Mpenzi wangu amenizuia kwenda kwake, naombeni ushauri

hwasa

Member
Oct 17, 2023
14
55
Mimi ni mwanamke mchumba wangu ameanza likizo ya wiki mbili tukakubaliana aje nyumbani kwangu, alikuja kwangu siku ya Jumatano, ilipofika Ijumaa asubuhi akasema anaenda kuhakiki baadhi ya nyaraka, tukatoka wote siku hiyo.

Nilienda kwenye biashara zangu tukakubaliana jioni niende nyumbani kwake, ghafla akanipigia simu nisiende tena nyumbani kwao, niende nyumbani kwangu atakuja huko nikamwambia nipo karibu na nyumbani kwako nije kisha turudi wote nyumbani kwangu, anaishi na dada yake nyumbani kwake. Akasema hapana, dada yake ameondoka na gari na hajui atarudi saa ngapi.

Alijibu kwa ukali kwamba niende tu nyumbani kwangu. Mpaka leo hajanipigia simu wala kunitumia meseji na hajafika nyumbani nimechoka mimi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom