USHAURI: Nimeachiwa Familia ya Mtu Bila Taarifa Rasmi!!

Pole sana Ndugu.

Cha msingi, kaa na mke wako pamoja na mkewe. Mueleze kuwa hali ya sasa si nzuri hata kidogo. Na unashindwa kuimudu familia, hivyo watafute namna ya kusaidiana.

Ama La!. Mkeo awapigie ndugu zake na kuwaeleza kuwa sasa umeshindwa kuhudumia familia ya kaka yake. Watakusaidia.

Au, gawaneni watoto. Kila ndugu achukue mtoto mmoja, ili angalau wewe upunguziwe na mzigo.
Asante kwa ushauri wako!
 
Upumbavu huo sikubali, nikiona ngumu namtongaza huyo wifi yake wife kiaina ili wife haisi kitu.. wenyewe wataondoka bila kuaga.
 
Mnunulie unnga wa ngano kilo 5 huyu bidada mwambie akiwa anamsubiri mume wake atafute hoteli itakayochukua maandazi au chapati na wewe itakuwa unasave budget ya break fast asubuhi

ukitaka kujua tofauti ya mwanamke na mwanaume kwenye kufikiri hapa ndo mfano mkubwa ,angalia sky Eclat alichocomment alafu anagalia wanaume walichocomment ati amtom.b.e.e mkewe.hahahah had inatia kichefu chefu ahsante MAMA zetu kutuzaa wanawake..
bdw huyo mkewe nae ni KILAZA first bgrade unasdhindwa ht kupika maandaz??kichwa changu mm kingechemka ningejua nailishaje familia yangu shme to her kwakweli mwanamke mwenzetu...hongera mdada kutoa ushauri kuntu
 
Ni kukufahamisha kuwa iko siku hata hiyo familia yako itakuwa kubwa ,lkn hizo ni sehem za baraka zako muombe mungu nyie atakufungulia lkn pia sisi binadam tunategemeana iko siku utakwama saa ingine huyohuyo atakusaidia pambana hizo ni njia.
Asante ndugu, nimekupata vizuri, lakini kumbuka msaada unapozidi uwezo unageuka kuwa mateso kwako! Hapa saizi asubuhi hii kumekucha sijui itakuwaje,mi mweupe mfukoni, nimepigana kiume mpaka hatua hii mtu Hatokei kuja kuchukua familia yake, mbaya zaidi kodi yangu inaisha mwezi wa saba tarehe 15 yaani mpaka sasa nina mwezi mmoja tu wa kukaa kihalali mahali ninapokaa, mshahara wa mwezi huu natakiwa nilipe kodi ya nyumba, hapo hapo natakiwa kulisha familia yangu na ya jamaa, halafu jamaa mwenyewe karelax huko hata hana habari kabisa,hajui maumivu ninayoyapata huku!
Cha kushangaza haipiti siku bila kumpigia mke wake, lakini mimi hajawahi kunipigia simu, wala kuniandikia meseji wala kunibeep tangu aache familia yake, hata siku anakuja na familia yake nyumbani hakunijulisha kwamba Shemeji tunakuja huko nyumbani kwenu, alikuja kimya kimya mida ya saa mbili kasoro usiku, mi natoka kwenye mihangaiko kuja nyumbani nakuta familia imeongezeka mara mbili zaidi, nikajua labda wamekuja kutusalimia tu, na wataondoka kesho yake, lakini jamaa kesho yake kaondoka pekee yake tena bila hata kuniaga akaiacha familia yake,,,,,, ndugu,,, kwakweli ni maumivu!! Ila basi tu, halafu unaniambia nivumilie, hata maandiko matakatifu yanasema TUWE NA KIASI.
Pia Marehemu Ngurumo aliwahi kuimba wimbo mmoja kwenye bendi yao ya MSONDO NGOMA MUSIC BAND, "tenda wema uende zako, lakini wema usizidi uwezo" Kwakweli mi maji yako shingoni,hali imeshakuwa ngumu kwa sasa, tukubaliane tu na hali yenyewe,
Siyo kwamba inapokuwa ngumu kwake kwa wengine iko vizuri,hapana kila mtu inakuwa ngumu kwa nafasi yake,ni kukomaa tu,hakuna kingine zaidi!
BTW nakushukuru kwa ushauri wako!
NB: Mimi ni mkristo,tunafundishwa upendo, lakini inabidi tu tukubaliane na udhaifu wa kibinadamu, hali ni mbaya,ninaposema ni mbaya naomba mnielewe kabisa, sina jinsi, ikumbukwe mimi huwa napokea wageni wa kila aina kutoka kwa ndugu wa mke wangu, lakini wanakaa siku mbili tatu wanaondoka, sasa hii ya mwezi mzima tena bila hata taarifa rasmi,
Inaniumiza sana moyoni,,,,,,!!!!
 
Upumbavu huo sikubali, nikiona ngumu namtongaza huyo wifi yake wife kiaina ili wife haisi kitu.. wenyewe wataondoka bila kuaga.
Kanyela mumo wewe wasema!
Tena nina imani unatokea kanda ileile tunayotokea mi na huyu jamaa, unajua mila na desturi za huko, kiasili sisi huwa siyo wachoyo kabisaaa! Lakini kwa maisha ya hapa DSM inabidi wakati mwingine uzalendo ukuishe bwana Kanyela mumo!
 
Huyo mwanamke pamoja nahao watoto wapeleke kwa mama mkwe wake yaani bibi zao na hao watoto,halingumu saiv.
 
Asalam!!

Kama kichwa cha habari kisemavyo hapo juu, ni takribani mwezi sasa unaelekea kuisha tangu hii familia iwepo nyumbani kwangu!

Habari yenyewe kiundani wake iko hivi;

Mwenye familia ni ndugu wa mke wangu, Ni weekend moja ya siku za nyuma nilikuwa kwenye mihangaiko yangu ya kimaisha, niliporudi nyumbani jioni saa moja, nilimkuta huyo ndugu wa mke wangu yupo nyumbani kwangu akiwa na Familia yake yote, yaani Yeye, mke wake pamoja na watoto wake watatu!
Walilala nyumbani kwangu usiku huo, kesho yake mimi nikaamkia kwenye mihangaiko yangu, jioni niliporudi nyumbani sikumkuta nyumbani huyo jamaa, lakini watoto wake na mke wake walikuwepo!
Mimi nikajua labda yuko kwenye mizunguko tu atarudi baadae na pia nilijua wamekuja kutusalimia tu kwa muda wataondoka kesho yake, nilisubiri siku hiyo sioni mtu, ikawa usiku ikawa asubuhi, kesho yake hakuonekana tena! Nikamuuliza mke wangu!
Huyu ndugu yako vipi,akasema hana taarifa naye!
Nikasema isiwe shida madam ni mtu mzima atarudi!! Tumekaa siku kadhaa haonekani,nami sijataka kumtafuta kwenye simu!
Basi baada ya siku kadhaa akapiga simu kwa mke wangu akilalamika, eti maisha magumu sana siku hizi, wife akamjibu kwani tangu lini maisha yakawa mepesi!!!!

Jamaa akakata simu mpaka leo hii ninapoandika uzi huu, jamaa hajapiga simu tena, na familia yake bado iko kwangu!

Sasa shida inakuja kwenye bajeti ya nyumbani, imeshoot ghafla tangu jamaa alete familia yake, mi nina mke na mtoto mmoja, sasa hili ongezeko la watu wanne ghafla limebadilisha kabisa hali ya bajeti ya nyumbani,na ukizingatia hali ya uchumi ya sasa ilivyokaa, nashindwa kumudu mambo mengine,nilikuwa na kaujenzi imebidi nisimame kwanza ili nilishe familia nikitumaini kuwa jamaa atakuja kuchukua familia yake soon, lakini ndo hivyo jamaa kakausha utafikiri hajui kitu, na mimi huku maji yako shingoni, si unajua mshahara wa mwalimu Wa shule ya msingi, tena maisha ya Dar es Salam!

Samahani kwa kuwachosha ndugu wanaJF!

Ninachoomba kutoka kwenu ni kitu kimoja tu, ni ushauri namna ya kumwambia ili aje kuchukua familia yake, maana kila mtu atabeba msalaba wake mwenyewe! Mi uwezo wa kumtunzia familia yake umefikia kikomo, nimwambiaje huyu jamaa wandugu, make mpaka saizi nafikiria kesho tutakula nini, sijalala wala usingizi sipati, nawaza kesho itakuwaje, na jamaa kimyaa hadi muda huu!!!
Nisaidieni jamani!

Nawasilisha!!
Pole, hapo ndipo uwezi wa Mugu unapoonekana. Jamaa, ni Genius sana. Baada ya kuona kuwa huna uwezo wa kuzalisha watoto wengi, huku ukiwa na uwezo mkubwa wa kulea familia kubwa akaona bora aje akuongezee familia.
TIMUA HAOOOOOOOOOOOOOOOO, waende kwa mama au baba mkwe wako. Uko ndiko wanakostahiri kuishi bada ya kukimbiwa na jamaa aliyekimbia familia.
 
Asalam!!

Kama kichwa cha habari kisemavyo hapo juu, ni takribani mwezi sasa unaelekea kuisha tangu hii familia iwepo nyumbani kwangu!

Habari yenyewe kiundani wake iko hivi;

Mwenye familia ni ndugu wa mke wangu, Ni weekend moja ya siku za nyuma nilikuwa kwenye mihangaiko yangu ya kimaisha, niliporudi nyumbani jioni saa moja, nilimkuta huyo ndugu wa mke wangu yupo nyumbani kwangu akiwa na Familia yake yote, yaani Yeye, mke wake pamoja na watoto wake watatu!
Walilala nyumbani kwangu usiku huo, kesho yake mimi nikaamkia kwenye mihangaiko yangu, jioni niliporudi nyumbani sikumkuta nyumbani huyo jamaa, lakini watoto wake na mke wake walikuwepo!
Mimi nikajua labda yuko kwenye mizunguko tu atarudi baadae na pia nilijua wamekuja kutusalimia tu kwa muda wataondoka kesho yake, nilisubiri siku hiyo sioni mtu, ikawa usiku ikawa asubuhi, kesho yake hakuonekana tena! Nikamuuliza mke wangu!
Huyu ndugu yako vipi,akasema hana taarifa naye!
Nikasema isiwe shida madam ni mtu mzima atarudi!! Tumekaa siku kadhaa haonekani,nami sijataka kumtafuta kwenye simu!
Basi baada ya siku kadhaa akapiga simu kwa mke wangu akilalamika, eti maisha magumu sana siku hizi, wife akamjibu kwani tangu lini maisha yakawa mepesi!!!!

Jamaa akakata simu mpaka leo hii ninapoandika uzi huu, jamaa hajapiga simu tena, na familia yake bado iko kwangu!

Sasa shida inakuja kwenye bajeti ya nyumbani, imeshoot ghafla tangu jamaa alete familia yake, mi nina mke na mtoto mmoja, sasa hili ongezeko la watu wanne ghafla limebadilisha kabisa hali ya bajeti ya nyumbani,na ukizingatia hali ya uchumi ya sasa ilivyokaa, nashindwa kumudu mambo mengine,nilikuwa na kaujenzi imebidi nisimame kwanza ili nilishe familia nikitumaini kuwa jamaa atakuja kuchukua familia yake soon, lakini ndo hivyo jamaa kakausha utafikiri hajui kitu, na mimi huku maji yako shingoni, si unajua mshahara wa mwalimu Wa shule ya msingi, tena maisha ya Dar es Salam!

Samahani kwa kuwachosha ndugu wanaJF!

Ninachoomba kutoka kwenu ni kitu kimoja tu, ni ushauri namna ya kumwambia ili aje kuchukua familia yake, maana kila mtu atabeba msalaba wake mwenyewe! Mi uwezo wa kumtunzia familia yake umefikia kikomo, nimwambiaje huyu jamaa wandugu, make mpaka saizi nafikiria kesho tutakula nini, sijalala wala usingizi sipati, nawaza kesho itakuwaje, na jamaa kimyaa hadi muda huu!!!
Nisaidieni jamani!

Nawasilisha!!
Pole sana ila Mkuu vumilia tu coz mimi shem wangu aliniachia familia yake miezi 6+ ila baadae yule wife wake alivyoona jamaa haji ikabidi arudi kwa wazazi wake.
 
Asante ndugu, nimekupata vizuri, lakini kumbuka msaada unapozidi uwezo unageuka kuwa mateso kwako! Hapa saizi asubuhi hii kumekucha sijui itakuwaje,mi mweupe mfukoni, nimepigana kiume mpaka hatua hii mtu Hatokei kuja kuchukua familia yake, mbaya zaidi kodi yangu inaisha mwezi wa saba tarehe 15 yaani mpaka sasa nina mwezi mmoja tu wa kukaa kihalali mahali ninapokaa, mshahara wa mwezi huu natakiwa nilipe kodi ya nyumba, hapo hapo natakiwa kulisha familia yangu na ya jamaa, halafu jamaa mwenyewe karelax huko hata hana habari kabisa,hajui maumivu ninayoyapata huku!
Cha kushangaza haipiti siku bila kumpigia mke wake, lakini mimi hajawahi kunipigia simu, wala kuniandikia meseji wala kunibeep tangu aache familia yake, hata siku anakuja na familia yake nyumbani hakunijulisha kwamba Shemeji tunakuja huko nyumbani kwenu, alikuja kimya kimya mida ya saa mbili kasoro usiku, mi natoka kwenye mihangaiko kuja nyumbani nakuta familia imeongezeka mara mbili zaidi, nikajua labda wamekuja kutusalimia tu, na wataondoka kesho yake, lakini jamaa kesho yake kaondoka pekee yake tena bila hata kuniaga akaiacha familia yake,,,,,, ndugu,,, kwakweli ni maumivu!! Ila basi tu, halafu unaniambia nivumilie, hata maandiko matakatifu yanasema TUWE NA KIASI.
Pia Marehemu Ngurumo aliwahi kuimba wimbo mmoja kwenye bendi yao ya MSONDO NGOMA MUSIC BAND, "tenda wema uende zako, lakini wema usizidi uwezo" Kwakweli mi maji yako shingoni,hali imeshakuwa ngumu kwa sasa, tukubaliane tu na hali yenyewe,
Siyo kwamba inapokuwa ngumu kwake kwa wengine iko vizuri,hapana kila mtu inakuwa ngumu kwa nafasi yake,ni kukomaa tu,hakuna kingine zaidi!
BTW nakushukuru kwa ushauri wako!
NB: Mimi ni mkristo,tunafundishwa upendo, lakini inabidi tu tukubaliane na udhaifu wa kibinadamu, hali ni mbaya,ninaposema ni mbaya naomba mnielewe kabisa, sina jinsi, ikumbukwe mimi huwa napokea wageni wa kila aina kutoka kwa ndugu wa mke wangu, lakini wanakaa siku mbili tatu wanaondoka, sasa hii ya mwezi mzima tena bila hata taarifa rasmi,
Inaniumiza sana moyoni,,,,,,!!!!
Samahani sana kwakukuambia hili ww una roho mbaya sana tena huna hutuma chukulia ndg zako wamekuja hapo kuishi kwako utalalamika hivyo ?mbona inaonekana wa ajabu sana lkn kingine utalalamika sana he wangekuwa 7 wacha hayo lkn pia hutoiona baraka kwa staili hiyo kama unaumia sana wafukuze ili jamii ielewe umetaka ushauri bado malalamiko we waajabu sana mkuu.
 
Umetumwa? mbona unatoa povu sana? Hata kama ni msaada unatakiwa uendane na uwezo.
 
Mdinye huyo mke wake. Mkeo akijua unamdinya wifi yake atamfukuza yeye mwenyewe haraka sana nawe utaenda kanisani kutubu dhambi
 
Samahani sana kwakukuambia hili ww una roho mbaya sana tena huna hutuma chukulia ndg zako wamekuja hapo kuishi kwako utalalamika hivyo ?mbona inaonekana wa ajabu sana lkn kingine utalalamika sana he wangekuwa 7 wacha hayo lkn pia hutoiona baraka kwa staili hiyo kama unaumia sana wafukuze ili jamii ielewe umetaka ushauri bado malalamiko we waajabu sana mkuu.
Asante bwana Hakika utakufa!
Nakubaliana na wewe kuwa mimi ni wa ajabu, kwa sababu nalalamika, kwahiyo mtu yeyote anayeomba ushauri ni mlalamikaji, Heri wenye kuudhiwa kwa ajili ya haki maana,,,,,, nakutakia kila la heri!
Na nimeshakusamehe bure!
BTW nakushukuru kwa yote!
 
Mwambie jamaa ukweli wote bila chenga, aje abebe familia yake, usimumunye maneno, au kama vipi nipatie namba zake nikusaidie kumpasha
 
Pole kwa majkm hayo mapya mkuu, haya mambo yapo sn kwani siku hazifanani. Ukiona hivyo ujue hata jamaa huko alipo anaumia an kuliko hata ww uliyetwishwa zigo la familia yake. Nakushauri tu uwe mvumilivu kwani muda si mrefu watapata akili yakujikata kivingine
 
Asalam!! Kama kichwa cha habari kisemavyo hapo juu, ni takribani mwezi sasa unaelekea kuisha tangu hii familia iwepo nyumbani kwangu!
Pole kaka, ila ndio majukumu yetu kwa tamaduni zetu, huwezi watupa nje, huwezi wafukuza, ila badilisha hayo mawazo ya kuona umeonewa au kuongezewa mzigo na kuleta mbinu za kuwanufaisha wote, kuna mmoja kashauri kumnunulia shemeji unga wa ngano apike chapati, kuna swala ka kagenge, kuna swala la kabustani, kuna mambo ya kijasiriliamali waweza kugundua wewe na mama watoto na shemeji, na hata watoto wa kaka mkaweza kuongeza kipato, kuna kuuza juice, ice cream, mama ntilie n.k. n.k.
Kaza butu mwanaume, tulizaliwa kupata shida, kutoa jasho, sasa huu ndio mtahani kama mwanaume uonyeshi ujasiri wako..kila la heri, chukulia kama umeongezewa nguvu nyingine ya kujikwamuwa kiuchumi, na nyumba yako ilivyo jaa sasa mbona mtakuwa na amani na vicheko tu..
 
Back
Top Bottom