?

Jeshi lihitaji imani au kupendwa na wananchi kwa faida gani?

Eti warekodi movie ili wapendwe na wananchi!

Peleka utoto wako huko Facebook
 
Aliyeandika kurekodi movie ni mimi au unasoma kiarabu hapa?.

Nyie ndio huwa nasikia mnasema wanajeshi hawafi.Kiufupi hujui hata dhumuni la kuanzishwa kwa JWTZ.Ungekuwa unajua usingekuwa unauliza kwanini jeshi linahitaji kuaminiwa na wananchi.

Kama huu ndio mwisho wako wa kuwaza basi kuna watu wengi FB wanakuzidi mbali.Mwenzetu shule ulienda au napoteza muda wangu bure tu hapa?

Wanajeshi nashinda nao Makole na hawana maajabu.Ushamba wako tu ndio mzigo kwani wanajeshi si wanatoka uraiani au unadhani wale ni viumbe special kutoka sayari nyingine?ningelikuwa napenda jeshi sahivi ningekuwa natafuta kuwa captain maana nilikataa huo ujinga.Hakuna kitu special kwa mwanajeshi labda nikusanue kuanzia leo.
 
Haya lisuseni halafu uone nini kitatokea

Unaweza kuwasusia labda polisi au mgambo ila siyo JWTZ

Jeshi ni nchi nyingine kabisa ndiyo maana hakuna kitu unashea nao, wana hospitali zao, maduka yao, mahakama zao na maisha yao

Hata barabarani wakipita hawatumii sheria wala kufuata sheria za barabarani kama raia wengine wa kawaida

Wewe Endelea kujiwazia una akili
TAKATAKA NA AKILI NDOGO!
KUWA NA MADUKA YAO AU HOSPITAL ZAO KUNAWASAIDIA NINI?

SHIDA,MNAAJIRI VIJANA WASIOJIELEWA.
 
Aliyeandika kurekodi movie ni mimi au unasoma kiarabu hapa?.

Nyie ndio huwa nasikia mnasema wanajeshi hawafi.Kiufupi hujui hata dhumuni la kuanzishwa kwa JWTZ.Ungekuwa unajua usingekuwa unauliza kwanini jeshi linahitaji kuaminiwa na wananchi.

Kama huu ndio mwisho wako wa kuwaza basi kuna watu wengi FB wanakuzidi mbali.Mwenzetu shule ulienda au napoteza muda wangu bure tu hapa?

Wanajeshi nashinda nao Makole na hawana maajabu.Ushamba wako tu ndio mzigo kwani wanajeshi si wanatoka uraiani au unadhani wale ni viumbe special kutoka sayari nyingine?ningelikuwa napenda jeshi sahivi ningekuwa natafuta kuwa captain maana nilikataa huo ujinga.Hakuna kitu special kwa mwanajeshi labda nikusanue kuanzia leo.
Hawa wapumbavu sana hawajui jinsi uungwaji wa mkono na wananchi ulivyo wa muhimu ,vita ikiibuka hapa wanaopelekwa mstari wa mapambano ni raia , vita ya kagera raia ndio waliosombwa kwenda mstari wa mbele wa mapambano na si askari tu ambao nchi hii ,hawafiki laki moja .NI UPUUZI KUDHARAU WANANCHI ,........ MZALENDO WA KWANZA NCHI HII NI MWANANCHI .........Hawa wasennge chama cha maharamia unaowaona kwenye majukwaa kujitia wazalendo na mabendera shingoni hutawaona wao wala matoto yao yakipelekwa mstari wa mapambano vitani ........
..........MPUMBAVU NDIO HAJUI NCHI NI WANANCHI RAIA
 
Aliyeandika kurekodi movie ni mimi au unasoma kiarabu hapa?.

Nyie ndio huwa nasikia mnasema wanajeshi hawafi.Kiufupi hujui hata dhumuni la kuanzishwa kwa JWTZ.Ungekuwa unajua usingekuwa unauliza kwanini jeshi linahitaji kuaminiwa na wananchi.

Kama huu ndio mwisho wako wa kuwaza basi kuna watu wengi FB wanakuzidi mbali.Mwenzetu shule ulienda au napoteza muda wangu bure tu hapa?

Wanajeshi nashinda nao Makole na hawana maajabu.Ushamba wako tu ndio mzigo kwani wanajeshi si wanatoka uraiani au unadhani wale ni viumbe special kutoka sayari nyingine?ningelikuwa napenda jeshi sahivi ningekuwa natafuta kuwa captain maana nilikataa huo ujinga.Hakuna kitu special kwa mwanajeshi labda nikusanue kuanzia leo.
Kati ya mimi na wewe nani ameanza kumu-quote mwenzake?

Mimi nimemjibu aliyeleta uzi wewe ukaanza kujibizana na mimi

Kwenda shule na kuwa na akili ni vitu viwili tofauti

Inawezekana ulienda shule ukapata Elimu ila Akili bado huna

Elekea kule Facebook kuna jamaa zako mnafanana
 
Jeshi halihitaji imani au kupendwa na wananchi

Ni taasisi nyingine kabisa, ina sheria zao, hospitali zao, maduka yao, mahakama zao na maisha yao

Hawahitaji imani wala kupendwa na mtu
Unaelewa nini principle moja Administration
" Military civilian cooperation" ?

Unafahamu kuwa bila Raia tusingeshinda vita ya Uganda???? Vita inategemea information na Info au Int huipati kokote mbali na Raia....Raia wakisusia umeisha ndugu....

Ndani tukivamiwa sasahivi hata na Burundi wanatuchakaza vizuri ...

Mimi nikitaka kuja kwako kukuibia sihitaji kuja na silaha, nitahitaji kijana wako au housgirl wako anape Info za kwako muda na wakati unaingia na kutoka ...bhaaaass.....sasa wewe poteza trust kwa mfanyakazi wako uone cha moto
 
Back
Top Bottom