Ushauri: Pete ya ndoa

Nashukuru kwa ushauri wenu, binafsi sikuwa na uzoefu wa haya mambo ndiyo maana nikauliza ili nisije kukosea na kiukweli nimejifunza sana,

Nadhani Gold ya Gram 3 inaweza tosha au itakuwa ndogo?
 
kitu gold bana, una Bahati dolla imeshuka gram moja leo ni 81 058.14

kama pesa ipo mtengenezee kwa gram 9 kitu kama laki 7....

tumia pesa ikuzoe
 
Princess cut mara nyingi budget yake huwa ni kubwa [relatively speaking].

Ukiwa na muda wa ku shop around unaweza ukabahatisha bei yenye nafuu kulingana na uwezo wako.

Ila kwa uzoefu wangu, ukitaka kum 'wow' mdada basi mnunulie princess cut diamond ring.

Lakini kwanza ni lazima huyo mdada awe na exposure na ufahamu wa princess cut ni nini.

Kibongo bongo sidhani kama wengi hata wanajua hicho ni kitu gani achilia mbali uthamani wake.

Ningeweza ku suggest atafute round brilliant cut lakini....
Hii kwa hawa wetu wa manzese si balaa!
 
Back
Top Bottom