Ushauri: TANESCO rudisheni Service Charges

Hardlife

JF-Expert Member
Apr 11, 2021
2,750
6,247
Miaka ya nyuma kidogo TANESCO walikuwa wana charge Tsh. 7,000/= kwa mwezi kama Service Charge kwa wateja wake. Lakini ilikuja kufutwa kwakuwa ilionekana ni mzigo kwa watumiaji wa umeme hasa wale wa Tariff 1 na Tariff 0 kwakuwa ndio wateja zaidi ya 90% ya wateja wote wa TANESCO. Hii nikiri kwamba ulikuwa ni mzigo mkubwa sana kwa watumiaji wa umeme.

Katika uchunguzi wangu naona TANESCO wanajiendesha kwa gharama kubwa sana katika kuhudumia wateja wake maeneo mbalimbali nchini. Mfano mteja anaweza akawa yupo umbali wa Kilometre 100 kutoka ofisi zilipo na akatoa taarifa kuwa hana umeme. TANESCO wataenda kumhudumia na ajabu wanaenda kukuta ni Circuit Breaker tu imetrip. Hapo go and return umeenda 200km. Kwa gari yenye burning rate ya 5kms/l maana yake hapo umetumia litre 40. Let say litre 1 ni Tsh 2000.

Maana yake umetumia Tsh 80,000/= kwenda kumhudumia mteja tena wa Tariff 0 ambaye maximum ananunua umeme wa Tsh 9000 kwa mwezi. Hapo nimepigia mteja mmoja wa direction moja na pia gharama za wear and tear za gari hazijapigwa, gharama za kusogeza odometer karibu na service hazijapigwa. Sasa katika hili jaribu kuzidisha na magari yote Tanzania uone gharama zake. Hii kwangu mimi inachelewesha maendeleo kwa TANESCO hata kama wanapata faida.

Wazo langu ni kuwa TANESCO wa charge angalau Tsh 1000/= kwa mwezi kama mamlaka nyingine zinavyofanya. Naamini idadi ya wateja wa TANESCO wanaweza kuwa zaidi ya 2m. Maana yake hapo TANESCO wanaweza kupata zaidi ya Tsh. 2B kwa mwezi na zikasaidia kwenye mambo yafuatayo.

a) Kuboresha huduma kwa kuongeza idadi ya magari na wafanyakazi ili kuhudumia wateja ipasavyo.

b) Kupata fedha za kupeleka umeme maeneo ya kimkakati hasa viongozi wa kitaifa wanapoagiza.

c) Kuboresha hali ya umeme maeneo ambayo umeme sio mzuri sana.

d) Kupata fungu la kuhakikisha miundo mbinu chakavu inafanyiwa kazi na kupata reliable power supply.

e) n.k.

Najua hapa nitashambuliwa sana lakini lengo ni kujenga nchi na si vinginevyo.

Nawasilisha.
 
Una Roho Mbaya kuelekea ya Mchawi.
Naomba ujibu hoja. Nilijua nitashambuliwa sana. Juzi juzi hapa mbunge mmoja sikumbuki jina alitoa wazo la kodi fulani alishambuliwa kama nini vile. Lete wazo.
 
Kusogeza huduma karibu ni gharama pia.
Jaribu kufanya tathmini kati ya kusogeza huduma karibu na wanainchi, ofisi ndogo ya TANESCO ktk miji midogo, na kundelea kuwatumikia wanainchi kwa umbali wa kilometers kutoka makao Makuu ya halmshauri. Je, kipi ni gharama zaidi?

Habari za kuturudisha nyuma hatutaki. Service charge ulikuwa ni uhuni wa kitapeli kwa wanainchi.
 
Service charge = Capacity charge

Kama ni nguzo unanunua
Waya, mita na kila kitu unanunua kwa gharama halisi wanayopanga wao.
Bei ya unit moja ya umeme wanapanga wao na serikali yao.
Wanalipa mamilioni kwa akina Songas kifisadi
Hiyo service charge ni kwaajili ya??? kVA?

Kaangalie maisha ya kuanzia senior staffs mpaka MD, ufananishe na vipato vyao vya mwezi, kisha uje useme shirika halina uwezo wa kumhudumia mwananchi mtoa kodi aliye mbali na ofisi zai kisa wao hawastahili kuwa na ofisi remote area!

Kamuulize Ngeleja na Kazaula, Muhongo na Maswi, Mhando na Jei, Sa..ma na Greenbird, Ruge na Singh. Wakiwa na maoni ya kuwa shirika linahitaji service charge kutuhudumia, basi hamna budi irudishwe.
 
Jaribu kufanya tathmini kati ya kusogeza huduma karibu na wanainchi, ofisi ndogo ya TANESCO ktk miji midogo, na kundelea kuwatumikia wanainchi kwa umbali wa kilometers kutoka makao Makuu ya halmshauri. Je, kipi ni gharama zaidi?..
Ila kwa ile gharama ya 7000 hata mie sikubali kabisa. Kusogeza huduma karibu kutahitaji Jengo, wafanyakazi, usafiri, vitendea kazi (Tools na Magari), mtandao nk. Sasa fanya unaongeza vituo 100 tu. Ni gharama kubwa sana.
 
Back
Top Bottom