Ushauri: TANESCO rudisheni Service Charges

Mambo hayaendi hivyo

Ungekua mshabiki wa mpira usingeshangaa tanesco kutumia gharama kubwa kwenye ishu ndogo

Watu hatushangai kuona yanga akitoa mil 40 kuihonga prisons kwenye ligi ambayo kombe lake lina thamani ya 20M.

Ajabu ni kwamba kahonga ili ashinde mechi na sio kuchukua kombe ambapo kuna iwezekano akaja kulikosa kombe lenyewe

We unataka kuniambia hasara ya tanesco no kubwa sana kuliko hasara ya yanga?
 
Lengo la tanesco sio kupata faida.

Ile Ni taasisi kwa ajili ya kutoa huduma kwenye jamii.
 
Umetumwa na mbunge wa Ilala ..
Miaka ya nyuma kidogo TANESCO walikuwa wana charge Tsh. 7,000/= kwa mwezi kama Service Charge kwa wateja wake. Lakini ilikuja kufutwa kwakuwa ilionekana ni mzigo kwa watumiaji wa umeme hasa wale wa Tariff 1 na Tariff 0 kwakuwa ndio wateja zaidi ya 90% ya wateja wote wa TANESCO. Hii nikiri kwamba ulikuwa ni mzigo mkubwa sana kwa watumiaji wa umeme.
Katika uchunguzi wangu naona TANESCO wanajiendesha kwa gharama kubwa sana katika kuhudumia wateja wake maeneo mbalimbali nchini. Mfano mteja anaweza akawa yupo umbali wa Kilometre 100 kutoka ofisi zilipo na akatoa taarifa kuwa hana umeme. TANESCO wataenda kumhudumia na ajabu wanaenda kukuta ni Circuit Breaker tu imetrip. Hapo go and return umeenda 200km. Kwa gari yenye burning rate ya 5kms/l maana yake hapo umetumia litre 40. Let say litre 1 ni Tsh 2000. Maana yake umetumia Tsh 80,000/= kwenda kumhudumia mteja tena wa Tariff 0 ambaye maximum ananunua umeme wa Tsh 9000 kwa mwezi. Hapo nimepigia mteja mmoja wa direction moja na pia gharama za wear and tear za gari hazijapigwa, gharama za kusogeza odometer karibu na service hazijapigwa. Sasa katika hili jaribu kuzidisha na magari yote Tanzania uone gharama zake. Hii kwangu mimi inachelewesha maendeleo kwa TANESCO hata kama wanapata faida.

Wazo langu ni kuwa TANESCO wa charge angalau Tsh 1000/= kwa mwezi kama mamlaka nyingine zinavyofanya. Naamini idadi ya wateja wa TANESCO wanaweza kuwa zaidi ya 2m. Maana yake hapo TANESCO wanaweza kupata zaidi ya Tsh. 2B kwa mwezi na zikasaidia kwenye mambo yafuatayo.
a) Kuboresha huduma kwa kuongeza idadi ya magari na wafanyakazi ili kuhudumia wateja ipasavyo.
b) Kupata fedha za kupeleka umeme maeneo ya kimkakati hasa viongozi wa kitaifa wanapoagiza.
c) Kuboresha hali ya umeme maeneo ambayo umeme sio mzuri sana.
d) Kupata fungu la kuhakikisha miundo mbinu chakavu inafanyiwa kazi na kupata reliable power supply.
e) n.k.

Najua hapa nitashambuliwa sana lakini lengo ni kujenga nchi na si vinginevyo.

Nawasilisha.
 
Hongera kwa mada ila nakushauri Rudi field wakuambie ukweli.
Moja..tanesko wana matatizo ya kiusimamizi zaidi kuliko matatizo ya kupewa.
Pili kaangalie au wakuonyeshe maslah wanayopewa na output washukuru wao wana pelekwa na magari watumishi wengine wanajilipia nauli.

Mtazamo wangu

Kuongeza gharama za umeme kwa namna yoyote kutaongeza gharama za maisha na uzalishaji na kupandisha mfumuko wa bei. Hivyo gharama za uzalishaji kuwa juu kuliko washindaniwa kibiashara hivyo kuna kadhaa kadhaa kama vile
Wezi wa umeme kuongezeka
Matumizi ya mkaa na mafuta ya taa/petrol kuongezeka(athali mazingira )
Kupunguza kwa watu wako n uhitaji wa umeme..wengi watamua kutumia umeme binafsi au biogas nk.

Ushauri
Waongeze idadi ya sub office ambazo haitakuwa kazi(kujenga kuajili ni investment cost hata km ni kubwa ila ni fursa kiuchumi na pia kupunguza running expenses na kupanua wigo wa kipato/uchumi .
Wakishindwa Waongeze wafanya kazi na wawe wanakakagua line zao ..line nyingi hazijakaguliwa muda mrefu na manguzo mengi mabovu hiyo ya main switch ya nyumba ya mtu ni 0.0000000001%, ya matatizo halisi
Waambie watoe matope kwenye mabwawa na kufanya service mitambo yao kwa wakati na kwa viwango.
Waambie Wapitie ramani zao za line na kuboresha kilicho field na kilicho kwenye management ni tofauti line zingine zina mzigo mkubwa au mdogo mno kuliko uwezo wake /Km ilivyo kwenye makabrasha.
Waambie wakiitwa wasishikize siku mbili tatu ili waitwe wajaze over time wakifika saiti wapige kaz ya uhakika wasirudi Rudi sehem.moja mara kumi kumi.

Mengine nitakuja baadae kujazia.. alisikika chizi mmoja aliporuhusiwa kutoa maoni
 
Kmmk
 
Kuajiriwa juzi tu umeanza kuwa na kiburi na majivuno, hapa ni Duniani hakuna mwenye makazi ya kudumu, hata mngejikusanyia mabilioni ya dunia nzia lazima tu ungeonekana haujakamilika na unauhitaji, Mungu akisamehe kinywa na akili yako
 
"Kuna watu wanafikiri kwa kutumia makalio".....alisikika mbunge huyo mstaafu
 
Mkuu sahau! watanzania kujitolea hilo suala sahau kabisa, tembelea shule za msingi na sekondari ndio utajua akili ya watanzania ni kiwango gani.
Ukitaka kujuwa uwezo wa kufikiri wa jamii angalia shule zao, binafsi huwa nachukilia watanzania sisi ni wadumavu wa akili kuliko mataifa mengi ya Afrika.
Watanzania wapo tayari wajenge msikiti/kanisa wakati shule hazina madirisha na mabati yanavuja.
Mtanzania yupo tayari mtoto wake ashinde njaa shule kwa sababu serikali haitoi chakula shule, yeye hawezi kuchangia anataka chakula cha bure shuleni.
Nilitegemea watu wahoji matumizi halali ya pesa zinazokusanywa na Tanesco, je pesa haziibiwi na wachache, je hakuna mianya ya upotevu na si kupinga shirika kukusanya na kujiendesha.
Wakati hoja ya bandari ya Bagamoyo imeibuka binafsi nikawaza, hivi kama watu wanaishuku china katika huo mkataba, je watanzania hawawezi kujichanga kwa umoja wao kukusanya hizo trilioni 21 hata kama itachukua miaka 5., je kampuni moja ya china inaweza kuwashinda watanzania wote !
Sasa mtoa mada napata majibu kuwa watanzania hawapo tayati kujenga nchi yao kwa kutoa visingizio vya hovyo hovyo.
Chaji ya Huduma ilitakiwa isamehewe kwa wazee, wagonjwa na na sio vijana wenye nguvu wanataka mtelemko.
Kijana mzima unapinga kuchangia buku au 2000 kwa maendelea ya Taifa lako, unataka Taifa lijengwe ma nani?
 
Hongera kwa mada ila nakushauri Rudi field wakuambie ukweli.
Moja..tanesko wana matatizo ya kiusimamizi zaidi kuliko matatizo ya kupewa.
Pili kaangalie au wakuonyeshe maslah wanayopewa na output washukuru wao wana pelekwa na magari watumishi wengine wanajilipia nauli.

Mtazamo wangu

Kuongeza gharama za umeme kwa namna yoyote kutaongeza gharama za maisha na uzalishaji na kupandisha mfumuko wa bei. Hivyo gharama za uzalishaji kuwa juu kuliko washindaniwa kibiashara hivyo kuna kadhaa kadhaa kama vile
Wezi wa umeme kuongezeka
Matumizi ya mkaa na mafuta ya taa/petrol kuongezeka(athali mazingira )
Kupunguza kwa watu wako n uhitaji wa umeme..wengi watamua kutumia umeme binafsi au biogas nk.

Ushauri
Waongeze idadi ya sub office ambazo haitakuwa kazi(kujenga kuajili ni investment cost hata km ni kubwa ila ni fursa kiuchumi na pia kupunguza running expenses na kupanua wigo wa kipato/uchumi .
Wakishindwa Waongeze wafanya kazi na wawe wanakakagua line zao ..line nyingi hazijakaguliwa muda mrefu na manguzo mengi mabovu hiyo ya main switch ya nyumba ya mtu ni 0.0000000001%, ya matatizo halisi
Waambie watoe matope kwenye mabwawa na kufanya service mitambo yao kwa wakati na kwa viwango.
Waambie Wapitie ramani zao za line na kuboresha kilicho field na kilicho kwenye management ni tofauti line zingine zina mzigo mkubwa au mdogo mno kuliko uwezo wake /Km ilivyo kwenye makabrasha.
Waambie wakiitwa wasishikize siku mbili tatu ili waitwe wajaze over time wakifika saiti wapige kaz ya uhakika wasirudi Rudi sehem.moja mara kumi kumi.

Mengine nitakuja baadae kujazia.. alisikika chizi mmoja aliporuhusiwa kutoa maoni
Hao wafanyakazi watawalipa nini mku ?.
Watanzania tufanyeni kazi tuijenge nchi kwa nini tunataka huduma zaburebure tu.
Je ukimwita fundi aje acheki system ya umeme humlipi hela?
Tuache siasa za elimuu bure .
Service charge inatakuwa ila isiwe kubwa ya kuumiza.
Tunataka ifike wakati Tanesco wasimike nguzo bila kusubiri watu, nguzo ziwasubiri wat sio watu wasubiri nguzo za umeme.
 
Angalia: Natumia umeme wa sh 9,000 kila mwezi lkn siku 1 tanesco/ mawakala walikuwa wanashida ya mtandao tukalazimika kununua umeme mara 3 lkn hatupati unit mwishowe tukaenda tanesco wakatatua tatizo lkn tukawa tumepata unit ndogo sana, tulipowauliza tanesco wakasema umevuka kiwango cha matumizi kwa mwezi na wakasema tutakurejesha kwenye hali ya kawaida baada ya miezi 6, sasa jiulize kwa nini nidhurumiwe miezi 6 yote ? je kwa nchi nzima wanadhurumu watu wangapi? Angalia unapotaka huduma ya kuhamisha nguzo unadhani gharama wanazokupigia ni sahihi? kuhamisha nguzo kwa hatua 1 au 2 unaweza aambiwa ni sh 400,000 wakati hualisia haizidi sh50,000. Tanesco gharama zao ni za kiwiziwizi hazina uhalisia wowote.
 
Huna tofauti na yule mbunge zuzu alotoa hoja ya kuanzishwa kwa kodi ya uzalendo.
 
Mna roho mbaya hapo kadegree kamoja tuu na hata vieti hujawahi panda ukija kupanda vieiti utawakumbuka vijijini huko ambako hata hiyo elfu tano ya kupata mlo inawasumbua ndio unakuja na hoja hizo sema sishangai Tanzania imesomesha wageni wengi sana na wengine ndio watoa maamuzi wana roho mbaya mno na ya kikatili Kama yako...
 
Back
Top Bottom