relis
JF-Expert Member
- May 24, 2015
- 3,429
- 5,469
Kinachokupa shida ni kushindwa kutofautisha sabwoofer na hometheatre,hiyo uliyochukua ni subwoofer iliyowekwa sifa za home theatre kelele tu lkn theatre sterio take sio kelele kwa majirani na hata unapoifungulia mpaka mwisho ni watu kufurahia haina kelele za kutingisha paa la nyumba,ungaunga tafuta Sony utakuja kutuletea mrejesho jinsi mjumbe na majirani walivyoongeza upendo kwako,na majaribio kadhaa ya kuvunjiwa kimlango chako waunyakue mziki.Nimefanikiwa kupata kitu BOSE....aisee asikwambie mtu kitu. Hii kitu inagonga. Ni juzi juzi tu nlikuwa na kikao kwa mjumbe. Mtaani wameenda kulalamika kuwa nina ponda nyumba zao na kitu kizito wanashindwa kulala maana bati zao zinapiga kelele na kuta kutikisika. Nmemkatalia kabisa mjumbe hajaamini anahisi kuna vitu nafanya home illegal basi imebidi nimlete home akakagua akaenda kuwapa ujumbe kuwa hamna kitu.
Jumamosi mi najilia music wangu sina hili wala lile kaja mjumbe na wazee wawili wakagonga geti nkaenda kuwafungulia. Moja kwa moja wakaongoza ndani. Kufika wanaaanza kukagua kumbe wale wazee wameenda tena kumwambia mjumbe nagonga. Ndo wakagundua ni mziki.aiseee walishangaa sana. Wamesambaza habri mtaani kuwa napiga disco.sasa imekuwa shida nikipita nanyooshewa vidole. Mabint wanataka waje kusikilizia nyimbo zao kwangu... Matozi nao imekuwa shida na flash zao kila wakati wanataka waje wajaribu nyimbo zao kwangu.
BOSE ni balaah asikwambie mtu.inatisha hasa...hata hivyo nililetea zawadi na bro toka kwa mzee obama. Huu muziki ukifungua kwa saut kubwa unaweza sababisha tetemeko la ardhi kabisa. Cha ajabu wewe ukiwa ndani husikii sana. Hapo nashindwa kuelewa inakuaje