g vizy
JF-Expert Member
- Jan 5, 2016
- 896
- 977
- Thread starter
- #41
Asante mkuu ntajitahidi kufanya hvyo na kuhakikishia ntaleta mrejesho hali yake ikitengamaaNimesoma huu uzi, from my lower understanding of Psychology naweza kuelezea hivi.
Kuna tatizo maarufu sana kwa watu wazima, linaitwa PARANOIA, ni tatizo la kiakili yaani "Hali ya juu ya kujishuku", hii hutokea kwa watu wazima wafuatao;
1. Wale ambao walifeli baadhi ya mambo katika maisha yao, na watu wengine wakawa wanajua 'Failures' zao. Mara nyingi hawa, huwa wanawindwa na mawazo ya majuto "Hallucinations" ambapo anahisi kama watu wengine pia wanamsema kama yeye anavyojuta. Hii inapelekea mtu kuona hakuna sababu ya kuendelea kuishi, kwa sababu maisha ni muingiliano (Interaction) kama unahisi wanaokuzunguka wanakusengenya, kuna haja gani kuishi? Ni rahisi mtu kutaka kujitoa uhai.
2. Wale wenye magonjwa ya kudumu; kwa uzoefu wangu, watu hawa pamoja na walemavu ni makundi yanayoongoza kuwa na shida hii (Paranoia); kwa kuwa hujitofautisha na wengine, hivyo husisi wametengwa, japo huenda ikawa kweli ama yeye ndiye akawa amejitenga (Self Isolation), ndio maana, ARVs hazikutosha kutatua shida yake kiafya, matibabu ya kihisia ni salama zaidi na ya kudumu, tunatibu hisia kupitia Muingiliano, ndio mana nikutoe kidogo kwenye mada, kama mkeo upo nae mbali, muingiliano hushuka, hisia hupotea, mapenzi pia yanakufa. Nagusia tu
Sasa basi, kitendo cha watoto wake wa kuzaa kuwa mbali, kunachochea kushuka kwa muingiliano, kushuka kwa hisia, hivyo kupoteza tumaini. No hope, no reason to live.
Kwa nini hasa asingizie wengine?
Turudi hapo hapo kwenye somo la Saikolojia, umeona hilo kundi namba moja? Yani watu wenye failures za maisha, sasa nikwambie hakuna anayekubali failures kirahisi ndungu yangu, ni hivi.
Timu ya mpira inaweza kucheza Fyongo, ikafungwa, ila haitakosa wa kumlaumu, naomba uelewe ni "Wa Kumlaumu" maana yake ni mtu, aidha refa, mchezaji ama hata kocha. Ndivyo ilivyo kwa mtu mwenye majuto, akianza kuyakataa, kitaalamu tunasema ana "Play, victim side" yaani yeye hujiweka kama mhanga wa shida anayopitia, ila mtu fulani ndiye lazima awe sababu.
Katika pita pita yako, uliwahi kusikia mzee yeyote anayeshinda kwenye vijiwe vya kahawa huko akasimulia historia yake ya shule akasema alikuwa wa mwisho darasani? Hapana, imekuwaje leo kawa hivo? Atamtafuta wa kumtupia lawama. Kitendo hiki, kwa kingereza kinajulikana kama PROJECTION DEFENSIVE MECHANISM
Ni nini haswa?
Ni hali ya kujilinda kutoka kwenye makosa/majuto ama lawama, kwa kumuona mwengine kama sababu ya shida yako.
Je mama yako anayo?
Jibu ni NDIO, anahisi kutengwa, jiulize, aseme anataka kuuliwa kwa lipi? Kitendo cha kuhisi kutengwa kinamfanya ajihisi kama mnasema/mnamsimanga/ ama mnamuonea kinyaa, hilo ndio PARANOIA bwana , anatumia njia ya Projection, ili siku kwa bahati mbaya (Siombei) akiaga dunia, msije mkazungumzia hali yake (UKIMWI) bali ugomvi wake na mtu fulani, kwa sababy ikiwa hivo, ni aibu, kama ujuavyo ugonjwa wenyewe kwenye jamii yetu unavyochukuliwa.
MFANYE NINI?
Kabla ya kuhangaika na Watabibu wa akili, ninyi ndio mnapaswa kuwa watabibu wa kwanza (Kumbuka ulisema hali yake kabla hamjaondoka) kaeni na mama yenu, ikiwa mna familia zenu, fanyeni ratiba ya kila siku moja ya wiki muwepo woote, mkae nae, mle nae, stori n.k. hakikisha hamzungumzii masuala yenye kutia huzuni huko, sio mnaanza stori za marehemu bibi yenu wa Kibaigwa, hapana, ni mwendo wa kujichekelesha.
Halafu; kama ulivyotuletea ombi hili la ushauri, utuletee na mrejesho baada ya kufanya hivi.
Mwl. Diwani