Ushauri tafadhali - Toyota Vitz, Duet, Allex, RunX, Suzuki SWIFT,

Ipsum/Gaia ya mwaka gani?

Ipsum na Gaia zinafanana sana, tofauti kubwa ipo tu kwenye mwonekano wake. Kuna zenye 2,000cc na 2,400cc kutegemeana na mwaka. Za miaka ya nyuma kidogo nyingi zina engine ya 3S ambayo ndio inatumika kwenye RAV4 (za zamani).

Opa ni nzuri pia, ingawa ipo chini sana. Huwezi itumia kwenye barabara mbovu mbovu. Opa inatumia engine ileile kama ya Runx au IST na ipo poa kabisa. Ni VVTi.

Kuna watu wanasema OPA ni mayai sana (so delicate) but me binafsi sina uhakika na hilo.
nimependa michango yako, inaelekea ww ni mtaaalam wa magar
 
Kwa kiasi chake mkuu. Karibu sana

Mkuu nimepata bonge la shule nilikuwa na mpango wa kununua swift below 2005 itabidi nijipange vp kuhusu toyota alteza? Au toyota progress vipuli vinapatikana kwa bei nzuri?
 
I think Jamii forum is more than an ordinary University
I real Enjoy thread za namna hii kulikoni zile za "JAMANI NIMEAMKA WIFE KANUNA" Nifanyeje?
Big up all
 
off all the list, hakuna gari apo. chukua toyota corrola,sprinter au Corsa. (cc 1300)
Lazima ukue kimtazamo, we kama hujaona waache wenzio wanaojua wamshauri, this is uncivilized habits achana nayo, inawezekana aliyeomba ushauri huko ndo uwezo wake ulipo. Ebu kuwa kidogo.
 
Mkuu nimepata bonge la shule nilikuwa na mpango wa kununua swift below 2005 itabidi nijipange vp kuhusu toyota alteza? Au toyota progress vipuli vinapatikana kwa bei nzuri?

Mkuu, inategemea na mfuko wako.

Ila mara kumi Altezza, hiyo Progress ni moto wa kuotea mbali. Engine size ya Progress inaanzia 2,500 hadi 3,000cc. Ni six cylinder, halina mzaa kwenye foleni. Kama wewe ni mtu wa budget lazima litakushinda - litakua linapigwa vumbi tu nyumbani.

Altezza kuna zenye 2,000cc, 2,500cc hadi 3,000cc - so inategema umechagua lipi.

Body parts kwa zote mbili ni gharama. Ila kama ukichukua lenye engine ya 3S (Altezza) ulaji wa mafuta sio mbaya sana.

Altezza hata me mwenyewe naipenda. Ila ni gharama kidogo mkuu kulinunua na kulihudumia pia. Ila kama mfuko unaruhusu, we vuta kitu nyumbani.
 
Kuna mdau ameni PM kuhusu ni gari gani achague kati ya Subaru Forester na Nadia. So I thought I would share it with all of you and get more input from the entire community.

Subaru Forester ni gari ngumu, kama ilivyo RAV 4 (Engine 3S-FE model 1994 - 2000, 1997 - 2003 RAV4 EV). Spare zake kwa wastani zipo juu, zaidi hata ya RAV4.

Kwa kifupi, Subaru Forester ina compete na RAV4, na zote zimetolewa almost at the same time.

Subaru Forester ina engine kubwa, 2500cc (RAV4 2000cc), hivyo lazima ujiandae kuweka mafuta ya kutosha, ukizingatia na foleni zetu za bongo.

Engine kubwa ni nzuri kwa safari, au kama una mizunguko ambayo hakuna foleni. Kama kula foleni, injini kubwa itakula mafuta mengi zaidi ya engine ndogo. Unapochagua ukubwa wa engine, zingatia matumizi na uwezo wako kiuchumi.

Kwa kifupi, kwa mtu wa kipato cha chini anaeanza maisha, Subaru Forester si gari ya kununua period.

Toyota Nadia.

Nadia inatumia engine ya D4, na hii ni pamoja na RAV4 (Engine 1AZ 2000 - 2005) na gari nyinginezo.
Kwa kifupi, D4 engine ni technologia mpya, mafundi bongo hakuna.

In short, KAA MBALI na D4 engine.

Soma hizi links:

Toyota Nadia with a D4 engine - AA New Zealand

https://www.jamiiforums.com/matangazo-madogomadogo/49023-mtaalam-wa-engine-za-d4.html

Bottom line:

Kama unaanza maisha, kati ya Subaru Forester na Nadia hakuna la kununua hapo.

Kama una budget ya kutosha na uchumi mzuri, Forester in not a money wester.

You are welcome,

Ramthods

Mkuu Ramthods nakupa big up sana maana hapo penye red umegusa wengi mno. Hebu tupe (twaomba mkuu) shule zaidi hususani inayowalenga watu ambao wanaangukia kwenye red; unawashauri waanze na gari gani?
Asante
 
Mkuu,

Sina uhakika kama tayari ushanunua gari, ila kwa hayo magari uliyoyalist, ushauri wangu ni kama ifuatavyo:

Toyota Vitz
Ni nzuri kwa utumiaji wa mafuta. Spea zipo ila bei mbaya. Sio gari imara sana kwa kifupi. Kama una hela ya kununua spea kwa gharama, ni gari nzuri.

Duet
Hili sikushauri hata kidogo. Lina 3 pistons. Hii engine inasumbua na kuna wakati inaweza kuleta mlio fulani kwenye engine (kawaida ya 3 pistons engine) ambao kuurekebisha ni ngumu (au haiwezekani kabisa). Utaangaika tu kwa mafundi.

Utumiaji wake wa mafuta ni mzuri, ila engine ni kimeo.

Allex
Hii sijawahi kuigusa, hivyo sina uzoefu wa spea wala uimara wake. Haina tofauti na toyota RunX, zote zinatumia engine sawa (inategemea na model lakini)

RunX
Hii ni Corolla Runx. Ni nzuri, ila sina uhakika na ubora wa engine wala upatikanaji wa spea. Ila, kama ilivyo kawaida, gari mpya spea zake ni ngumu kidogo kupata na bei huwa juu. Hii inawezekana kwa Allex na RunX, ingawa sina uhakika.

Pia, kama unatazamia kununua Allex au RunX, angalia pia na IST. Zote zinatumia Engine sawa, na bei zake zinakaribiana sana, lakini zipo juu. FOB ya chini ni around USD 3,600 (kwa gari nzuri)

Suzuki SWIFT
Achana na hii gari mkuu. Spea ni ngumu kupata.

Inatumia mafuta vizuri, na ni gari nzuri. Ishu itakupata kwenye spea tu.


Bottom line:

Kama mdau mmoja alivyosema hapo juu, engine ndogo ya Toyota 4E-FE ni engine bomba sana, imetulia na spea ni bei chee kila kona. Inatumika kwenye Toyota Starlet na Raum (na model nyingine nyingi tu)

Toyota Starlet ni model ya nyuma kidogo, ni nzuri, ila Raum ni ya mpya zaidi ya Starlet.

Kama unataka gari ndogo, spea zinazopatikana ki urahisi na bei nafuu, Toyota Raum is among the best options out there.

Ila, kama wewe sio mtunzaji mzuri, mlango wa nyuma unaweza kuharibika mapema. But anyway, spea zipo na ni bei nafuu.

Kazi kwako.

Ramthods

i do second.... Toyota starlet ni ngumu... Its a car for economy... Hata ubora wake ni mathubuti... Si gari nyingine zapasuka kama mabox... Yenyewe huwa inabonyea na hivyo waweza kunyoosha...,
nawasilisha hoja... Ni pm nikupe namna ya kugo abt one..
 
Umesahau Toyota Starlet (SOLEIL 4DOORS) sio REFLECT ni bomba mbaya hasa ukiweka spot tyre unasafiria popote confortable, mi ninayo SOLEIL ya mwaka 96 ila huwezi amini naipiga masafa ya Mza, Mby na Arusha haichemshi wala kupata miss, 4E FE ni njini bomba na ndizo mjapani alipotulia na kuziunda.

kwa nini reflect sio nzuri ndugu yangu??
 
Bajaji is the best aisee, kama ni ishu ya mafuta I suggest u go to this stuff
Tafadhali naombeni ushauri kwa wote wanaomiliki au waliowahi kumiliki moja kati ya gari hizi: Toyota Vitz, Toyota Duet, Toyota Allex, Toyota RunX na Suzuki Swift.

Nataka kununua gari yenye injini ndogo ( 1- 1.3 litres) na ningependa kupata uzoefu juu ya uimara wa magari haya, upatikanaji wa vipuri (spare parts) na maelezo mengine kiujumla.

Natanguliza shukrani zangu.
 
kukwepa haya yote we nunua gari mpya kabisa, achana na mitumba ukinunua unapewa na 2yrs guarantee ama kilometa 160,000 ikileta shida u get a replacement
 
Wadau vipi ulaji mafuta wa Ipsum ya 1999 engine 3S-FE? kuna mtu anataka kuniuzia odormeter 90000km?
 
Jamani hivi hizi Toyota PASSO zikoje? Zimenivutia bei nzuri na ni za miaka ya karibuni 2004-2006

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom