Marejesho ni zadi ya miezi miwili kila nikiamka natamani kuoa

The patriot man

JF-Expert Member
Aug 16, 2015
968
1,064
Wakuu kwema naimani mko poa.

Nililetaga uzi wangu hapa kuwa kila mda nilikua nawaza kuoa.

Sasa nilikua na Girlfriend wangu wa kitambo nikamcheki tukachati chati nikamsetisha akakubali nikamtumia nauli ya kutoka Arusha kuja dar akaja dar tukawa tunaishi wote hapo kumbuka sijamuambia kuwa nataka nikuoe nilimuita tuu aje nikae naye nisome upepo nikimuona anaeleweka ndo nimuambie. Umri wake ni 27.

Kaja nikamkaribisha vizuri kwa mara ya kwanza alikua April mara ya pili alikuja mwanzoni wa july.

Sasa tokea aje nilichogundua kuhusu yeye.

1.Anaongea sana alafu vitu vingi anavyoongea havina maana.
2.Mlalamishi yaani daaah.

3.Mbishi mbishi mpaka upige kelele ndo afanye
4.Hana shukrani.

5.Simu zangu zikipigwa anapokea yeye

6.Ananichunguza saana yaani mpaka kero.

7.Matumizi yangu yamekua makubwa naweza.
kutumia 8000 mpka 10000 wakati hyo ilikua ni hela ya siku 3 kwangu.

8.Msumbufu hapendi kuniona nimetulia mda wote ananisumbua, hataki nitoke.

9.Anataka umkubalie kila kitu hata kama hakina maana ukimkosoa anakuambia unanyanyasa.

Hitimisho nimeona siwezi ishi na mwanamke aisee kama ndo wanawake wote wako hivi.
Sifa yangu kubwa mimi sio muongeaji ni mkimya.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom