Ushauri: Nichukue gari ipi kati ya hizi?

Mtoa mada ina maana umejenga nyumba zote hizo ukiwa unakwea bodaboda? Kuna kama ka chai flani hivi. Unless hizo nyumba ziwe unga unga mwana ila mtu anayejenga nyumba mbili za kawaida hawezi kosa hata IST maana bei yake ni kama Tiles za nyumba moja tu
Mkuu wengine gari tumezipanda ukubwani...so sio priority ukilinganisha na mahitaji mengine. Nina miaka zaidi ya kumi kaka nafanya vitu vingine tu nilipoona vinaisha ndo nikawaza niangalie upande huu pia.
Asante kwa maoni yako lakini
 
Mzee
Kwa namna ulivyojieleza nakutazama kama mhangaikaji asiyependa au anayependa but asiyekuwa na anasa---Maana yake hata muda wa kushinda na kutumia budget kubwa kwa matengenezo na visits za garage.
In that sense, mzee nenda kachukue Rav 4 pasipo kusita. Go go for it!!
Utaenda nayo popote, kwa barabara yoyote.
Real men na wapambanaji hujulikana kwa komenti km hizi. ASANTE mkuu
 
Nashukru Mkuu sana mkuu kwa mawazo
Mtoa mada hongera kwanza kwa kupambana na mpaka kufikia ulipo...

Kwa kuwa umeamua kuwa na SUV chipi hapa ndio ushauri wangu....

Binafsi nimeshatumia RAV 4 2006. Ilikua gari nzuri na imara. Issue yake kubwa ni lile tairi la nyuma ukiendesha sana rough roa inaulegeza ule mlango.

So sipendelei tairi la spair kukaa nyuma.

RAV 4 ya 2008-2010 ni nzuri tairi imeingizwa ndani na gari ina muonekano mzuri. Pia kutokana na bajeti yako kuwa mwisho 40m basi hizo zitakufaa....

Don't go for other brand out of toyota na nissan (mimi nilikuja kuopt for Dualis coz of budget).....

Go for TOYOTA RAV 4 2008-2010

Kuhusu site ya kuchagua ni moyo wako tu wa uvumilivu kutafuta mtandaoni..... Wote wana magari mazuri ila uwe mvumilivu na utenge muda wako ku search mtandaoni....

If you don't mind na kuondokana na usumbufu kuna vijana wanafanya hiyo kazi siku hizi. Unawalipa wanakuagizia mpk kufanya clearance na usajili..... (Nilitumia option hiyo baada ya kuchoka kutafuta mtandaoni).....

Good luc
 
Sasa mkuu mtu akiniagizia gari nitakuwa na uhakika gani na ubora wa gari hiyo?Si anaweza kunichagulia ambayo imechakaa sana?Si anaweza kunichagulia ambayo imeenda kilomita nyingi?
Hapana. Kabla ya kuagiza anakuonyesha kila kitu. Picha na specification zote. Na wao wanatumia site hizi hizi kina beforward, TCV na nyingine.....

Hivi ushaingia kwenye kuchagua gari ukakuta 10 enquiries? Wengi ni hawa vijana wana reserve magari huku wao wanatafuta mteja...
So kama haupo online muda mwingi unajikuta kila ukichagua gari unaambiwa under negotiation....

Hebu check hiyo picha hapo chini ya beforward.....

Pia angalia mfano wa picha ya pili wa hawa vijana wanaoshinda internet kukufanyia hiyo kazi..... (Hii ni kama upo busy)
Screenshot_2021-07-30-15-08-13-23.jpg
Screenshot_2021-07-30-15-11-05-69.jpg
 
Kluger haujaiweka, RAV4 sio mbaya na hapo 3 kwakuwa gari yako ya kwanza sikushauri sana
 
Kluger haujaiweka, RAV4 sio mbaya na hapo 3 kwakuwa gari yako ya kwanza sikushauri sana
 
Mkuu, kwa ushauri wangu (nimezingatia sana suala la wewe kuwa ni mgeni kwenye sekta hii) ningekutoa hapo ulipolenga nikakupa chaguzi hizi hapa chini:

TOYOTA Pixis Epoch G, 2010>
HONDA Life G, Zest 2010>
NISSAN Moco, Otti 2010>
MITSUBISHI EK Wagon 2010>

DAIHATSU Mira, Move, Esse 2010>
SUZUKI Alto, Wagon R, Palette 2010>
SUBARU Stella, Pleo, Lucra 2010>
MAZDA Carol 2010>

Hizi gari zote siyo SUV na bajeti ni chini ya m15, ili usevu hela nyingine maana hujui ya mbele, ila zinakuwa msaada mkubwa kwako kwani utaokoka na mengi sana hasa spea na usumbufu wa gereji kwa gari ulizotaja wewe, ila ukipenda ulivyoamua napo ni sawa, wafuate walioshauri juu wameshauri vizuri sana pia.
 
Anipe nani? Umezoea vya kupewa?

Mimi sipewi ila najinunulia. Kamwe siwezi kununua Dualis. Kwa sababu, by my perception it is for women.

Kama unayo Dualis, basi Mkuu endelea kupush, ila ipo kikike zaidi.
Kama gari zinaenda kwa jinsia basi IST na Vits zote ni za watoto wa sekondari sababu ni vidogo.

Hizo ni perceptions tu umejiwekea. Hakunaga gari ya kike au ya kiume.

We bili ya service ya Nissan Dualis unaijua mzee au unaongea kwasababu tunafurahishana hapa.

Uliza bei tu ya oil ya engine na gear box, hapo sijaongelea shock ups.....

Mzee kama haufahamu uliza.
 
Mkuu, kwa ushauri wangu (nimezingatia sana suala la wewe kuwa ni mgeni kwenye sekta hii) ningekutoa hapo ulipolenga nikakupa chaguzi hizi hapa chini:

TOYOTA Pixis Epoch G, 2010>
HONDA Life G, Zest 2010>
NISSAN Moco, Otti 2010>
MITSUBISHI EK Wagon 2010>

DAIHATSU Mira, Move, Esse 2010>
SUZUKI Alto, Wagon R, Palette 2010>
SUBARU Stella, Pleo, Lucra 2010>
MAZDA Carol 2010>

Hizi gari zote siyo SUV na bajeti ni chini ya m15, ili usevu hela nyingine maana hujui ya mbele, ila zinakuwa msaada mkubwa kwako kwani utaokoka na mengi sana hasa spea na usumbufu wa gereji kwa gari ulizotaja wewe, ila ukipenda ulivyoamua napo ni sawa, wafuate walioshauri juu wameshauri vizuri sana pia.
Nashukru sana mkuu kwa ushauri wako. Asante pia kwa mapendekezo, ila kwa sasa nilikua nahitaji aina au zinazoelekea na gari nilizozitaja.
Pia nafuatilia ushauri wa wengine pia km ulivyosema
 
Nawasalimu wakuu kwa jina la nguvu na uchakalikaji wetu.

Baada ya kupitia threads nyingi hapa na kujifunza mengi kuhusu magari nami natupia uzi hapa ili kupata ushauri.

Kiukweli mi mgeni sana wa magari hata kuendesha si mtaalam sana ila naweza sema sijakaa na gari tu nimesota kwa miaka 8 nasuhua bench kutimiza malengo mengine (nyumba ya wazazi kijijini nimemaliza na nyumba yangu mjini nimemaliza) nadhani mnajua ile hustle ya kuwa kichwa cha familia na umetoka kwenye umasikini wa kutupwa na baada ya kusoma ukoo mzima unakuangalia....

Mwaka huu nimejipinda nami nivute gari ya maana kidogo kwa matumizi ya familia na route ndefu km kwenda kijijini huko... (Naishi kanda ya kaskazini kwa rafiki zangu akina Mangi huku ila mimi ni mnyantuzu(Msukuma) kutoka kanda ya ziwa huko

Bajeti yangu ya gari inaanzia 30M-40M hivi, sasa ushauri nichague gari gani kati ya hizi?
1.Toyota
-RAV 4 New Model
-Lenus RX
-Harrier (Hapana nakubali ushauri)
-Vanguard (Hapana nakubali ushauri)

2.Nissan
-Muranno
-QSHANAI
-Dualis (hapana ila nakubali ushauri)
-X-Trail (hapana ila nakubali ushauri

3. SUZUKI
-Escudo Grand (Seat 7)
-Escudo (Seat 5)

Bajeti yangu inaangukia kwenye mid/lower SUV cars.

Kingine nataka kuagiza kutoka Japan (kulingana na maoni ya humu) ilq kuna jamaa yangu nimemshurikisha akasema bora nichukue yard but mimi nasita sababu ya kupata uzoefu wa yard kupitia jukwaa hili.

Pia naukiza ni kampuni gani nzuri kuagiza kati ya hizi
1.Be forwarded
2.SBT Japan
3.Enhance Japan

Natanguliza shukrani wa ushauri wenu na asanteni

Binafsi nakushauri uchukue harrier sababu kuu ikiwa ni muonekano wa ndani ila kama hutojali kuhusu uziri wa ndani chukua Rav 4 sababu ina ulaji mzuri wa mafuta kuliko harrier na pia ni imara zaidi kuliko harrier.Rav 4 in gear box kubwa yenye uwiyano sana na engine wakati harrier ina gear box ndogo ambayo haina uwiyano na engine hivyo kuifanya ile mafuta zaidi kuliko Rav 4.Otherwise kama unapenda luxury harrier utaenjoy
NOTE:Ukinunua gari jitahidi sana kutumia user manual kama sio mvivu wa kusoma itakusaidia na gari itafumu
 
Nakushauli uchukue toyota suf, ipo juu unaweza kwenda nayo popote ,ina but kubwa ya kubeba mzigo, lkn ipo kijanza zaid
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom