Ushauri: TANESCO rudisheni Service Charges

Wazo langu ni kuwa TANESCO wa charge angalau Tsh 1000/= kwa mwezi kama mamlaka nyingine zinavyofanya. Naamini idadi ya wateja wa TANESCO wanaweza kuwa zaidi ya 2m. Maana yake hapo TANESCO wanaweza kupata zaidi ya Tsh. 2B kwa mwezi na zikasaidia kwenye mambo yafuatayo.
Let me guess...

Itakuwa TANESCO wanakujia mara kwa mara ili uwakopeshe pesa za kuendeshea shughuli zao...

...Aidha, pamoja na kukujia mara kwa mara na wewe kuwakopesa, inaelekea wanakuwa waziti kukulipa pesa zako!!

Kama ilivyo, kila mtu ana kiwango chake cha uvumilivu, na wewe inaelekea umeshawachoka TANESECO....

...Baada ya wewe kuchoshwa na TANESCO na tabia yao ya kutokukulipa mabilioni yako, kwa uzalendo mkubwa unawashauri wa TANESCO warudishe service charges ili iwasaidie kujiendesha, na ikiwezekana surplus waitumie kukulipa pesa zako!

Si nimepatia ndugu..... ebo! Kumbe unajiita Hardlife

Halafu sijui kwanini kama njaa inakuuma kweli kweli wala huwezi kupata hamu ya ugali maharage, au ugali mchicha... yaani hapo lazima utamani chips kuku, na pepsi ya bariiiiiiidi, na pili pili ya kutafunia!
 
Miaka ya nyuma kidogo TANESCO walikuwa wana charge Tsh. 7,000/= kwa mwezi kama Service Charge kwa wateja wake. Lakini ilikuja kufutwa kwakuwa ilionekana ni mzigo kwa watumiaji wa umeme hasa wale wa Tariff 1 na Tariff 0 kwakuwa ndio wateja zaidi ya 90% ya wateja wote wa TANESCO. Hii nikiri kwamba ulikuwa ni mzigo mkubwa sana kwa watumiaji wa umeme.

Katika uchunguzi wangu naona TANESCO wanajiendesha kwa gharama kubwa sana katika kuhudumia wateja wake maeneo mbalimbali nchini. Mfano mteja anaweza akawa yupo umbali wa Kilometre 100 kutoka ofisi zilipo na akatoa taarifa kuwa hana umeme. TANESCO wataenda kumhudumia na ajabu wanaenda kukuta ni Circuit Breaker tu imetrip. Hapo go and return umeenda 200km. Kwa gari yenye burning rate ya 5kms/l maana yake hapo umetumia litre 40. Let say litre 1 ni Tsh 2000.

Maana yake umetumia Tsh 80,000/= kwenda kumhudumia mteja tena wa Tariff 0 ambaye maximum ananunua umeme wa Tsh 9000 kwa mwezi. Hapo nimepigia mteja mmoja wa direction moja na pia gharama za wear and tear za gari hazijapigwa, gharama za kusogeza odometer karibu na service hazijapigwa. Sasa katika hili jaribu kuzidisha na magari yote Tanzania uone gharama zake. Hii kwangu mimi inachelewesha maendeleo kwa TANESCO hata kama wanapata faida.

Wazo langu ni kuwa TANESCO wa charge angalau Tsh 1000/= kwa mwezi kama mamlaka nyingine zinavyofanya. Naamini idadi ya wateja wa TANESCO wanaweza kuwa zaidi ya 2m. Maana yake hapo TANESCO wanaweza kupata zaidi ya Tsh. 2B kwa mwezi na zikasaidia kwenye mambo yafuatayo.

a) Kuboresha huduma kwa kuongeza idadi ya magari na wafanyakazi ili kuhudumia wateja ipasavyo.

b) Kupata fedha za kupeleka umeme maeneo ya kimkakati hasa viongozi wa kitaifa wanapoagiza.

c) Kuboresha hali ya umeme maeneo ambayo umeme sio mzuri sana.

d) Kupata fungu la kuhakikisha miundo mbinu chakavu inafanyiwa kazi na kupata reliable power supply.

e) n.k.

Najua hapa nitashambuliwa sana lakini lengo ni kujenga nchi na si vinginevyo.

Nawasilisha.
Hii bangi tu
 
Kwanini 100km, Chalinze wahudumie morogoro mjini! Wapi huko kwenye umbali mrefu hivo? Na sehemu kama hizo zinaweza kuwa ngapi?
 
TANESCO hawahawa waliokuwa wanajilipa mpaka milioni 60 bonus ya mtu mmoja mwisho wa mwaka?

Ukitaka umeme unanunua nguzo zao?

Ukiwa na kiwanda kikubwa unanua Transfoma na hawakurudishii gharama zao wakati huohuo umeme wao unanunua?

Unahitaji kujua kwamba matatizo ya Tanesco ni makubwa zaidi ya hio service charge.
 
Hiyo service charge tunalipa sema wewe huko field ulienda kupoteza muda tu, means kwa sasa baadhi ya garama hazijawekwa kama zamani, but now tunalipa kwa manunuzi ya umeme, angalia yake makato baada ya kununua umeme ndipo utajua.
 
Utakua mchawi wewe, vyuma vimekaza alafu unajiongelesha utumbo, kama unaitaka hiyo service charge ww Nenda kawaombe tanesco wakuekee mjaalaana mkubwa, unakatwa na wachawi
 
unatoa mbwa wewe itakua unakaa kwenu bado kodi shikamoo au umeachiwa nyumba ya urithi na huchangii huduma za umeme hapo kwenu
 
Miaka ya nyuma kidogo TANESCO walikuwa wana charge Tsh. 7,000/= kwa mwezi kama Service Charge kwa wateja wake. Lakini ilikuja kufutwa kwakuwa ilionekana ni mzigo kwa watumiaji wa umeme hasa wale wa Tariff 1 na Tariff 0 kwakuwa ndio wateja zaidi ya 90% ya wateja wote wa TANESCO. Hii nikiri kwamba ulikuwa ni mzigo mkubwa sana kwa watumiaji wa umeme.

Katika uchunguzi wangu naona TANESCO wanajiendesha kwa gharama kubwa sana katika kuhudumia wateja wake maeneo mbalimbali nchini. Mfano mteja anaweza akawa yupo umbali wa Kilometre 100 kutoka ofisi zilipo na akatoa taarifa kuwa hana umeme. TANESCO wataenda kumhudumia na ajabu wanaenda kukuta ni Circuit Breaker tu imetrip. Hapo go and return umeenda 200km. Kwa gari yenye burning rate ya 5kms/l maana yake hapo umetumia litre 40. Let say litre 1 ni Tsh 2000.

Maana yake umetumia Tsh 80,000/= kwenda kumhudumia mteja tena wa Tariff 0 ambaye maximum ananunua umeme wa Tsh 9000 kwa mwezi. Hapo nimepigia mteja mmoja wa direction moja na pia gharama za wear and tear za gari hazijapigwa, gharama za kusogeza odometer karibu na service hazijapigwa. Sasa katika hili jaribu kuzidisha na magari yote Tanzania uone gharama zake. Hii kwangu mimi inachelewesha maendeleo kwa TANESCO hata kama wanapata faida.

Wazo langu ni kuwa TANESCO wa charge angalau Tsh 1000/= kwa mwezi kama mamlaka nyingine zinavyofanya. Naamini idadi ya wateja wa TANESCO wanaweza kuwa zaidi ya 2m. Maana yake hapo TANESCO wanaweza kupata zaidi ya Tsh. 2B kwa mwezi na zikasaidia kwenye mambo yafuatayo.

a) Kuboresha huduma kwa kuongeza idadi ya magari na wafanyakazi ili kuhudumia wateja ipasavyo.

b) Kupata fedha za kupeleka umeme maeneo ya kimkakati hasa viongozi wa kitaifa wanapoagiza.

c) Kuboresha hali ya umeme maeneo ambayo umeme sio mzuri sana.

d) Kupata fungu la kuhakikisha miundo mbinu chakavu inafanyiwa kazi na kupata reliable power supply.

e) n.k.

Najua hapa nitashambuliwa sana lakini lengo ni kujenga nchi na si vinginevyo.

Nawasilisha.
Hesabu hizo piga kwa mteja aliye nje ya ofisi ya TANESCO
 
Mkuu sahau! watanzania kujitolea hilo suala sahau kabisa, tembelea shule za msingi na sekondari ndio utajua akili ya watanzania ni kiwango gani.
Ukitaka kujuwa uwezo wa kufikiri wa jamii angalia shule zao, binafsi huwa nachukilia watanzania sisi ni wadumavu wa akili kuliko mataifa mengi ya Afrika.
Watanzania wapo tayari wajenge msikiti/kanisa wakati shule hazina madirisha na mabati yanavuja.
Mtanzania yupo tayari mtoto wake ashinde njaa shule kwa sababu serikali haitoi chakula shule, yeye hawezi kuchangia anataka chakula cha bure shuleni.
Nilitegemea watu wahoji matumizi halali ya pesa zinazokusanywa na Tanesco, je pesa haziibiwi na wachache, je hakuna mianya ya upotevu na si kupinga shirika kukusanya na kujiendesha.
Wakati hoja ya bandari ya Bagamoyo imeibuka binafsi nikawaza, hivi kama watu wanaishuku china katika huo mkataba, je watanzania hawawezi kujichanga kwa umoja wao kukusanya hizo trilioni 21 hata kama itachukua miaka 5., je kampuni moja ya china inaweza kuwashinda watanzania wote !
Sasa mtoa mada napata majibu kuwa watanzania hawapo tayati kujenga nchi yao kwa kutoa visingizio vya hovyo hovyo.
Chaji ya Huduma ilitakiwa isamehewe kwa wazee, wagonjwa na na sio vijana wenye nguvu wanataka mtelemko.
Kijana mzima unapinga kuchangia buku au 2000 kwa maendelea ya Taifa lako, unataka Taifa lijengwe ma nani?
Mkuu ni kweli mchango wako, lakini chuki na povu jingi ulionalo labda ni matokeo ya watoa huduma wenyewe ni kwa namna gani wamekuwa wakiwahudumia watanzania? hapa nahisi ndio penye chuki halisi ya watanzania, ilifika mahala umeme ulionekana ni anasa wakati ni huduma muhimu, ilifika mahala ukilipia umeme utasahau maana iabidi uwabembelezeeeee na rushwa uwape ili waje kukufungia umeme, likitokea tatizo la nguzo kuanguka au waya kukatika watakuja katika muda watakao ilifika mahala baadhi ya staffs walijiona ka miungu watu hii kitu inauma sana na ndiyo inacreate chuki baina ya mtoa huduma na wapewa huduma na hii ndio maana unaona povu la kumwaga katika uzi huu, na sio watoa huduma hawa tu angalia hata watoa huduma wa kimiminika nao pia wako hovyo sana, sasa nambie ni nani atakubali kuwachangia ili waendelee ilhali huduma ni mbovu na wengi baadhi yao wametanguliza uchu wa rushwa.
Zamani kulikuwa na shirika moja la vilongalonga hawa nao walijisahau sana lakini wakaletewa wapinzani oooohh saa hizi kila siku wanabuni namna bora ya kujiendesha na washukuru bado wako mikononi, otherwise tungeshawasahau.
Watanzania si kwamba hawapendi maendeleo au hawapendi kuchangia maendeleo ya nchi lakini kuna vitu vinawakwaza mnooooo mpaka watu wakuwa na roho ngumu kuliko jiwe.
Ni mtazamo wangu tu.
 
Hao wafanyakazi watawalipa nini mku ?.
Watanzania tufanyeni kazi tuijenge nchi kwa nini tunataka huduma zaburebure tu.
Je ukimwita fundi aje acheki system ya umeme humlipi hela?
Tuache siasa za elimuu bure .
Service charge inatakuwa ila isiwe kubwa ya kuumiza.
Tunataka ifike wakati Tanesco wasimike nguzo bila kusubiri watu, nguzo ziwasubiri wat sio watu wasubiri nguzo za umeme.
Mkuu ni kweli, lakini ili hawa watoa huduma akili ziwakae sawa yabidi kuwe na ushindani, hawa jamaa hawana mshindani kwa hiyo usemayo ya kusimika nguzo na kadhalika ni lazima uwabembeleze kwa kuwa huna pa kwenda, nasistiza tena kwa msistizo hawa watafutiwe mwenza halafu kuwekwe mazingira bora ya ushindani kama hawatobadilika tutawasahau.
 
Ishauri serikali irudishe kodi ya kichwa maana serikali inatumia hela nyingi sana kujenga barabara, hospital, shule n.k au sio ndugu.
 
Mkuu hili shirika kumbuka halifanyi biashara badala yake ni huduma ivo hii kampuni sio business oriented kuna mambo mzigo mkubwa serikali inabeba imagine mtu analipa shirika 27000 na anapata service hizi
-Survyeying
-Meter
-Conductors
-Other accessories
ambapo hio 27k haiwezi kununua hata other accessories ukiachia labor charges na Transport Charges yani ni hatari
Bado JPM alitaka wapeleke dividend wakati Shirika kujiendesha lenyewe haliwezi
 
Miaka ya nyuma kidogo TANESCO walikuwa wana charge Tsh. 7,000/= kwa mwezi kama Service Charge kwa wateja wake. Lakini ilikuja kufutwa kwakuwa ilionekana ni mzigo kwa watumiaji wa umeme hasa wale wa Tariff 1 na Tariff 0 kwakuwa ndio wateja zaidi ya 90% ya wateja wote wa TANESCO. Hii nikiri kwamba ulikuwa ni mzigo mkubwa sana kwa watumiaji wa umeme.

Katika uchunguzi wangu naona TANESCO wanajiendesha kwa gharama kubwa sana katika kuhudumia wateja wake maeneo mbalimbali nchini. Mfano mteja anaweza akawa yupo umbali wa Kilometre 100 kutoka ofisi zilipo na akatoa taarifa kuwa hana umeme. TANESCO wataenda kumhudumia na ajabu wanaenda kukuta ni Circuit Breaker tu imetrip. Hapo go and return umeenda 200km. Kwa gari yenye burning rate ya 5kms/l maana yake hapo umetumia litre 40. Let say litre 1 ni Tsh 2000.

Maana yake umetumia Tsh 80,000/= kwenda kumhudumia mteja tena wa Tariff 0 ambaye maximum ananunua umeme wa Tsh 9000 kwa mwezi. Hapo nimepigia mteja mmoja wa direction moja na pia gharama za wear and tear za gari hazijapigwa, gharama za kusogeza odometer karibu na service hazijapigwa. Sasa katika hili jaribu kuzidisha na magari yote Tanzania uone gharama zake. Hii kwangu mimi inachelewesha maendeleo kwa TANESCO hata kama wanapata faida.

Wazo langu ni kuwa TANESCO wa charge angalau Tsh 1000/= kwa mwezi kama mamlaka nyingine zinavyofanya. Naamini idadi ya wateja wa TANESCO wanaweza kuwa zaidi ya 2m. Maana yake hapo TANESCO wanaweza kupata zaidi ya Tsh. 2B kwa mwezi na zikasaidia kwenye mambo yafuatayo.

a) Kuboresha huduma kwa kuongeza idadi ya magari na wafanyakazi ili kuhudumia wateja ipasavyo.

b) Kupata fedha za kupeleka umeme maeneo ya kimkakati hasa viongozi wa kitaifa wanapoagiza.

c) Kuboresha hali ya umeme maeneo ambayo umeme sio mzuri sana.

d) Kupata fungu la kuhakikisha miundo mbinu chakavu inafanyiwa kazi na kupata reliable power supply.

e) n.k.

Najua hapa nitashambuliwa sana lakini lengo ni kujenga nchi na si vinginevyo.

Nawasilisha.

Hoja yako ime base upande mmoja hivyo haina mashiko
UNGEANZA KUTUELEZA MAPATO YA TANESCO KWA MWEZI NI KIASI GANI NA MGAWANYO WAKE
Ilitujiridhishe kwanza kile kinachokusanywa kinatumika vizuri na sio kinaishia kwenye .......................
wakati mwalimu analipwa kwenye 450,000 halafu unataka kumuongezea tena mzigo
 
Mkuu sahau! watanzania kujitolea hilo suala sahau kabisa, tembelea shule za msingi na sekondari ndio utajua akili ya watanzania ni kiwango gani.
Ukitaka kujuwa uwezo wa kufikiri wa jamii angalia shule zao, binafsi huwa nachukilia watanzania sisi ni wadumavu wa akili kuliko mataifa mengi ya Afrika.
Watanzania wapo tayari wajenge msikiti/kanisa wakati shule hazina madirisha na mabati yanavuja.
Mtanzania yupo tayari mtoto wake ashinde njaa shule kwa sababu serikali haitoi chakula shule, yeye hawezi kuchangia anataka chakula cha bure shuleni.
Nilitegemea watu wahoji matumizi halali ya pesa zinazokusanywa na Tanesco, je pesa haziibiwi na wachache, je hakuna mianya ya upotevu na si kupinga shirika kukusanya na kujiendesha.
Wakati hoja ya bandari ya Bagamoyo imeibuka binafsi nikawaza, hivi kama watu wanaishuku china katika huo mkataba, je watanzania hawawezi kujichanga kwa umoja wao kukusanya hizo trilioni 21 hata kama itachukua miaka 5., je kampuni moja ya china inaweza kuwashinda watanzania wote !
Sasa mtoa mada napata majibu kuwa watanzania hawapo tayati kujenga nchi yao kwa kutoa visingizio vya hovyo hovyo.
Chaji ya Huduma ilitakiwa isamehewe kwa wazee, wagonjwa na na sio vijana wenye nguvu wanataka mtelemko.
Kijana mzima unapinga kuchangia buku au 2000 kwa maendelea ya Taifa lako, unataka Taifa lijengwe ma nani?
Ishaurini serikali basi irudishe kodi ya kichwa (kila raia alipe kodi) ili tupate maendeleo makubwa kama mnafikiri maendeleo yanapatikana zaidi kwa kuwatoza raia.
Unanunua umeme na unalipa VAT 18%, REA 3% na EWURA 1%.Watu wanachangia maendeleo huko vijijini kwa kulipa hiyo REA 3% bila kelele lakini bado mnawaona sio wazalendo na uzalendo kwenu ni kuwatoza tu raia zaidi na zaidi.
 
Hahahhahaha
255652209235_status_144e461da9474005900cf67c319bcfc3.jpg
 
Back
Top Bottom