Ushauri: Nisaidieni namna Bora ya kutibu tatizo linalomuandama mama yangu

g vizy

JF-Expert Member
Jan 5, 2016
896
977
Habari wakuu poleni na majukumu mbalimbali ya Kila siku

Mama yanguamekumbwa na tatizo ambalo hata sisi binafsi kama watoto wake tumeshindwa kumuelewa

Labda nianze Kwa kusema mama ni mwathirika wa virusi vya ukimwi Kwa Muda mrefu na amekua akitumia vidonge vya ARVS Kwa Muda mrefu sana. kipindi cha nyuma tulikua tukiishi nae vizuri tu tukiwa wote nyumbani kabla ya sisi watoto wake kutawanyika Kila mmoja kuishi katika mji wake na familia yake (baba yetu alifariki Muda mrefu sana tangu mwaka 1994)

Sasa mnamo mwaka 2018 baada ya sisi watoto kutawanyika nyumbani tulimwacha mwenyewe pale nyumbani na ikawa tunamuhudumia Kwa matumizi ya hapa na pale,ilipofika mwezi wa 11 kuelekea mwezi wa 12 mwaka huo ndipo tatizo hili lilipoanza

Akawa anatuambia wanangu hapa nyumbani naona Kuna watu wanakuja wananifatilia wanataka kuniua Mimi siwaelewi tukawa tuna muuliza ni watu gani hao mbona sisi wakati tunaishi hapo hatukuwai kuwa na tatizo na mtu,akazidi kusisitiza kwamba Mimi siwezi kuendelea kuishi hapa naomba mje mnichukue

Basi dada yetu mkubwa ikabidi apange safari aende akamchukue mana yeye ndiye anaeishi nae karibu zaidi kuliko sisi wengine mana tupo mikoa ya mbali, baada ya kumchukua na kuanza kuishi nae lile tatizo likawa kama limemtoka la kuhisi watu wanamfatilia wanataka wamuue.... Bas ikaenda Kwa Muda kama wa mwaka mmoja hivi akadai anataka aende kijijini kukaa Kwa madai yake kwamba anataka kubadilisha mazingira haikua tatizo
Tukampeleka Kwa mama yetu mdogo nae alisema ngoja nijaribu kuishi nae mana mama mdogo ni mtu wa maombi sana kanisani masaa 24

Yaan tulivyompeleka kule ndo kama tukawa tumeongeza tatizo ikawa Kila Muda tunaambiwa kwamba mama yenu anataka kujinyonga ety amechoka kuishi anaona Kila mtu mbaya kwake Hana Nia njema juu yake ikawa ni kulalamika Kila Leo kwamba mama yenu mdogo ananichukia,mara watoto wake hawanieshimu yaani ikawa taflani

Mpaka kufikia hatua mamdogo kusema mje mumchukue mama yenu Mimi amenishinda inafikia hatua anataka ajinyongee nyumbani kwangu tena mbele ya watoto wangu Mimi Kwa kweli hapana

Dada ikabidi aende akamchukue amrudishe tena nyumbani kwake mana ni mama yetu hatuna namna inabidi tuishi nae hvyo hvyo
Sasa baada ya kumrudisha yaan ndo kama tatizo limezidi kua kubwa zaidi mpaka dada nae ameanza kuhofia juu ya uhai wake mana amekua ni mtu wa kulaumu Kila mtu hamna mtu anaefanya jema kwake imefikia hatua anadai sisi tunapanga njama za kumuua kwanza hatumthamini kitu ambacho sio kweli mbaya zaidi anadai Mimi Bora nife tu Sina nilichobakiza Dunian,wakati mwingine anaongea vitu havieleweki,avielezeki yaan
Amekua ni mtu wa kuwaza tuuuu Muda wote Yani halali usingizi,ni kama mtu mwenye uwoga
Muda mwingine anatukana mpaka watoto wa dada kwamba nao Wana njama za kutaka kumuua,Sasa unajiulizan watoto wadogo hawa akili ya namna hiyo waitolee wapi

Kifupi ni kama mtu aliyechanganyikiwa,analaumu Kila anaemuona mbele yake kwamba ni sababu ya yeye kua hivyo.
Sasa wakuu hii tatizo linaniumiza sana kichwa changu sijui tunafanyaje kutibu hili tatizo.mana kama ni kuombewa ameshaombewa sana tu tangu kule Kwa mamdogo lakini wapi Mambo yamekua magumu

Najiuliza uenda ni issue ya phycology tumtafutie wanasaikolojia wakae nae wazungumze nae sisi tulishaongea nae mara nyingi sana hamna kitu tumeambulia

Sasa ndugu zangu nimeleta kwenu mnishauri nifanyaje kutibu tatizo halilonalo mama angu
Sipendi awe kwenye hali hii inatuchanganya familia nzima hatuelewi la kufanya we are so confused Kwa kweli

Natanguliza shukrani wakuu
 
Kuna binamu yangu naye ni mgonjwa , naye alichizika kabisa, alikuwa akitoroka 8 za usiku na kanga moja na kudakiwa kesho yake asubuh , kwenye kata nyingine. But kwa sasa Ni mzima amerudi kwenye hali yake ya kawaida na ana afya nzuri.

TIBA: Kutumia mda mwingi ktk MUNGU ( kusikiliza station za injili ) , kutokukaa bila kazi na kumuuonesha unampenda zaidi ya chochote
 
Poleni sana mkuu

Shida aliyonayo mama ni ya kisaikolojia hasa ukozingatia na hali yake ya kiafya, anakua keshakata tamaa na hali hiyo ilikosa mfariji na mshauri wa kua naye karibu tokea mwanzo wa tatizo sasa limekua kubwa

Jaribuni kumpeleoa rehab ya saikolojia tena kwa muda mrefu atakaa sawa,

Wakati anaendelea na tiba kuweni naye karibu sana naongeleeni mambo chanya juu yake

Kuhusu kifo mfarijini kwamba si yeye tu hata nyie na sisi sote tupo kwenye foleni itakuja siku tutaondoka asikiogope kifo
 
Nasikiaga mtu muathirika wa HIV huwa vitu vinapanda kichwani anakua kama chizi sio mzima, muda wote ni makasiriko, muda wote anaona anaonewa hasira nk sijui virus anaharibu brain au ni madawa anayotumia ila sina uhakika maana sijafanyie tafiti ya kisayansi
 
Hallucination ni kitu cha kawaida kwa wagonjwa wanaotumia dawa kwa muda mrefu sana ... anaona na kusikia sautu ambazo hazipo.... hasa hizo LSD na baadae atahama stage na kuanza kupoteza kumbukumbu. Ni vyema mkamuona daktari wana weza kuamua kumbadilishia dawa na ushauri mwingine wa kitabibu na kisaikolojia.
 
Poleni sana mkuu

Shida aliyonayo mama ni ya kisaikolojia hasa ukozingatia na hali yake ya kiafya, anakua keshakata tamaa na hali hiyo ilikosa mfariji na mshauri wa kua naye karibu tokea mwanzo wa tatizo sasa limekua kubwa

Jaribuni kumpeleoa rehab ya saikolojia tena kwa muda mrefu atakaa sawa,

Wakati anaendelea na tiba kuweni naye karibu sana naongeleeni mambo chanya juu yake

Kuhusu kifo mfarijini kwamba si yeye tu hata nyie na sisi sote tupo kwenye foleni itakuja siku tutaondoka asikiogope kifo
Mkuu nashukuru sana ngoja nijaribu hii njia
 
19 Reactions
Reply
Back
Top Bottom