Ushauri: Ni zaidi ya miezi miwili kila siku nikiamka natamani kuoa

The patriot man

JF-Expert Member
Aug 16, 2015
968
1,064
Wakuu kwema?

Wakuu mimi ni kijana nina miaka 30 na pia nimuajiriwa na naishi peke yangu kwa zaidi ya miaka miwili. Sina biashara nyingine zaidi ya ajira ila kuna vikazi vidgo dogo vya computer huwa nafanyaga vinanipa hela.

Nimekua kwenye mahusiano na wanawake wengi tofauti tofauti. Mimi sio mgeni wa mapenzi hata ukisoma baadhi ya thread zangu hapa utaona nina visa vingi tuu vya mapenzi

Tatizo lipo hapa tokea mwaka huu mwezi wa 3 nilianza kutamani sana kuoa nikasema ngoja nijipe mda tuu labda ni mihemko tu.

Lakini aisee huwezi amini zaidi ya miezi miwili kila siku nikiamka natamani kuoa

Kilichonifelisha mpaka sasa hivi nina mwanamke zaidi ya mmoja na sijui nimuoe nani na wote ni wana chuo mmoja anamaliza mwakani mwingine 2025

Kidogo anayemaliza 2025 naona kama nampenda zaidi.

Mimi sijielewi ni mihemko au msaada please.
 
Back
Top Bottom