Ushauri: Nitumie mbinu gani kuongea na baba aachane na mchepuko wake?

sepema

JF-Expert Member
Jun 13, 2019
591
1,000
Wakuu salaam,

Mara kadhaa mama amekuwa akimtuhumu mzee kujihusisha kimahusiano na mama fulani ambae ni shemeji yake. Mama amejaribu kufanya jitihada za kuwaachanisha kwa njia ya mazungumzo lakini wamegoma kuachana kabisa.

Mara ya mwisho mama kajaribu kumweleza mume wa huyo mchepuko kila kitu ila cha ajabu mzee yule kaamua kumtetea mkewe kuwa hana hizo tabia na hawezi kutoka kimapenzi na mzee wangu.

Upo ushahidi wakutosha kuwa mzee anatoka na huyo mama. Baada ya kuvumilia kwa miaka mingi mama ameamua anipigie simu kunishirikisha jambo hilo. Amenambia ameamua kunishirikisha mimi kwani ni kijana wake mkubwa na kwa hali ilivyo anaweza kupoteza maisha kwa pressure hivyo niangalie nini naweza kufanya.

Nimefikiria kumchukua bimkubwa niishi nae ila nahofia familia itajigawa. Ndugu wa mzee wameongea lakini mzee habadiliki kabisa, ndio kwaanza anachochea makaa kwenye treni. Nimefikiria kumvaa baba nimweleze kuhusu hilo tatizo nakwamba aache mara moja ila nahofia reaction yake. Wakuu; huu msala na utatua vipi ili ninusuru hii ndoa ya wazee wangu ambayo imedumu kwa zaidi ya miaka 30 Sasa.

Mwisho: Ukihisi huwezi kuchangia naomba usome nakupita. Kama itakulazimu kuchangia kwa kutukana, naomba hayo matusi yaelekee kwangu ila sio kwa wazazi.

Wasalaam!
 
Wakuu salaam....
Mara kadhaa mama amekuwa akimtuhumu mzee kujihusisha kimahusiano na mama flani ambae ni shemeji yake. Mama
Mzee wako Ana tumia kilevi? Kama jibu ni YES kwangu mimi ingekuwa rahisi ....mbinu namba 2 : jaribu kuongea na mzee usiogope reaction yake vaa ujasiri kuna kitu atajifunza , mwisho kabisa zote hizo zikishindikana jaribu kwenda kwa mjumbe ... ukiwa upo na mjumbe mkajaribu kuzungumza naye pia itasaidia kitu flani ....... njia zote hizo zikofeli mpelekee ushahidi wa picha kwa mume wa huyo mama
 
Pole sana ila usimchukue mama yako vaa moyo wa ujasiri muulize huyo mzee wako kuhusu hizo tuhuma usikie atajibu nini lakini ajabu huyo baba mkubwa wako nae hakubali kama anachapiwa ni jambo la ajabu maana ilibdi iwe kesi ya UKOOO hiyo... usikurupuke
 
😂...
Sasa umchukue mke wa watu Ili iweje...

Mama achukue likizo Mzee ammiss 😂. Ukute na wewe una mke hapo akae kuangalia mwanamke mwenzie aliyekimbia mumewe!
Sema nini mkuu, Mama yako kakosea kukushirikisha haya mambo, lakini basi...
Wamama huwa wanavumilia sana ukiona kasema jua yamemshinda japo huwaga wanawapa stress watoto zisizokuwa za maana maana hayo mambo ni makubwa sana aisee....huwezi kuamua wala kusaidia majanga
 
Wakuu salaam....
Mara kadhaa mama amekuwa akimtuhumu mzee kujihusisha kimahusiano na mama flani ambae ni shemeji yake. Mama amejaribu kufanya jitihada zakuwaachanisha kwa njia ya mazungumzo lakini wamegoma kuachana kabisa.
Aisee, Atakayekufa hapo ni mzee na Wala sio Mama!!

Naendelea kuona sababu ya Wanawake kuishi muda mrefu.

Hivi Wewe kama Baba utaanzia wapi kumwambia mtoto wako kuwa Mama yake anachepuka? Tena anachepuka na fulani?

Aisee...
Mama hawezi kufa, akishalitoa hivyo hakuna pressure tena.
Si unaona kila mtu anajua?

Angekuwa Mama anachepuka hata nyie watoto msingejua
 
Ni ngumu mtu kuacha Tabia Kwa kusikiliza ushauri peke take,na umesema Mzee wako ameshauriwa na mkewe aache na amekuwa mgumu.....Kifupi ktk mahusiano anayeacha mwanamke,mwanaume haachi kirahisi km mwanake hajaamua ,hasa km utelezi anauoata kirahis kutoka Kwa huyo mchepuko

Ushauri wangu; Mfate huyo mchepuko mke wa babaako mpige mkwara mzito Sana,km ile mkwara ya Baba ubaya wa kwenye gazeti, mshinikize aachane na babaako la sivyo utamfanyia kitu kibaya sn ambacho hajawai kufanyiwa kwenye maisha yake,alafu mchimbe mkwara mwingine kwamba asimwambie Mzee wako kuhusu wewe kmfata ukamoiga biti waachane,ajifanye Tu ameamua mwenyewe kubaki na mumewe njia kuu.

Nakupa mwezi hlutakuja kutoa ushuhuda hapa wameachana
 
Mzee wako Ana tumia kilevi? Kama jibu ni YES kwangu mimi ingekuwa rahisi ....mbinu namba 2 : jaribu kuongea na mzee usiogope reaction yake vaa ujasiri kuna kitu atajifunza , mwisho kabisa zote hizo zikishindikana jaribu kwenda kwa mjumbe ... ukiwa upo na mjumbe mkajaribu kuzungumza naye pia itasaidia kitu flani ....... njia zote hizo zikofeli mpelekee ushahidi wa picha kwa mume wa huyo mama
Mzee anatumia kilevi.Inaeza kuwa njia nzur Ila changamoto nipale atakapokubaliana namimi kwa kuongozwa na kilevi kichwani.Kesho au keshokutwa anaweza aendelee
 
...
Sasa umchukue mke wa watu Ili iweje...

Mama achukue likizo Mzee ammiss . Ukute na wewe una mke hapo akae kuangalia mwanamke mwenzie aliyekimbia mumewe!
Sema nini mkuu, Mama yako kakosea kukushirikisha haya mambo, lakini basi...
Ndio maana wanaishi muda mrefu, hawaweki kitu yani.
Mambo walala walala...
 
pole sana ila usimchukue mama yako vaa moyo wa ujasiri muulize huyo mzee wako kuhusu hizo tuhuma usikie atajibu nini lakini ajabu huyo baba mkubwa wako nae hakubali kama anachapiwa ni jambo la ajabu maana ilibdi iwe kesi ya UKOOO hiyo... usikurupuke
Wanaume tunatunza mambo!! Pengine huyo Baba mkubwa anajua ila ndiyo hivyo, ni kawaida yetu kuwalindia heshima wake zetu, kitu ambacho wao hawawezi kabisa yani!!
 
...
Sasa umchukue mke wa watu Ili iweje...

Mama achukue likizo Mzee ammiss . Ukute na wewe una mke hapo akae kuangalia mwanamke mwenzie aliyekimbia mumewe!
Sema nini mkuu, Mama yako kakosea kukushirikisha haya mambo, lakini basi...
Hata Mimi nilihisi hakupaswa kunambia.Ila ndohivyo kashanambia..likitokea baya atahisi sikufanya chochote kumsaidia.
 
Ni ngumu mtu kuacha Tabia Kwa kusikiliza ushauri peke take,na umesema Mzee wako ameshauriwa na mkewe aache na amekuwa mgumu.....Kifupi ktk mahusiano anayeacha mwanamke,mwanaume haachi kirahisi km mwanake hajaamua ,hasa km utelezi anauoata kirahis kutoka Kwa huyo mchepuko

Ushauri wangu;
Mfate huyo mchepuko mke wa babaako mpige mkwara mzito Sana,km ile mkwara ya Baba ubaya wa kwenye gazeti, mshinikize aachane na babaako la sivyo utamfanyia kitu kibaya sn ambacho hajawai kufanyiwa kwenye maisha yake,alafu mchimbe mkwara mwingine kwamba asimwambie Mzee wako kuhusu wewe kmfata ukamoiga biti waachane,ajifanye Tu ameamua mwenyewe kubaki na mumewe njia kuu.

Nakupa mwezi hlutakuja kutoa ushuhuda hapa wameachana
Yaah afanye hivyoo sema mzee wake kama anakula kweli atamuuliza lakini pia anaweza muuliza sababu dogo atakua kavunja heshima kwa huyo maza... hizi kesi wazee ni kuwaacha tu huawaga siku wanaamua kuacha tu wenyewe japo ni ngumu ila ukweli huyu jamaa hawezi badilisha chochote
 
Wakuu salaam....
Mara kadhaa mama amekuwa akimtuhumu mzee kujihusisha kimahusiano na mama flani ambae ni shemeji yake. Mama amejaribu kufanya jitihada zakuwaachanisha kwa njia ya mazungumzo lakini wamegoma kuachana kabisa.
Acha kuingilia maisha ya wazazi wako!!
hizo ni shida zao sio zako EBOO!
ingilia kwenye maisha ya wazazi wako pale panapokuwa na shida za kiuchumi ama magonjwa ili usaidie lkn kuweka pua yako mbele mbele kwenye maswala kama haya huo ni ushuzi!
 
Mzee anatumia kilevi.Inaeza kuwa njia nzur Ila changamoto nipale atakapokubaliana namimi kwa kuongozwa na kilevi kichwani.Kesho au keshokutwa anaweza aendelee
Mkuu hii battle ni ngumu, usijaribu kumtamkia baba yako lolote kuhusu haya mahusiano.

Kama una akili, cheza na huyo mchepuko(japo si vizuri).

Tumia mbinu za kijeshi na kiintelijensia!! Bila kuathiri uhusiano wa Baba na Mama.
 
Back
Top Bottom