Naomba ushauri: Mshahara wangu ni mdogo sana; hautoshelezi mahitaji yangu na familia inayonitegemea

Melancholic

JF-Expert Member
Oct 12, 2018
1,831
3,063
Mimi ni muajiriwa wa kampuni X, ila kiukweli mshahara ni mdogo sana nalipwa 250/month.

kiukweli hii pesa nashindwa kuigawa coz ni ndogo, 90% inaisha kwenye kula na matumizi mengine madogo madogo. Ni changamoto kiasi kwamba nashindwa hata kununua aset za ndani sababu pesa yote inakwisha najikuta hata akiba sina kabisa ukiweka kodi na mambo mengine.

Kutokana na ugumu ninaopitia imenifanya nijiweke kando kabisa na masuala ya mahusiano sababu kiuchumi sipo vizuri, pamoja na yote hayo lakini bado kusave pesa inakuwa changamoto.

Ndugu zangu najua humu kuna watu wanapitia changamoto kama zangu au walishazipitia hivyo wana uzoefu wa kutosha namna ya kusurvive kwa kiwango hiki cha mshahara, na ni vipi unaweza kujiongezea kipato kupitia mshahara kama huu niupatao.

Hivyo nahitaji mawazo yenu ni vipi naweza kujianzishia hata kibiashara kidogo kupitia mshahara huu na nikakuza kipato changu coz mzigo nilionao ni mzito sana.

Naomba ushauri na mawazo yenu ndugu zangu coz JF ni mtandao mpana wenye watu waelewa na mitazamo mikubwa.

Note: Naweza nikajibana bana kibishi nikafikisha laki 5 endapo nitapewa wazo chanya la biashara.

Nipo Dar es Salaam.
 
Unahitaji nidhamu kubwa sana ya pesa hiko ni kiwango cha Boom nakumbuka nlikua naishi na hiyo hela na kulipia kodi the bad thing now gharama za maisha ni kubwa..Tuendelee kupambana mpaka hapo umepambana sana
Shukran mkuu kwa kunipa moyo
 
Hata ikatokea ukalipwa laki 6 kwa mwezi, bado haitatosha. Na kwa ufupi tu mshahara hautoshi. Hivyo unatakiwa kujiongeza kwa kuanzisha kashughuli ka kukuongezea kipato kila mwezi.
 
Mkuu kwani kosa lipo wapi kuomba mawazo chanya ikiwa huna ushauri ni vema unyamaze kuliko kuropoka ujinga wako hapa
Ujinga kitu gani angalia fursa zingine mbona tuna matoto ya ndugu kibao tunasupport ada wewe hao nduguzo chakula tu unataka forum isimame Ebho!!! Kuwa serious basi last born
 
250, n pesa ndgo kwa mwez kama huna kipato kingne…hvyo fanya namna uongeze kipato kwa kufanya biashara kwa muda wako wa ziada na weekend,hatuwez kukushaur uache kaz wakat huna kipato kingne

Kijana,

Zingatia haya

1.pangilia matumiz yako vizur,punguza yote yanayopunguzika ili angalau uweze kusave 50 had 100 kwa mwez kama sehem ya mtaji unatunza .fanya hv kwa miez kadhaa min 6

Nb.kama unagodoro,jiko,vyombo kias wachana na asset za ndan n ANASA kwako kwasasa,kwaza sio productive na huwez kuafford hyo pesa ifanye mtaji

Kipengele cha mahusiano kuyaacha sio busara labda kama utajiweza kuthibiti hisia zako vingnevyo tafuta kabint ka viwango vyako ambako sio kafujaji ukikapa hata 5k kanardhka

2.wakat huohuo weka ratiba zako vzr zinabe haswa upate muda wa ziada baada ya kaz na weekend

3.tafuta idea ya mtaji mdogo unayoweza iendesha kwa mtaji mdgo lkn ikawa smart mfano kuuza matunda ya package nk

4.hakikisha unajifunza Elimu ya fedha kuptia vitabu,mabandko na majarda,google nk kadri unavyojifunnza ndvyo unavyozid kupata ufaham na kujitawala sana kwenye eneo la fedha..

Nakutakia utekelezaji mwema
 
Ujinga kitu gani angalia fursa zingine mbona tuna matoto ya ndugu kibao tunasupport ada wewe hao nduguzo chakula tu unataka forum isimame Ebho!!! Kuwa serious basi last born
Kaa kimya huna akili wewe usikute hapo unatype ukiwa kwa shemej yako ukisubili chakula cha mchana
 
250, n pesa ndgo kwa mwez kama huna kipato kingne…hvyo fanya namna uongeze kipato kwa kufanya biashara kwa muda wako wa ziada na weekend,hatuwez kukushaur uache kaz wakat huna kipato kingne

Kijana,

Zingatia haya

1.pangilia matumiz yako vizur,punguza yote yanayopunguzika ili angalau uweze kusave 50 had 100 kwa mwez kama sehem ya mtaji unatunza .fanya hv kwa miez kadhaa min 6

Nb.kama unagodoro,jiko,vyombo kias wachana na asset za ndan n ANASA kwako kwasasa,kwaza sio productive na huwez kuafford hyo pesa ifanye mtaji

Kipengele cha mahusiano kuyaacha sio busara labda kama utajiweza kuthibiti hisia zako vingnevyo tafuta kabint ka viwango vyako ambako sio kafujaji ukikapa hata 5k kanardhka

2.wakat huohuo weka ratiba zako vzr zinabe haswa upate muda wa ziada baada ya kaz na weekend

3.tafuta idea ya mtaji mdogo unayoweza iendesha kwa mtaji mdgo lkn ikawa smart mfano kuuza matunda ya package nk

4.hakikisha unajifunza Elimu ya fedha kuptia vitabu,mabandko na majarda,google nk kadri unavyojifunnza ndvyo unavyozid kupata ufaham na kujitawala sana kwenye eneo la fedha..

Nakutakia utekelezaji mwema
Ahsante mkuu haya ndio mawazo tunayoyahitaji humu barikiwa sana
 
Back
Top Bottom