USHAURI: Nimeachiwa Familia ya Mtu Bila Taarifa Rasmi!!

msesalonike

Member
Nov 4, 2016
29
95
Asalam!!

Kama kichwa cha habari kisemavyo hapo juu, ni takribani mwezi sasa unaelekea kuisha tangu hii familia iwepo nyumbani kwangu!

Habari yenyewe kiundani wake iko hivi;

Mwenye familia ni ndugu wa mke wangu, Ni weekend moja ya siku za nyuma nilikuwa kwenye mihangaiko yangu ya kimaisha, niliporudi nyumbani jioni saa moja, nilimkuta huyo ndugu wa mke wangu yupo nyumbani kwangu akiwa na Familia yake yote, yaani Yeye, mke wake pamoja na watoto wake watatu!
Walilala nyumbani kwangu usiku huo, kesho yake mimi nikaamkia kwenye mihangaiko yangu, jioni niliporudi nyumbani sikumkuta nyumbani huyo jamaa, lakini watoto wake na mke wake walikuwepo!
Mimi nikajua labda yuko kwenye mizunguko tu atarudi baadae na pia nilijua wamekuja kutusalimia tu kwa muda wataondoka kesho yake, nilisubiri siku hiyo sioni mtu, ikawa usiku ikawa asubuhi, kesho yake hakuonekana tena! Nikamuuliza mke wangu!
Huyu ndugu yako vipi,akasema hana taarifa naye!
Nikasema isiwe shida madam ni mtu mzima atarudi!! Tumekaa siku kadhaa haonekani,nami sijataka kumtafuta kwenye simu!
Basi baada ya siku kadhaa akapiga simu kwa mke wangu akilalamika, eti maisha magumu sana siku hizi, wife akamjibu kwani tangu lini maisha yakawa mepesi!!!!

Jamaa akakata simu mpaka leo hii ninapoandika uzi huu, jamaa hajapiga simu tena, na familia yake bado iko kwangu!

Sasa shida inakuja kwenye bajeti ya nyumbani, imeshoot ghafla tangu jamaa alete familia yake, mi nina mke na mtoto mmoja, sasa hili ongezeko la watu wanne ghafla limebadilisha kabisa hali ya bajeti ya nyumbani,na ukizingatia hali ya uchumi ya sasa ilivyokaa, nashindwa kumudu mambo mengine,nilikuwa na kaujenzi imebidi nisimame kwanza ili nilishe familia nikitumaini kuwa jamaa atakuja kuchukua familia yake soon, lakini ndo hivyo jamaa kakausha utafikiri hajui kitu, na mimi huku maji yako shingoni, si unajua mshahara wa mwalimu Wa shule ya msingi, tena maisha ya Dar es Salam!

Samahani kwa kuwachosha ndugu wanaJF!

Ninachoomba kutoka kwenu ni kitu kimoja tu, ni ushauri namna ya kumwambia ili aje kuchukua familia yake, maana kila mtu atabeba msalaba wake mwenyewe! Mi uwezo wa kumtunzia familia yake umefikia kikomo, nimwambiaje huyu jamaa wandugu, make mpaka saizi nafikiria kesho tutakula nini, sijalala wala usingizi sipati, nawaza kesho itakuwaje, na jamaa kimyaa hadi muda huu!!!
Nisaidieni jamani!

Nawasilisha!!
 
Akili Unazo!

JF-Expert Member
Feb 18, 2009
3,450
2,000

KWANI HUJUWI ANAKOISHI AU MKE WAKO HAJUI KWAKE AU FAMILIA YAKE HAIJUI ILIKOTOKA MPAKA TUKUSHAURI HUMU JAMVINI.. JE UNDUGU WALIO NAO NA MKE WAKO UKOJE KAKA NA DADA AU BABA MDOGO AU NI NANI..? JE UJIOO WAKE ULISHIRIKISHWA AU ALISHIRIKISHWA MKE WAKO?
 
the viking

JF-Expert Member
Apr 23, 2017
1,202
2,000
nmesoma mahali fulani jioni hii kuwa,"njooni nyote mliolemewa na mizigo,nanyi mtarudi nazo maana sisi pia tuna mizigo yetu"ifahamike sio maneno yaliyoko kwenye biblia..
 
Joseverest

Verified Member
Sep 25, 2013
42,853
2,000
Mkuu pole sana kwa unayoyapitia aisee, ni magumu mno..kuhudumia familia mbili hatari sana
 
hosh kosh

JF-Expert Member
Mar 2, 2017
755
1,000
Acha uoga mkuu,..mung ndo anaelisha viumbe zake we no asbabu tu tafuta kitakachopatikana na hiko hiko na wao wanaelewa ivo ivo ht mkila ugal chukuchuku hawatakusumbua..na huwo ni mtihan kwako kwa mung na familia ya mwanamke ..usiwafukuze wala kuwaonesha kitu kibaya ww ongea na mkeo mpnge mwambie bhn kitakachopatikana sasa ndo hiko hiko cz hal inaeleweka..ni hyo tu uvumilivu tu.
 
Nichumu Nibebike

JF-Expert Member
Aug 28, 2016
8,696
2,000
Pole mkuu, msaidie saidie kwa mwezi mmoja. Jamaa kaenda kurekebisha maswala yake... Ukiona mambo yamekuwa magumu, wapangishie chumba kimoja uwape debe mbili za mchele na debe moja la maharagwe na pesa kidogo warudi kwao kuendesha maisha (kama bado wana mahali pa kukaa)...
 
Matungiza

JF-Expert Member
May 6, 2017
524
500
Wafukuze, hatokuja kukushukuru kamwe bali akirudi atakudhihaki. Mfukuze usiku huu huu kama unasoma sms yangu.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom