USHAURI: Nimeachiwa Familia ya Mtu Bila Taarifa Rasmi!!

hivi kweli kabisa unapeleka mke na watoto watatu kwa shemeji yako .hakuwa na option nyingine kabisa? halafu akakimbia eti .
Hapo sasa utafikiri alimwolea mtu mwingine badala apambane na hali yake anahamisha matatizo.

Anafaa kutandikwa makwenzi kabisa wanaume kama yeye wanaponda kokoto kulea familia yeye anakimbia shenzi kabisa
 
Great power comes from great responsibilities. Endelea kupigana kuwatunza usione kama mzigo we are strong because we need carry those who are weak.
 
Unawahudumia vizuri ndo mana wanakaa we piga dagaa kavu siku 3 tu utanambia kama hawaagi ,mumewe anavoongea nae na anaambiwa tunaishi vizuri ndo anaendelea kubweteka
 
Usiache bajeti nyumbani utaona mwanamke mwenzie atakavyo muondoa na familia yake.
 
Wewe MPE nauli mkeo mwambie akapumzike kwao maana hali yako ishakuwa tete ukijipanga vizuri utamrudisha hapo ndipo solution ya unachotaka kukifanya utafanikiwa
 
Samahani sana kwakukuambia hili ww una roho mbaya sana tena huna hutuma chukulia ndg zako wamekuja hapo kuishi kwako utalalamika hivyo ?mbona inaonekana wa ajabu sana lkn kingine utalalamika sana he wangekuwa 7 wacha hayo lkn pia hutoiona baraka kwa staili hiyo kama unaumia sana wafukuze ili jamii ielewe umetaka ushauri bado malalamiko we waajabu sana mkuu.
Duuuh
 
Halafu watu wa namna hiyo huwa hawanaga shukrani, siku wanapoondoka hapo wataondoka na rundo la lawama
 
Back
Top Bottom