Ushauri:Ndugu kukudharau kwasababu huna kitu

bnyanya

Senior Member
Sep 27, 2013
178
195
Ndugu wana jf....kwa kweli nipo kwenye mtihani mkubwa sana na majaribu makubwa. Nimesoma mpaka elimu ya juu...sina kazi kwasasa. Yan wanafamilia plus ndugu zangu wananidharau mpaka daaah...kama kuna mtu imewahi kumtokea hali hii. Alifanyaje mpaka akafanikiwa??..au kuna mtu aliwahi kupitia hali hii??
 

TANMO

JF-Expert Member
Apr 12, 2008
9,988
2,000
Dharau dawa yake ni kiburi...

Ila siyo kile kiburi cha kijinga bali kile cha i know what i know and value who i am & f-ck the rest........
 

kibaravumba

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
6,153
2,000
Hili jambo lipo sana.Pengine linaweza kuzidishwa na tabia yako mwenyewe ya kudharau kazi ambazo unadhani zinatakiwa kufanywa na watu wasioenda shule.Cha msingi jiamini,fanya kazi yoyote hata kama ni kuuza nyanya.Usijali ingawa watakaoanza kukukejeli wanaweza kuwa ndugu zako,watu wako wa karibu na wasomi wenzio.Tumia elimu yako kama nyenzo ya kukuvusha juu dhidi ya fikra za wengi wakiwamo 'wasomi' wa vyeti wanaodhani kazi ya maana ni ya kuajiriwa tu.Nina rafiki yangu ana dip.lakini yuko anashona viatu na kung'arisha stand.Huwezi kuamini ukimwona alivyojiachia,lakini huweza kuingiza hadi laki moja kwa siku.Sina uhakika ni kiza gani huwaingia wasomi na kushindwa kuona fursa katika mazingira yao.Siku hizi pesa ndio kila kitu,usipokuwa nayo hata ndugu hutawaona.Lakini kwako hili linaweza kuwa somo.Kwamba siku utakapofaanikiwa,usijikweze na kuwatenga ndugu zako,kwani watapata maumivu kama unayopitia sasa

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 

kipimo

JF-Expert Member
Dec 30, 2010
828
0
kama bado unawahitaji tafuta hicho kitu ili wasikudharau, ila kama unaamini ktk unayoyafanya endelea na maisha yako tu kwani wale watabakim ndg zako tu ktk hali zote
 

Zyamwelele

JF-Expert Member
Aug 5, 2013
405
250
Ndugu wana jf....kwa kweli nipo kwenye mtihani mkubwa sana na majaribu makubwa. Nimesoma mpaka elimu ya juu...sina kazi kwasasa. Yan wanafamilia plus ndugu zangu wananidharau mpaka daaah...kama kuna mtu imewahi kumtokea hali hii. Alifanyaje mpaka akafanikiwa??..au kuna mtu aliwahi kupitia hali hii??


Jiangalie mkuu' huenda wew ndo chonzo cha hayo yote! Maana mara nyingi hayo nimatokeo yakujishaua na kujiona enzi ukiwa unasoma au katika maisha ya kawaida. Kwahari yakawaida haiwezekani watu wengi wakuchukie nakukudharau eti kisa hauna kazi.

Hata hivyo pole' jaribu kujishughurisha na ujasiriamali na usikate tamaa na maisha.

Kwamaelezo yako mafupi inaonekana ulikuwa na matarajio makubwa yakuajiriwa, baada yakukosa ajira umekata tamaa.
 

tototundu 1

Senior Member
Mar 8, 2013
138
195
Sa unataka heshima ya nini na kazi huna? Heshima pesa, tafuta pesa kwa style yoyote ile ukishazipata ndo utakapojua kuwa tajiri hanuniwi
 

ankol

JF-Expert Member
Aug 21, 2012
1,331
2,000
Pole ndugu. But kumbuka wanasema 'what do not kill you make you stronger'. Ninaimani ukijapata kajichance kadogo tu kakukuingizia kipato utatoka mbayaa.
 

LILENDI

JF-Expert Member
Oct 27, 2013
1,400
0
Ndugu wana jf....kwa kweli nipo kwenye mtihani mkubwa sana na majaribu makubwa. Nimesoma mpaka elimu ya juu...sina kazi kwasasa. Yan wanafamilia plus ndugu zangu wananidharau mpaka daaah...kama kuna mtu imewahi kumtokea hali hii. Alifanyaje mpaka akafanikiwa??..au kuna mtu aliwahi kupitia hali hii??

pole sana mkuu! naomba ujibu maswali yafuatayo:
1. wewe ndo msomi pekee ktk familia?
2. hao wanafamilia walishiriki kukusomesha?
3. tabia zako wakati unasoma, hasa elimu ya juu na mara baada ya kumaliza zilikuwaje?

mi nilikuwa nadharauliwa na baadhi ya ndugu wakati nasoma. nilipoingia tu elimu ya juu, wakaanza kujigonga shenzi type. ninakaajira kangu, siwasaidii saana hao ndugu zangu lakini tunaheshiana sana tu.. ukiachilia mbali viatu
 

BADILI TABIA

JF-Expert Member
Jun 13, 2011
31,391
2,000
ni kwamba wanakufharau

Au unahisi wanakudharau

Dawa ni kupambana

Kama ajira zimegoma uza hata genge mpaka kieleweke
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom