Ushauri: Nichukue gari ipi kati ya hizi?

Nawasalimu wakuu kwa jina la nguvu na uchakalikaji wetu.

Baada ya kupitia threads nyingi hapa na kujifunza mengi kuhusu magari nami natupia uzi hapa ili kupata ushauri.

Kiukweli mi mgeni sana wa magari hata kuendesha si mtaalam sana ila naweza sema sijakaa na gari tu nimesota kwa miaka 8 nasuhua bench kutimiza malengo mengine (nyumba ya wazazi kijijini nimemaliza na nyumba yangu mjini nimemaliza) nadhani mnajua ile hustle ya kuwa kichwa cha familia na umetoka kwenye umasikini wa kutupwa na baada ya kusoma ukoo mzima unakuangalia...😀😀😀😀.

Mwaka huu nimejipinda nami nivute gari ya maana kidogo kwa matumizi ya familia na route ndefu km kwenda kijijini huko... (Naishi kanda ya kaskazini kwa rafiki zangu akina Mangi huku ila mimi ni mnyantuzu(Msukuma) kutoka kanda ya ziwa huko😀😀😀

Bajeti yangu ya gari inaanzia 30M-40M hivi, sasa ushauri nichague gari gani kati ya hizi?
1.Toyota
-RAV 4 New Model
-Lenus RX
-Harrier (Hapana nakubali ushauri)
-Vanguard (Hapana nakubali ushauri)

2.Nissan
-Muranno
-QSHANAI
-Dualis (hapana ila nakubali ushauri)
-X-Trail (hapana ila nakubali ushauri

3. SUZUKI
-Escudo Grand (Seat 7)
-Escudo (Seat 5)

Bajeti yangu inaangukia kwenye mid/lower SUV cars.

Kingine nataka kuagiza kutoka Japan (kulingana na maoni ya humu) ilq kuna jamaa yangu nimemshurikisha akasema bora nichukue yard but mimi nasita sababu ya kupata uzoefu wa yard kupitia jukwaa hili.

Pia naukiza ni kampuni gani nzuri kuagiza kati ya hizi
1.Be forwarded
2.SBT Japan
3.Enhance Japan

Natanguliza shukrani wa ushauri wenu na asanteni
Chukua hio Rav 4.
 
Hivi kutuelezea kuwa umejenga mjini na kijijini ina uhusiano gani na hitaji lako la gari?
wewe unadai ni mkubwa ila bado mshamba,acha ushamba halafu jiamini,haya sasa ndio nakushauri,nenda kanunue VW,achana na hizo toys ulizoorodhesha hapo.
Aisee!
 
kama gari ni moja usinunue gari ya muingereza wala mjerumani nunua nenda Japan esp TOYOTA.
Nunua gari utakayoweza ihudumia kwa haraka ukipata tatizo nje ya mji.

Nina experience, gari ya muingereza na mgerumani ni mazuri sana ila linaweza kukulaza porini hata wiki kwa tatizo dogo tu la FUSE kukata.

MJAPAN FUNDI ANABYPASS WAYA UNAFIKA MJINI UNAPATA MSAADA.

Yaani usisafiri porini na hizi gari vijana wanazisifia sijui za kiume, mnyama sijui mashine. Ni mashine kweli ila tatizo dogo unalala porini, ukivuta gharama, ukiagiza fundi aje gharama, na likifika mjini unaenda A-art wanabadili fuse kwa Tsh 200,000/= bila VAT. Kwa ufupi unakuwa umebadili fuse kwa almost 1m na ulilala porini.
 
Mzee
Kwa namna ulivyojieleza nakutazama kama mhangaikaji asiyependa au anayependa but asiyekuwa na anasa---Maana yake hata muda wa kushinda na kutumia budget kubwa kwa matengenezo na visits za garage.
In that sense, mzee nenda kachukue Rav 4 pasipo kusita. Go go for it!!
Utaenda nayo popote, kwa barabara yoyote.
 
Katika gari za Nissan hapo juu, achana nazo zote isipokuwa X-Trail. The rest is mostly for women (I'm sorry to say). Mwanaume aliyekula age kama wewe, gari ndogo ndogo kama hizo ni za kuhonga tu au kumnunulia mama watoto.



Be a gentleman.

Suala la kujisikia mwanamke ukiendesha gari aina fulani ni suala binafsi na homon zako.

Sasa ukipewa hizo gari uendeshe itabidi upewe na taulo za kike usije ingia period ghafla yaani.
 
Suala la kujisikia mwanamke ukiendesha gari aina fulani ni suala binafsi na homon zako.

Wewe ukipewa dualis uendeshe itabidi upewe na taulo za kike usije ingia period ghafla?
Anipe nani? Umezoea vya kupewa?

Mimi sipewi ila najinunulia. Kamwe siwezi kununua Dualis. Kwa sababu, by my perception it is for women.

Kama unayo Dualis, basi Mkuu endelea kupush, ila ipo kikike zaidi.
 
Yaani usisafiri porini na hizi gari vijana wanazisifia sijui za kiume, mnyama sijui mashine. Tatizo dogo unalala porini, ukivuta gharama, ukiagiza fundi aje gharama, na likifika mjini unaenda A-art wanabadili fuse kwa Tsh 200,000/= bila VAT. Kwa ufupi unakuwa umebadili fuse kwa almost 1m na ulilala porini.
Tuachie sisi mkuu,tunasafiri nazo kila siku, changamoto za hapa na pale zipo tunapambana nazo.
 
Anipe nani? Umezoea vya kupewa?

Mimi sipewi ila najinunulia. Kamwe siwezi kununua Dualis. Kwa sababu, by my perception it is for women.

Kama unayo Dualis, basi Mkuu endelea kupush, ila ipo kikike zaidi.

Ofini kwako wewe au nyumbani kwako mnatumia gari za aina gani? Zote unajisikia ni wa kiume ukitumia? Au kwenye maisha yako huendeshi kabisa gari fulani fulani kwa hofu ya kujisikia wa kike?

Brand ambayo sijatumia ni mkorea na mhindi, nyingine nimetumia na sijawahi jisikia mwanamama.

Sina tatizo nikiwa nahitaji gari nikakuta hiyo dualis japo sijawahi ipenda wala kuifikiria kuinunua ndo ipo available kutumika, nitaindesha tu na sitajisikia wa kike.

Mambo ya kujisikia wa kike ukiendesha gari fulani ni mambo binafsi na homini zako.

Siku ukiendesha wakupe vitendea kazi usichafuke yaani.
 
Mkuu chukua eskudo kawaida siti tano. Grand vitara ninayo spare zake ziko juu sana mkuu. Lakini suzuki ni ngumu na zinadumu. Mara nyingi huudhurii garage tofauti na nissan cars. Kama unanunua nissan nunua ile model ya zamani kidogo. Hizi mpya nazo spea ni ghali na hazidumu mida mrefu
 
Back
Top Bottom