USHAURI: Nimeachiwa Familia ya Mtu Bila Taarifa Rasmi!!

Pole sana Ndugu.

Cha msingi, kaa na mke wako pamoja na mkewe. Mueleze kuwa hali ya sasa si nzuri hata kidogo. Na unashindwa kuimudu familia, hivyo watafute namna ya kusaidiana.

Ama La!. Mkeo awapigie ndugu zake na kuwaeleza kuwa sasa umeshindwa kuhudumia familia ya kaka yake. Watakusaidia.

Au, gawaneni watoto. Kila ndugu achukue mtoto mmoja, ili angalau wewe upunguziwe na mzigo.
 
Huyo mke wako ni mama wa nyumbani tu? Kama ni hvyo wakalishe chini ongea nao. *some text missing*fanikiwa. Pole sana ndo ukubwa.
 
Dawa ni kumtimua tuu huyo mke wake na watoto wake, acha kuona aibu, uoga wako ndio umaskini wako
 
Mnunulie unnga wa ngano kilo 5 huyu bidada mwambie akiwa anamsubiri mume wake atafute hoteli itakayochukua maandazi au chapati na wewe itakuwa unasave budget ya break fast asubuhi

Hapana si sawa.....aanze mchakato wa kumgegeda wife wa huyo jamaa....either wife wake akihisi lazima amtimue wifie ama jamaa huko aliko akipata taarifa atakuja kumchukua mkewe mara moja.
 
Asalam!!

Kama kichwa cha habari kisemavyo hapo juu, ni takribani mwezi sasa unaelekea kuisha tangu hii familia iwepo nyumbani kwangu!

Habari yenyewe kiundani wake iko hivi;

Mwenye familia ni ndugu wa mke wangu, Ni weekend moja ya siku za nyuma nilikuwa kwenye mihangaiko yangu ya kimaisha, niliporudi nyumbani jioni saa moja, nilimkuta huyo ndugu wa mke wangu yupo nyumbani kwangu akiwa na Familia yake yote, yaani Yeye, mke wake pamoja na watoto wake watatu!
Walilala nyumbani kwangu usiku huo, kesho yake mimi nikaamkia kwenye mihangaiko yangu, jioni niliporudi nyumbani sikumkuta nyumbani huyo jamaa, lakini watoto wake na mke wake walikuwepo!
Mimi nikajua labda yuko kwenye mizunguko tu atarudi baadae na pia nilijua wamekuja kutusalimia tu kwa muda wataondoka kesho yake, nilisubiri siku hiyo sioni mtu, ikawa usiku ikawa asubuhi, kesho yake hakuonekana tena! Nikamuuliza mke wangu!
Huyu ndugu yako vipi,akasema hana taarifa naye!
Nikasema isiwe shida madam ni mtu mzima atarudi!! Tumekaa siku kadhaa haonekani,nami sijataka kumtafuta kwenye simu!
Basi baada ya siku kadhaa akapiga simu kwa mke wangu akilalamika, eti maisha magumu sana siku hizi, wife akamjibu kwani tangu lini maisha yakawa mepesi!!!!

Jamaa akakata simu mpaka leo hii ninapoandika uzi huu, jamaa hajapiga simu tena, na familia yake bado iko kwangu!

Sasa shida inakuja kwenye bajeti ya nyumbani, imeshoot ghafla tangu jamaa alete familia yake, mi nina mke na mtoto mmoja, sasa hili ongezeko la watu wanne ghafla limebadilisha kabisa hali ya bajeti ya nyumbani,na ukizingatia hali ya uchumi ya sasa ilivyokaa, nashindwa kumudu mambo mengine,nilikuwa na kaujenzi imebidi nisimame kwanza ili nilishe familia nikitumaini kuwa jamaa atakuja kuchukua familia yake soon, lakini ndo hivyo jamaa kakausha utafikiri hajui kitu, na mimi huku maji yako shingoni, si unajua mshahara wa mwalimu Wa shule ya msingi, tena maisha ya Dar es Salam!

Samahani kwa kuwachosha ndugu wanaJF!

Ninachoomba kutoka kwenu ni kitu kimoja tu, ni ushauri namna ya kumwambia ili aje kuchukua familia yake, maana kila mtu atabeba msalaba wake mwenyewe! Mi uwezo wa kumtunzia familia yake umefikia kikomo, nimwambiaje huyu jamaa wandugu, make mpaka saizi nafikiria kesho tutakula nini, sijalala wala usingizi sipati, nawaza kesho itakuwaje, na jamaa kimyaa hadi muda huu!!!
Nisaidieni jamani!

Nawasilisha!!
Ni kukufahamisha kuwa iko siku hata hiyo familia yako itakuwa kubwa ,lkn hizo ni sehem za baraka zako muombe mungu nyie atakufungulia lkn pia sisi binadam tunategemeana iko siku utakwama saa ingine huyohuyo atakusaidia pambana hizo ni njia.
 
Hapana si sawa.....aanze mchakato wa kumgegeda wife wa huyo jamaa....either wife wake akihisi lazima amtimue wifie ama jamaa huko aliko akipata taarifa atakuja kumchukua mkewe mara moja.
Kutokana na umasikini wa nchi zetu familia ndiyo social security, shida haina mwenyewe huwezi jua lini mleta mada atasaidiwa na familia hii.
 
Mkuu alisema kadiri muda unavyokwenda itakuwa ngumu kuishi kiujanja ujanja
 
Pole sana mwalimu, na mkeo anasemaje kuhusu hili maana naye ana kauli ambayo anaweza tumia hiyo familia pandikizi ikarudi kwenye himaya yake
 
mtumie sms hii
'ILIKUWA TAMU SANA" au
'TOKA BASI ILA ASIJUE'
au
'LEO HATUENDI TENA? MBN UMEKAA TU'

afu mtumie "TEXT SIYO YAKO" ..., usipomwona hapo ndani ya nusu saa utaniambia
 
Binadamu ni mnyama kama mnyama mwingine yeyote wa kufugwa ama wa pori. Tofauti yake ni ndogo sana. Binadamu aliyekamilika ana kitu kinaitwa utashi. Hiki kitu hutufanya tutofautiane kidogo na makundi mengine ya wanyama. Hapo kwenye utashi nitaeleza mwisho wa comment yangu.
Hayo yote uliyoshauri, yana vikwazo vyake, ndiyo maana jamaa kaomba ushauri.
Jamaa katendewa unyama kutokana na ubinafsi uliopitiliza wa mtelekezaji, kwamba shida zake za kimaisha ni kubwa sana kuliko za wengine.
Ushauri ninaoweza kuutoa ni kama ufuatao.
Hatua ya kwanza ni kuripoti tukio hilo polisi kwa ajili ya kinga ya kashifa ama kesi yoyote ya kijingajinga dhidi yake itokanayo na msala huo.
Pili kuwasiliana na ukweni kwake kuwajulisha jambo hilo, ili waweze kufikia uamzi wa pamoja namna ya kuweka sawa jambo hilo, sasa inategemeana na ukweni kwake kupoje, iwapo familia ni yenye kueleweka au vurugumechi.
Kimsingi jamaa kabebeshwa jukumu lisilo la kwake.
Tuchukulie mfano huyo shemeji yake aliyetelekezwa, ingekuwa kapewa talaka angelikabidhiwa yeye? Je angelifiwa na huyo mmewe, hiyo familia angerundikiwa yeye?
Tatizo kubwa kama hilo pindi litokeapo, inawapasa wanafamilia (ukoo wa mme) kuchukua hatua mahsusi za kunusuru familia ya ndugu yao.
Hivyo huyo mwanamke anastahili kurejeshwa kwa wazazi wake ama kwao.
Gharama za nauli za kuwarejesha nyumbani kwao, kama kutakuwa na sintofahamu, basi jamaa abebe uzito kuliko kuendelea kukaa na hiyo familia ya mme mwenziye baradhuli.
Asitegemee shukrani yoyote toka kwa huyo jamaa aliyetelekeza familia yake kinyama.
Atakapokuja kurejea atakuja katika sura ya kudai haki zaidi.
Kwa hiyo jamaa achukue tahadhari na hatua madhubuti kuepusha balaa zaidi siku za usoni.
Hilo tukio hufanywa na binadamu wabinafsi ama wenye matatizo ya kisaikolojia.
Binadamu tunaongozwa na utashi katika maamuzi kwamba ni nini kibaya na nini kizuri cha kufanya kuweza kumkwaza ama kumpendeza mwingine.
Matukio ya aina hiyo yapo mengi sana.
Wapo wengine hutorokea kwake akiacha mke na watoto wakihangaika bila ya chochote. Akija kurejea huanza kudai haki kipumbafupumbafu.
Wanaume wa namna hiyo hawatofautiani na wanawake wanaotelekeza watoto wao baada ya kujifungua kwa visingizio mbalimali.
Hastahili kuendelea kuishi na hiyo familia, awarejeshe kwao ama kwa ndugu zao.
Asante ndugu kwa ushauri wako! Nitaufanyia kazi!
 

Similar Discussions

9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom