Ncha Kali
JF-Expert Member
- Sep 19, 2019
- 14,523
- 27,021
Wakuu, yamenifika hapa
Nimekuwa nikiishi na binti wa watu kinyemela kwa takribani miezi MINNE sasa. Tulianza kama masikhara, mwisho nikamruhusu ahamie ili nijihakikishie tunda kila nikiwa na KIU.
Stori iko hivi:
Nilikutana na binti ambaye yupo kwenye kupambana aanze maisha. Alikuwa akiishi kwa dada’ke kipindi hicho. Katika stori za hapa na pale, binti akagusia hitaji lake la kujitegemea kimaisha. Japo kwa chumba kimoja tu, ili aondokane na kuishi kwa dada (shemeji).
Kumuuliza mipango yake ipoje, kasema anahitaji kiasi cha kodi tu. Na itamchukua miezi MITATU ikiwa ataitafuta kupitia kazi anayofanya.
Wakati huo tulishawahi kujadili lengo lake la kuanzisha ofisi yake ili tu awe na kazi yake. Hapa aliomba 'sapoti' yangu na nilimuahidi.
Basi bwana! Nikaona kitonga si hii, nikamwambia ahamie kwangu ili tuishi kwa hiyo miezi MITATU huku akijiandaa kupanga. Maaweee! Mtoto bila hiyana akafungasha, kaaga kwa dada’ke ya kuwa amepata chumba anahamia. Kapewa jiko dogo la gesi, na beseni kama zawadi ya kuanzia maisha. Huyu hapa.
Basi maisha yakaanza, yakasonga. Ahadi yangu nikatimiza akafungua ofisi yake, ikawa sasa kila anachopata anaboresha ofisi yake. Siku nikigusia kuhusu maandalizi yake ya kupanga anakuwa mkali balaa, nimvumilie hajaanza kupata faida, nikisema nimlipie kodi utasikia ooh nimemchoka nataka kuleta MKE mwingine!
Kumbe mwenzangu alisha-update STATUS, alishakuwa MKE tayari. Mwanzo nikadhani utani, siku zinasonga AKILI inazidi kunirudi.[emoji15. Sasa nawaza namna gani ya kuondokana naye kwa amani, sitaki kuoa wala sitaki kumuumiza kwa kumpotezea muda. Ingawa kwa hili labda aamue tu kunigeuka.
Hakuna namna ataweza kunishawishi kwenye mtazamo wangu juu ndoa, na hata msimamo wangu juu yake nilimweka wazi tangu mwanzo.
Jibu lake lilikuwa kama langu, kwamba hata yeye hahitaji kuolewa saivi anatafuta MAISHA kwanza. Ni wasiwasi wangu tu, naishije na mtu kinyemela muda wote huu. Japo hatuombei ya kutokea, God forbid!
Naombeni ushauri wenu ndugu zangu, hii ni tukio halisi linaloendelea sasa mubashara kwa ndugu yenu.
Natanguliza shukrani.
Ncha Kali.