Jirani yangu anafanya kazi gani?

haszu

JF-Expert Member
Oct 10, 2017
837
1,550
Sio kwamba namchunguza, ila natamani namimi niishi life style kama yake, mana wengine tunachapika na maisha huenda kuna watu wana shortcut.

Ni miaka miwili tangu amalize nyumba yake na kuhamia,
1. Amejenga ndani ya miezi miwili au mitatu.

2. Tangu ahamie, muda wote yuko ndani, mara kadhaa hutoka au husafiri na ananiaga ila hakai hata wiki anarudi.

3. Anaagiza mahitaji kwa boda au mara nyingine anatoka, (hii sio ajabu sana).

4. Kuna mdada/ wadada wanakuja ila hawakai sana wanaondoka, jamaa yuko mwenyewe

5. Hana kufulia, au aje aombe kitu, mimi ndo niliwahi kwama nikamfata aniazime kiasi cha pesa.

6. Kusema ni jambazi anatoka usiku hapana, mana hata usiku yupo, na ni mpole sana hana shida na mtu.

Je, anaishije?
 
Dunia imebadilika sana siku hizi, ofisi sio kama zamani kwamba hadi uvae nguo, uendeshw gari au kupanda daladala hadi kwenye jengo kubwa, zuri.

No. Siku hizi unaweza ukawa na ofisi home kwako, kikubwa unachohitaji ni laptop na internet tu! So, inawezekana jirani yako anafanya kazi remotely, kazi ambayo akiwa kwa PC anamaliza kila kitu.

Hizo unalipwa kwa $$, so you can imagine kama unaspend kwa Tshs kibongo ni rahisi kuonekana you are well off.
Au labda anafanya issues za forex trading au cryptocurrency, ambazo na zenyewe what you need ni laptop na internet ya uhakika tu!
 
Jirani yako ana mali zake alizowekeza zamani ndio zinamtunza.

Kama ni kijana ana urithi wa kutosha.

Nina jirani kama huyo. Ni dogo hajaoa bado anaishi kisela.

Hapa dar mama yake kamuachia urithi wa appartments kama 10 hivi. Ubungo, na chang'ombe.

Dogo alizaliwa peke yake na sababu alikuwa anasoma udsm akaamua aje kupanga karibu na chuo baada ya mama yake kufariki. Nyumba ya mama yake goba na appartment alizoachiwa ubungo na chang'ombe akazipangisha zote. Kwa mwezi tu average kodi anakusanya kama milioni 4.

Yeye dogo akaenda kupanga appartment kali karibu na chuo udsm.

Unaona kabisa kazi hafanyi ila anakula bata tu na kubadili magari. Huku majirani zake tunaoamka alfajiri kuwai kazini tunamuonea wivu
 
Watu ni ma External auditors
Wanamiliki firms zao zenye wafanyakazi bora.
Kuna Jamaa ni auditor aisee ana hela ile mbaya,na yupo simple sana na kazi zake huwa anafanyia kwenye mahotel anakunywa zake kahawa na cookies tu, aisee yule Mshikaji ana upepo sana na ana kiwanda chake kinachozalisha viburudisho Fulani, hilo jumba Sasa na hiyo mindinga aisee. 😊😊😊
 
Sio kwamba namchunguza, ila natamani namimi niishi life style kama yake, mana wengine tunachapika na maisha huenda kuna watu wana shortcut.

Ni miaka miwili tangu amalize nyumba yake na kuhamia,
1. Amejenga ndani ya miezi miwili au mitatu
2. Tangu ahamie, muda wote yuko ndani, mara kadhaa hutoka au husafiri na ananiaga ila hakai hata wiki anarudi.

3. Anaagiza mahitaji kwa boda au mara nyingine anatoka, (hii sio ajabu sana)

4. Kuna mdada/wadada wanakuja ila hawakai sana wanaondoka, jamaa yuko mwenyewe

5. Hana kufulia, au aje aombe kitu, mimi ndo niliwahi kwama nikamfata aniazime kiasi cha pesa.
6. Kusema ni jambazi anatoka usiku hapana, mana hata usiku yupo, na ni mpole sana hana shida na mtu.

Je anaishije?
Akikwambia kazi anayoifanya utaiweza mkuu!?...

Ishi maisha yako!... Haya maisha Yana siri nyingi!

Pengine yuko mahala ambapo walioko huko wanatamani kutoka!... Lakini hawawezi kutoka!... Walio nje ya huo mfumo wanatamani waingie... Lakini hawajui waanzie wapi!

Pengine usikute na yeye anaitamani furaha uliyonayo! Kuishi akiwa huru... Lakini hawezi kuipata!

Maisha Yana mambo mengi!... Hayako kama unavyoyaona!...

The more you look... The less you see!
 
Sio kwamba namchunguza, ila natamani namimi niishi life style kama yake, mana wengine tunachapika na maisha huenda kuna watu wana shortcut.

Ni miaka miwili tangu amalize nyumba yake na kuhamia,
1. Amejenga ndani ya miezi miwili au mitatu
2. Tangu ahamie, muda wote yuko ndani, mara kadhaa hutoka au husafiri na ananiaga ila hakai hata wiki anarudi.

3. Anaagiza mahitaji kwa boda au mara nyingine anatoka, (hii sio ajabu sana)

4. Kuna mdada/wadada wanakuja ila hawakai sana wanaondoka, jamaa yuko mwenyewe

5. Hana kufulia, au aje aombe kitu, mimi ndo niliwahi kwama nikamfata aniazime kiasi cha pesa.
6. Kusema ni jambazi anatoka usiku hapana, mana hata usiku yupo, na ni mpole sana hana shida na mtu.

Je anaishije?
Unamchunguza mtu. Muulize tu.

Hapa utapata majibu mengi ya kukisia.

Watu wengine hawafanyi kazi ili wapate pesa, pesa zinawafanyia kazi wao.

Kuna watu wanafanya kazi mitandaoni siku hizi.

Kuna watu wana mali za urithi.
 
Back
Top Bottom