USHAURI: Nimeachiwa Familia ya Mtu Bila Taarifa Rasmi!!

Asalam!!

Kama kichwa cha habari kisemavyo hapo juu, ni takribani mwezi sasa unaelekea kuisha tangu hii familia iwepo nyumbani kwangu!

Habari yenyewe kiundani wake iko hivi;

Mwenye familia ni ndugu wa mke wangu, Ni weekend moja ya siku za nyuma nilikuwa kwenye mihangaiko yangu ya kimaisha, niliporudi nyumbani jioni saa moja, nilimkuta huyo ndugu wa mke wangu yupo nyumbani kwangu akiwa na Familia yake yote, yaani Yeye, mke wake pamoja na watoto wake watatu!
Walilala nyumbani kwangu usiku huo, kesho yake mimi nikaamkia kwenye mihangaiko yangu, jioni niliporudi nyumbani sikumkuta nyumbani huyo jamaa, lakini watoto wake na mke wake walikuwepo!
Mimi nikajua labda yuko kwenye mizunguko tu atarudi baadae na pia nilijua wamekuja kutusalimia tu kwa muda wataondoka kesho yake, nilisubiri siku hiyo sioni mtu, ikawa usiku ikawa asubuhi, kesho yake hakuonekana tena! Nikamuuliza mke wangu!
Huyu ndugu yako vipi,akasema hana taarifa naye!
Nikasema isiwe shida madam ni mtu mzima atarudi!! Tumekaa siku kadhaa haonekani,nami sijataka kumtafuta kwenye simu!
Basi baada ya siku kadhaa akapiga simu kwa mke wangu akilalamika, eti maisha magumu sana siku hizi, wife akamjibu kwani tangu lini maisha yakawa mepesi!!!!

Jamaa akakata simu mpaka leo hii ninapoandika uzi huu, jamaa hajapiga simu tena, na familia yake bado iko kwangu!

Sasa shida inakuja kwenye bajeti ya nyumbani, imeshoot ghafla tangu jamaa alete familia yake, mi nina mke na mtoto mmoja, sasa hili ongezeko la watu wanne ghafla limebadilisha kabisa hali ya bajeti ya nyumbani,na ukizingatia hali ya uchumi ya sasa ilivyokaa, nashindwa kumudu mambo mengine,nilikuwa na kaujenzi imebidi nisimame kwanza ili nilishe familia nikitumaini kuwa jamaa atakuja kuchukua familia yake soon, lakini ndo hivyo jamaa kakausha utafikiri hajui kitu, na mimi huku maji yako shingoni, si unajua mshahara wa mwalimu Wa shule ya msingi, tena maisha ya Dar es Salam!

Samahani kwa kuwachosha ndugu wanaJF!

Ninachoomba kutoka kwenu ni kitu kimoja tu, ni ushauri namna ya kumwambia ili aje kuchukua familia yake, maana kila mtu atabeba msalaba wake mwenyewe! Mi uwezo wa kumtunzia familia yake umefikia kikomo, nimwambiaje huyu jamaa wandugu, make mpaka saizi nafikiria kesho tutakula nini, sijalala wala usingizi sipati, nawaza kesho itakuwaje, na jamaa kimyaa hadi muda huu!!!
Nisaidieni jamani!

Nawasilisha!!
Duh mshahara wa mwalimu wa primary unaishi Dsm na unajenga? Kweli Dunia duara
 
duuh pole sanaa mkuu,wasiliana na jamaa kiutu uzima hopeful ataelewa,ye mwenyewe anauona huu usawa maji ya shingo
 
Acha upuuzi wewe watu tunaandikisha aina ya Noah tutakazonunuliwa na serikali kutokana na malipo ya mchanga wewe unatuletea blue story
 
Pole Mkuu lkn kwasababu jamaa hakukukabidhi Familia yake we fanya kitu kimoja tu warudishe kijijini yani fanya uwatafutie nauri warudi kwao walikotoka maana huo ni mtihani wanakupa we bora hata ukope sehemu nauri tu warudi kwao utakua umemsaidia jamaa
 
Acha upuuzi wewe watu tunaandikisha aina ya Noah tutakazonunuliwa na serikali kutokana na malipo ya mchanga wewe unatuletea blue story
Au jamaa katoroka kaamua kufata NOAH yake mapema ndiomaana kaacha familia!!!....l anxiously prefer a black noah 'kwelikweli'
 
Ebo!! Warudishe walipotoka..amekaa kimya inamaanisha amekudharau huyo..kwann aiwapeleke kwa mtu mwingine..!!
 
Msaada unaomba ni ushauri au maneno ya kumwambia shemeji yako aje achukue familia yake! ndugu najua una uwezo bora wa kuliamua hili bila hata ya kuandika hapa chukua hatua ndugu.
 
Asalam!!

Kama kichwa cha habari kisemavyo hapo juu, ni takribani mwezi sasa unaelekea kuisha tangu hii familia iwepo nyumbani kwangu!

Habari yenyewe kiundani wake iko hivi;

Mwenye familia ni ndugu wa mke wangu, Ni weekend moja ya siku za nyuma nilikuwa kwenye mihangaiko yangu ya kimaisha, niliporudi nyumbani jioni saa moja, nilimkuta huyo ndugu wa mke wangu yupo nyumbani kwangu akiwa na Familia yake yote, yaani Yeye, mke wake pamoja na watoto wake watatu!
Walilala nyumbani kwangu usiku huo, kesho yake mimi nikaamkia kwenye mihangaiko yangu, jioni niliporudi nyumbani sikumkuta nyumbani huyo jamaa, lakini watoto wake na mke wake walikuwepo!
Mimi nikajua labda yuko kwenye mizunguko tu atarudi baadae na pia nilijua wamekuja kutusalimia tu kwa muda wataondoka kesho yake, nilisubiri siku hiyo sioni mtu, ikawa usiku ikawa asubuhi, kesho yake hakuonekana tena! Nikamuuliza mke wangu!
Huyu ndugu yako vipi,akasema hana taarifa naye!
Nikasema isiwe shida madam ni mtu mzima atarudi!! Tumekaa siku kadhaa haonekani,nami sijataka kumtafuta kwenye simu!
Basi baada ya siku kadhaa akapiga simu kwa mke wangu akilalamika, eti maisha magumu sana siku hizi, wife akamjibu kwani tangu lini maisha yakawa mepesi!!!!

Jamaa akakata simu mpaka leo hii ninapoandika uzi huu, jamaa hajapiga simu tena, na familia yake bado iko kwangu!

Sasa shida inakuja kwenye bajeti ya nyumbani, imeshoot ghafla tangu jamaa alete familia yake, mi nina mke na mtoto mmoja, sasa hili ongezeko la watu wanne ghafla limebadilisha kabisa hali ya bajeti ya nyumbani,na ukizingatia hali ya uchumi ya sasa ilivyokaa, nashindwa kumudu mambo mengine,nilikuwa na kaujenzi imebidi nisimame kwanza ili nilishe familia nikitumaini kuwa jamaa atakuja kuchukua familia yake soon, lakini ndo hivyo jamaa kakausha utafikiri hajui kitu, na mimi huku maji yako shingoni, si unajua mshahara wa mwalimu Wa shule ya msingi, tena maisha ya Dar es Salam!

Samahani kwa kuwachosha ndugu wanaJF!

Ninachoomba kutoka kwenu ni kitu kimoja tu, ni ushauri namna ya kumwambia ili aje kuchukua familia yake, maana kila mtu atabeba msalaba wake mwenyewe! Mi uwezo wa kumtunzia familia yake umefikia kikomo, nimwambiaje huyu jamaa wandugu, make mpaka saizi nafikiria kesho tutakula nini, sijalala wala usingizi sipati, nawaza kesho itakuwaje, na jamaa kimyaa hadi muda huu!!!
Nisaidieni jamani!

Nawasilisha!!

Ali Choki alilalama siku za nyuma kuwa "Ukubwa Jiwe." Pole sana mkuu.
 
Ni ngumu kuamini yan mtu mzima aliyeolewa anawekwa mahali kama mzigo na yeye anatulia kimya..??

Kwani huyo mke wake ni mtoto mdogo kwamba hawezi kujishugulisha shughuli halali akatunza familia yake..?? Walemavu wanafanya kazi sembuse mwanamke..?? Lazima atakua na taarifa na mme wake, muulize nini mstakabali wao na mme wake huyo mke wa jamaa..!! Ukitunza hiyo familia umejitakia mwenyewe huo mzigo...! Hao wote bwana na mke ni watu wazima iweje uwatunze..?? Na wasivyo wastaarabu wanakuja bila taarifa alafu wanaloea, kama wana shida / maisha magumu si waseme wapigwe tafu...?? Acha uzembe kaka jiongeze....
 
Muambie wife kwamba kwa hali ilivyo sasa unaona bora umtangazie ndoa huyo mke ili awe mke mwenza wake, then poteza siku moja ukijiweka karibu ya huyo mke wa jamaa,

WIFE NDANI YA SIKU 2 TU ATAHAKIKISHA HUYO ANATOKA NA WANAWE BILA WW KUMLAZIMISHA KUWATOA.
best ushauri ever, au atafune tu huyo mama ili kuweka shinikizo la kuondoka. Huyu mwalimu analialia tu hapa simple solution ipo
 
Ni ngumu kuamini yan mtu mzima aliyeolewa anawekwa mahali kama mzigo na yeye anatulia kimya..??

Kwani huyo mke wake ni mtoto mdogo kwamba hawezi kujishugulisha shughuli halali akatunza familia yake..?? Walemavu wanafanya kazi sembuse mwanamke..?? Lazima atakua na taarifa na mme wake, muulize nini mstakabali wao na mme wake huyo mke wa jamaa..!! Ukitunza hiyo familia umejitakia mwenyewe huo mzigo...! Hao wote bwana na mke ni watu wazima iweje uwatunze..?? Na wasivyo wastaarabu wanakuja bila taarifa alafu wanaloea, kama wana shida / maisha magumu si waseme wapigwe tafu...?? Acha uzembe kaka jiongeze....
Binadamu ni mnyama kama mnyama mwingine yeyote wa kufugwa ama wa pori. Tofauti yake ni ndogo sana. Binadamu aliyekamilika ana kitu kinaitwa utashi. Hiki kitu hutufanya tutofautiane kidogo na makundi mengine ya wanyama. Hapo kwenye utashi nitaeleza mwisho wa comment yangu.
Hayo yote uliyoshauri, yana vikwazo vyake, ndiyo maana jamaa kaomba ushauri.
Jamaa katendewa unyama kutokana na ubinafsi uliopitiliza wa mtelekezaji, kwamba shida zake za kimaisha ni kubwa sana kuliko za wengine.
Ushauri ninaoweza kuutoa ni kama ufuatao.
Hatua ya kwanza ni kuripoti tukio hilo polisi kwa ajili ya kinga ya kashifa ama kesi yoyote ya kijingajinga dhidi yake itokanayo na msala huo.
Pili kuwasiliana na ukweni kwake kuwajulisha jambo hilo, ili waweze kufikia uamzi wa pamoja namna ya kuweka sawa jambo hilo, sasa inategemeana na ukweni kwake kupoje, iwapo familia ni yenye kueleweka au vurugumechi.
Kimsingi jamaa kabebeshwa jukumu lisilo la kwake.
Tuchukulie mfano huyo shemeji yake aliyetelekezwa, ingekuwa kapewa talaka angelikabidhiwa yeye? Je angelifiwa na huyo mmewe, hiyo familia angerundikiwa yeye?
Tatizo kubwa kama hilo pindi litokeapo, inawapasa wanafamilia (ukoo wa mme) kuchukua hatua mahsusi za kunusuru familia ya ndugu yao.
Hivyo huyo mwanamke anastahili kurejeshwa kwa wazazi wake ama kwao.
Gharama za nauli za kuwarejesha nyumbani kwao, kama kutakuwa na sintofahamu, basi jamaa abebe uzito kuliko kuendelea kukaa na hiyo familia ya mme mwenziye baradhuli.
Asitegemee shukrani yoyote toka kwa huyo jamaa aliyetelekeza familia yake kinyama.
Atakapokuja kurejea atakuja katika sura ya kudai haki zaidi.
Kwa hiyo jamaa achukue tahadhari na hatua madhubuti kuepusha balaa zaidi siku za usoni.
Hilo tukio hufanywa na binadamu wabinafsi ama wenye matatizo ya kisaikolojia.
Binadamu tunaongozwa na utashi katika maamuzi kwamba ni nini kibaya na nini kizuri cha kufanya kuweza kumkwaza ama kumpendeza mwingine.
Matukio ya aina hiyo yapo mengi sana.
Wapo wengine hutorokea kwake akiacha mke na watoto wakihangaika bila ya chochote. Akija kurejea huanza kudai haki kipumbafupumbafu.
Wanaume wa namna hiyo hawatofautiani na wanawake wanaotelekeza watoto wao baada ya kujifungua kwa visingizio mbalimali.
Hastahili kuendelea kuishi na hiyo familia, awarejeshe kwao ama kwa ndugu zao.
 
Daah. Pole sana ila hiyo itakuwa walidhamiria na huyo mke wake sio bure.

Na kwa usawa huu aisee pole mkuu mana lazima wakusomeshe namba.
 
Back
Top Bottom