Ushauri: Nawaza kuuza kiwanja nifanye biashara baada ya kufukuzwa kazi. Nina familia inayonitegemea

Kaombe kazi za chapu chapu sehemu kama ukuli, kumenya chipsi, deiwaka saloon, kusaidia fundi ujenzi, deiwaka boda boda au bajaji, nenda minadani muuzie mtu vitu vyake kama mitumba, vyombo, mazao halafu kamisheni atakulipa huku unaweka akili yako sawa.

Usiuze kiwanja, anza kujengea mabati kama mdau alivyo sema hapo.

Adui yako mkubwa ni status quo, ngoja nikwambie ukweli sisi binadamu tulikuja uchi na tutaondoka bila chochote, usijionee aibu uko uchi tayari usiangalie kushoto wala kulia pambana kianaume, acha wakuseme wala hutomeguka.
Hii ndo point sasa
 
Umenena vizuri. Hebu haraka haraka fasta tuambie kijana wetu afanyeje? Usiniambie auze genge maana nayo Ni biashara. Usiniambie akabebe zege au arudi shamba kwa Kijiji.
Auze chupi za kike kwenye malango ya vyuo na shule
Chupi moja bei ya jumla 500 bei ya kuuza 100
Chupi kumi manunuzi 5000 mauzo 1000
Faida 5000
Huo ni mfano mdogo tuu
 
Aaah! Mkuu usimkatishe tamaa nadhani anatakiwa awekeze nusu ya mtaji ikitokea mambo yakaharibika ile nusu ingine itamsaidia lakini pia atakuwa amepata uzoefu huwezi Fanya biashara kwa Mara ya kwanza bila kupata hasara.
Ben nimeandika kutokana na uzoefu...angalia wastaafu wengi waliishia kufa baada ya kuwekeza pensheni kwenye biashara bila kuwa na uzoefu
 
Hizi za mambo za kukimbilia kufanya biashara kwa sababu umefukuzwa kazi ni mbaya sana ..kwa sababu kwanza muhusika hana uzoefu na "biashara yeyote ile" ..pili muhusika atafanya biashara siyo kwa kupenda, ni kwa sababu kafukuzwa kazi na ana familia inayomtegemea, hivyo anawaza watoto watakula nini. Kwa iyo itapelekea wewe muhusika kufanya ndivyo sivyo.

Unajua ninyi mnapokuwaga kazini mnatuonaga sisi wajasiriamali ni wajinga sana kana Kwamba tumekosa kazi hivyo tunafanya tu vibiashara vyisivyo na mbele wala nyuma ili kupata ela za kula.. unapotimuliwa kazini sasa ndo kimbembe kinaanza..hujui nini cha kufanya, hujui huanzie wapi, huna hata akiba (hili ni kosa kubwa) hapo ndo unafanya maamuzi ya ajabu kama hapa braza ana kiwanja anataka kuuza ila hajaplan akiuza iyo pesa atafanya biashara gani.

Kwanza bro pole sana, cha kwanza cha kufanya tafuta nini ambacho unaweza kufanya kwa sasa, kila mwanadamu ana strengths na weakness zake.
Usikurupuke kufanya kitu ambacho hujawahi kufanya kabisa. Tafuta watu ambao unaona wanafanya kitu ambacho wewe utaweza kufanya, then waulize wao wanafanyaje ili kupush..

Wekeza zaid kwenye Muda na siyo kwenye kupata pesa tu ..yani tumia sasa Muda wako kujua ni kitu gani ambacho unaweza kufanya halafu angalia sasa namna gani utaanza kufanya hizo harakati. Ukishapata mishe ya kufanya tafuta sasa pesa (lakini nakushauri usiuze kiwanja) hata kwa kukopa ukiwa na uhakika wa uwekezaji sehemu.

Bado una nafasi ya kuanza mpya ila ukubali kuanzia chini kabisa. Narudia tena angalia nini ambacho unaweza kufanya kwa sasa ..kabla ya kutafuta pesa ili usifanye biashara ambayo hujui inafanywaje.

Angalia eneo gani upo vizuri then anzia hapo hapo. Maisha lazima yaendelee..

Pambana.
 
Hiki ulichoandika hakitabadili uhalisia wa kile nilichoandika
Ni lazima uwe mtu wa kufikiri zaidi ya kufikiri...nimemwambia kama HAJAWAHI kufanya biashara kuuza kiwanja chake
Biashara ni taaluma yenye abc zake
Kuna aina ya biashara
Kuna eneo sahihi la biashara
Kuna mtaji
Kuna malighafi
Kuna matumizi
Kuna wateja
Kuna faida
Kuna hasara
Usijifanye motivational speaker ukamuingiza chaka mwenzako...kumbuka alichonacho ni kiwanja tuu ...biashara zikifeli kiwanja amekiuza unadhani atapata maumivu mara ngapi?
Mkuu ni kweli kabisa,,
Usiuze Kiwanja kwa lengo la kufanya biashara,, majuto Mara 2 mkuu.
Bali uza Kiwanja ununuwe Kiwanja kingine + ufanye biashara..
Hakuna kitu roho inauma Kama uuze chako na bado shida zipo pale pale.
 
ungeuza hiyo simu , hela kidogo utakayopata mwannzishie wife biashara ndogondogo kama vitumbua, maandazi ,samaki nk...ili mpate hela ya kula....halafu wewe angalia kama unaweza kukopea kiwanja then angalia mahiitaji ya hapo mlipo ufanye biashara
Simu hasa smartphone sio anasa ni connection mhimu sana angepata vipi ushauri humu angekua anatumia kitochi?
 
USHAURI WANGU!

Uza kiwanja mkuu,faida ya kuuza kiwanja ni nyingi kuliko kukiacha eti kwa kuogopa sijui pesa itaisha au kupotelea kwenye biashara.

Ukishauza,pesa utakayoipata kama itakuwa ni kubwa angalau zaidi ya 5M,basi lipa kodi ya nyumba miezi sita au zaidi kutegemea unalipaje kwa mwezi,kama unalipa kodi bei nzuri lipa hata mwaka,nunua chakula cha kutosha angalau mwaka mbele au zaidi.

Watoto kama wanasoma shule za kulipia wahamishe ,wapeleke serikalini wakasome huko sio dhambi mkuu mambo yakibana.Hata sisi wengi wetu humu tumesoma hizo hizo shule.

Ukishaweka mambo hayo mawili sawa,yaani chakula, kodi ukahakikisha utaanza kudaiwa baada ya miezi sita mbele au zaidi,basi chukua pesa iliyobaki jitose kwenye biashara,nenda sokoni hapo ulipo tafuta meza ya kukodi.

Mara nyingi kodi za meza za sokoni hasa masoko yetu kodi haizidi 30,000/= kwa mwezi ingawa inategemea na mahali,hapa kwetu jijini unaweza kupata hadi meza ya 15,000/= kwa mwezi,maana watu wengi wamepuuza meza wanajiachia kwenda kuuza nje.si unajua ni uhuru wa machinga mkuu? Popote kambi.

Ukishachukua meza lipia nayo hata miezi mitatu,anza kuuza dagaa wa Mwanza (ziwa victoria) na dagaa wa chumvi(dagaa wa nyama) kutoka Zanzibar au Tanga.,sijui huko ulipo mnaziitaje,nunua kiasi kidogo kwanza,ili uanze kupata uzoefu taratibu utakuwa unapandisha mtaji kadiri unavyojifunza ukiwa sokoni.

Anza hata na laki tano kwanza kutoka kwenye hiyo pesa ya kiwanja iliyobaki sijajua utauza shilingi ngapi,nimekadiria uuze kwa 5M bei ya kiwanja.,iliyobaki weka akiba utakuwa unaongeza kutegemea na uzoefu,maarifa unayopata sokoni,pia wateja wako wakiwa wengi taratibu unaongeza mzigo.

Kumbuka hapo unafanya biashara bila wasiwasi ya kudaiwa pesa sijui ya kodi au chakula nyumbani,ni taratibu tu,pia unaweza kufunga kwa pakiti baadhi ya dagaa zako ukawa unasambaza kwenye maduka mtaani unawauzia kwa bei nzuri ya sokoni,hakika utapata wateja wa maduka ya akina mangi wengi.ukishawapa dagaa za pakiti pesa utakuwa unapitia baada ya siku tano ,harafu unawaachia tena mzigo.

Hapo kusambaza mzigo ni kama partime tu,sio kwamba ndo utegemee hilo soko,hapana hapo unapanua wigo wa soko kuuza mzigo wako.

Hapo mkuu ,ukifanya kwa dhamira kuu kabisa,na uchungu wa kufukunzwa kazi,na kuhakikishia baada ya miezi sita utakuwa umeshaanza kuona angalau mwanga kidogo kwenye biashara hiyo ya dagaa.

Nitakuwa nakupa ushauri kidogo kidogo kadiri utakavyokuwa unaendelea,(kama ukitaka)maana Nina uzoefu na kile ninachokushauri kimewasaidia wengi na Mimi pia.

Biashara ndio njia itakayokupa utajiri(mafanikio) yasiyo na manyanyaso ingawa inahitajika kujitoa haswa.Maana karibu 98% ya watu wanaotuzunguka wanaogopa biashara,na wanaamini kwenye kuajiriwa tu.

Ukigusia biashara,utawasikia aah,hapana bora tafuta Kazi biashara ni ngumu na inahitaji uzoefu,sasa uzoefu ataupataje asipofanya biashara?

Hakuna namna kwa sisi vijana ya kujikomboa kiuchumi kama akili zetu zitakuwa zinawaza kuwa sehemu salama tu(kuajiriwa).maana wengi ndio wanavyodhani kuwa kuajiriwa ni sehemu salama.

Lazima vijana tuungane kwa nguvu zetu,umoja wetu,uzoefu wetu,maarifa yetu na kwa uaminifu kabisa ,tuwe suruhisho kwenye jamii na Taifa letu kwa ujumla.

Nina imani watu wana mawazo mazuri,wana muda mzuri, wana maarifa mazuri,wana mitaji mizuri,na mtandao wa watu wazuri,shida UAMINIFU,nani wa kushirikiane naye mwenye ndoto na maono makubwa na ya kitofauti?

Watu wanakufa na mitaji yao,wanakufa na mawazo yao,wanakufa na maarifa yao,wanakufa na mtandao wa watu wazuri walionao pasipo kuutumia kwa faida.KISINGIZIO ni UAMINIFU tufanyaje vijana ili tuweze kuaminika kwa watu wenye mitaji?,wenye mawazo Na maarifa sahihi?

Au zile methali tena hazina ukweli? Kidole kimoja hakivunji chawa,umoja ni nguvu utengano ni udhaifu?
UMOJA WETU NDIO NGUVU YETU.karibu kwa ushauri na ushirikiano wowote ule wa kibiashara,ujasiriamali na uchumi.
Asante kwa kunisoma!
 
Back
Top Bottom