Wazee tufundishane hapa!
Kwenye maisha yetu Kama waume hii inatokea Mara nyingi tu. Mzee penzi limenoga kwa mchepuko, mara tu mimba hii hapa.
Wengine wanakataa ujauzito na mahusiano yanakufa!
Wengine wanaamua kuondoa mimba fasta, ili maisha yaendelee!
Wengine wanalea ujauzito na mtoto kwa Siri!
Lakini hata hivyo dunia Haina Siri, mwisho wa siku katoto kanatambaa, Mara kanatembea, ohooo hakoo kanaingia darasa la kwanza!
Mke amepata taarifa ya uwepo wa mtoto wa pembeni, Mara ooh katoto kameletwa ndani ya nyumba!
Hapa ndipo naleta hoja yangu!
Nini ulazima wa kumleta mtoto huyu ndani ya nyumba ya mke?
Hivi mama yake ameshindwa kumlea kweli, akipewa sapoti zote na baba husika?
Unamleta kwa mkeo apate Nini chenye ulazima wa kibinadamu atakachokikosa
kwenye makazi ya mama yake?
Je, baba utashindwa kumpa huduma za chakula, mavazi, tiba na Elimu akiwa mikononi mwa mama yake?
Mfano mume aliyeoa wake wawili au watatu ambao wanaishi makazi tofauti, mbona anawalea watoto wake wote wakiwa makazi tofauti na hadhi ya baba inabaki palepale?
Naomba mwenye kujua Jambo hili atamke, sababu Mimi naona hii haijakaa poa!
Hata baba yetu Daudi, yule mfalme mkuu tunayemuenzi kwa kuifanya taasisi ya michepuko kuwa na heshima, hakuwa na desturi ya kuchukuwa watoto wa mwanamke huyu na kuwapeleka kwa mwanamke yule!
Mwanamke azae, alee na kukuza watoto wake aliowazaa akisapotiwa kwa asilimia zote na baba mzazi!
Naomba kuwasilisha!