Ushauri, natokaje hapa?

Ushauri, natokaje hapa?

Wakuu, yamenifika hapa!

Nimekuwa nikiishi na binti wa watu kinyemela kwa takribani miezi MINNE sasa. Tulianza kama masikhara, mwisho nikamruhusu ahamie ili nijihakikishie tunda kila nikiwa na KIU.

Stori iko hivi:

Nilikutana na binti ambaye yupo kwenye kupambana aanze maisha. Alikuwa akiishi kwa dada’ke kipindi hicho.

Katika stori za hapa na pale, binti akagusia hitaji lake la kujitegemea kimaisha. Japo kwa chumba kimoja tu, ili aondokane na kuishi kwa dada (shemeji).

Kumuuliza mipango yake ipoje, kasema anahitaji kiasi cha kodi tu. Na itamchukua miezi MITATU ikiwa ataitafuta kupitia kazi anayofanya.

Wakati huo tulishawahi kujadili lengo lake la kuanzisha ofisi yake ili tu awe na kazi yake. Hapa aliomba 'sapoti' yangu na nilimuahidi.

Basi bwana!
Nikaona kitonga si hii, nikamwambia ahamie kwangu ili tuishi kwa hiyo miezi MITATU huku akijiandaa kupanga.

Maaweee! Mtoto bila hiyana akafungasha, kaaga kwa dada’ke ya kuwa amepata chumba anahamia. Kapewa jiko dogo la gesi, na beseni kama zawadi ya kuanzia maisha. Huyu hapa.

Basi maisha yakaanza, yakasonga. Ahadi yangu nikatimiza akafungua ofisi yake, ikawa sasa kila anachopata anaboresha ofisi yake.

Siku nikigusia kuhusu maandalizi yake ya kupanga anakuwa mkali balaa, nimvumilie hajaanza kupata faida, nikisema nimlipie kodi utasikia ooh nimemchoka nataka kuleta MKE mwingine!

Kumbe mwenzangu alisha-update STATUS, alishakuwa MKE tayari. Mwanzo nikadhani utani, siku zinasonga AKILI inazidi kunirudi.

Sasa nawaza namna gani ya kuondokana naye kwa amani, sitaki kuoa wala sitaki kumuumiza kwa kumpotezea muda. Ingawa kwa hili labda aamue tu kunigeuka.

Hakuna namna ataweza kunishawishi kwenye mtazamo wangu juu ndoa, na hata msimamo wangu juu yake nilimweka wazi tangu mwanzo.

Jibu lake lilikuwa kama langu, kwamba hata yeye hahitaji kuolewa saivi anatafuta MAISHA kwanza. Ni wasiwasi wangu tu, naishije na mtu kinyemela muda wote huu. Japo hatuombei ya kutokea, God forbid!

Naombeni ushauri wenu ndugu zangu, hii ni tukio halisi linaloendelea sasa mubashara kwa ndugu yenu.

Natanguliza shukrani.

Ncha Kali.
Mishe zako si zinaenda kama kawaida?? Oa tu. Achana na maisha ya kisela. Maisha ndivyo huanza..
 
Hapa ndipo unafeli mzee. Fikiri kwa kina. Ingekua ni below standard usingepaswa kusubutu hata kumtongoza.

Kutongoza unapaswa kutongoza kila mwanamke mbele yako, kuna vitu ukiwa naye ndo utagundua hutoweza kuishi naye for life.
 
Nawatakia maisha mema ya ndoa

Tafuta room kimya kimya ukipata hama akiwa hayupo ila dhambi hii hainihusu
 
Kutongoza unapaswa kutongoza kila mwanamke mbele yako, kuna vitu ukiwa naye ndo utagundua hutoweza kuishi naye for life.
Kuwa makini na neno standard maana ni pana sana

Angalia usije pata standard yako alafu akawa kichomi balaa

Alafu kwanini unaishi na mwanamke nearly 4 months alafu sio standard yako. Inashangaza kwa kweli
 
Kuwa makini na neno standard maana ni pana sana

Angalia usije pata standard yako alafu akawa kichomi balaa

Alafu kwanini unaishi na mwanamke nearly 4 months alafu sio standard yako. Inashangaza kwa kweli

Sababu za kuishi naye zimeainishwa post #1 hapo juu, kuhusu standard (viwango) ni muhimu kuzingatiwa.

Hata ingekuwa ni mpango wa kuoana, basi kipindi cha uchumba au hata kabla... hufanyika upembuzi yakinifu.
 
Na nyie mnaojifanya hamtaki kuoa mnakamatwaga kizembe sana,apo ushaoa brathee,sema tu we hujajua,kikubwa halalisheni tu.

Sijaona ukisema anashida ya kitabia au laah,hivyo anaonekana ni mwanamke anaefaa kuoa.

Oa mkuu
 
Na nyie mnaojifanya hamtaki kuoa mnakamatwaga kizembe sana,apo ushaoa brathee,sema tu we hujajua,kikubwa halalisheni tu.

Sijaona ukisema anashida ya kitabia au laah,hivyo anaonekana ni mwanamke anaefaa kuoa.

Oa mkuu

Hana shida kitabia, ni kawaida tu kama wengine... kuoa kizembe ndicho ninachofikiria kujiepusha nacho.
 
Ok hupo tayari kuoa kwa sasa,lakini huyo ana vigezo vya mke umtakae?,wasi wasi wangu tu unamtupa huyo unaenda kuangukia kwenye mikono ya kicheche na kujutia.
 
Hata kuhama mwenyewe nako kutamfanya aone kua umemchok, kumbuka hapo njia ni kumfanya apange bila kumuumiza

Kwanza hakikisha unauhakika kua anaweza kujimudu kupitia ofisi yake anayoiendesha.

Halafu unaweza kumdanganya kua kuna pesa ulikopa na time ya kurudisha inakaribia kufika na uliweka rehani mali za ndani na kwasasa pesa hiyo hauna. (Hapo unaweza ukaingizia na ile pesa ambayo ulimpa kwa ajili ya kufungulia ofisi yake kua ilitokana na ule mkopo)

Baada ya hapo mtafute msela wako umpange kua baada ya siku fulani aje kuchukua vitu vyako vya ndani avitaifishe. Halafu we jidai kua unalala kwa geto la msela

Baada ya hapo msikilizie kama unaukauzu wakulala kwenye sakafu na pesa ya kununua mahitaji hayi imekunjwa kwenye pindo la kanga

Ukiona katusua hadi mwezi akiwa yupo kwenye sajafu, nakushauri bro rudisha vitu vyako uje umuoe huyo ndo wife material anaijua misoto hawezi kukuacha hata katika kile kipindi ambacho utakua umekwama
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom