Ushauri: Ndani ya vituo vya mwendo kasi kuwekwe huduma muhimu kama ATM na Vyoo, n.k

Kwamba simu za mkononi zilipata kupingwa hivyo hivyo, kuna watu walikuwa na vyombo vya kuzuia mawimbi, basi tu ilimradi cell phones zisipate nafasi! kukebehi, kudhalilisha, kwamba haiwezekani, kwamba ni mawazo ya CCM sidhani kama yatatupa maendeleo! Cha kushangaza simu hazina chama, maendeleo hayana chama, kama kila idea ya maendeleo wapinga sababu ya chama basi mwenzetu una issue zako..
Nakumbuka hata hizi Computers zilivyoingia, zilipata kupingwa na kukebehiwa sana sana, hasa wakina baba, wao walidhani ni typewriter, basi wakiona mwanaume anasomea ilikuwa shida! Njemba nzima inasomea kuwa typist! Kumbe mwenzao anapiga programming na ku operate application programs! Kwa kweli akili ni nywele...
haha kweli mkuu
 
ATM
Choo
na huduma ndogo ndogo muhimu ziwekwe nazo. nyie vipi bwana mnaachaje hela ya nje nje, pili mnakuwa mmetoa huduma na kupunguza usumbufu?
au mnasemaje wadau
Wakifanya hivyo sio tu uhalifu utaongezeka kwenye hivyo vituo, bali kuna wadau pia wataomba wafungue na pub/bar kabisa.
 
Wakifanya hivyo sio tu uhalifu utaongezeka kwenye hivyo vituo, bali kuna wadau pia wataomba wafungue na pub/bar kabisa.
Uhalifu hata bila hivyo vitu upo mkuu, natumaini wataweka CCTV cameras na polisi wetu kurandaranda, tutazoea tu, ofcourse watu waovu hawapendi mwanga, twategemea taa za kutosha..
 
Nyie wachangiaji mbona sijamwona hata mmoja aliyesemea viti vya kukalia? Njia nzima kuanzia Kivukoni mpaka Kimara mwiso kuna viti Ubungo na Kivukoni peke yake. Hebu fikiria namna wagonjwa na kina mama wajawazito wanavyoteseka kusimama kwa muda mrefu hasa wanapokuwa wanasubiri mabasi ya Gerezani na Morocco.!
 
Back
Top Bottom