Ushauri: Najuta kuingia kwenye mahusiano

Ushauri: Najuta kuingia kwenye mahusiano

Habarin za jioni wana MMU.

Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 24,nina kazi ambayo inaniingizia kipato changu kinachonikimu ktk maisha nipo kwenye mahusiano na binti mmoja kwa takribani mwaka mmoja sasa, ambaye pia ana kipato chake kizuri tu,tumekuwa tukisaidiana katika shida na raha, wiki moja iliyopita huyu binti, aliniambia kuwa amepatwa na shida ambayo inagharimu kiasi cha shiling laki nne na akaniahidi atanirudishia mwezi wa kwanza, hivo akaomba nimuazime.

Huyu binti namshirikisha kwenye mambo mengi sana, ikumbukwe nilishawahi kumshirikisha malengo yangu,na pia nikamjulisha kiaisi ambacho kinahitajika ili hayo malengo yaweze kutimia na pia isitoshe nikawa nmemjulisha kiasi ambacho nimefanikiwa kukikusanya na kukihifadhi katika account yangu ya akiba.Maana nlipanga kufikia 2016 mwezi wa 7 niweze kuanza kutekeleza hayo malengo yangu,vyote hvo nilimshirikisha.

Hivo alivyonifuata kuomba nimuazime hyo hela alijua kabisa siwezi kumnyima kiukweli kutoka moyoni sikupanga kabisa kuigusa hyo hela maana nafahamu madhara yake,nlikuwa nathubutu hata kujinyima mwenyewe kipindi nmekosa hela, niko tayari nitafute hela sehemu nyingine ili mrad tu saving account yang ibaki salama.

Baada ya yeye kuniahidi kuwa hyo hela itarudi mwezi wa kwanza kama ilivyo nkawa nmeamua kumkabidhi hyo laki nne.Juzi kati tar 20 siku ya ijumaa ya mwezi huu tukiwa tunachat akaniambia kuwa anashukuru kwa kumkabidhi hiyo pesa, mimi nkamuambia asijali ila nkamuomba anirudishie hyo pesa mwanzoni mwa huo mwezi wa kwanza.Hapo ndo ugomvi ulipoanzia, akaniambia kuwa mimi sina utu wala ubinadamu na nina roho ya kinyama,maana haiwezekani nimuazimishe pesa hata wiki mbili hazijapita naanza kumdai hivi wadau iko sawa kweli hii? Akawa amekasirika sana, siku ya jana usiku akanipigia tena akaongea tena maneno yaleyale kwa hasira sana, akasema kuwa amemuomba mtu amuazime hela ili anirudishie na hatothubutu tena kuniomba ama kuazma chochote kutoka kwangu.

Nimejaribu kumuomba sana na kumsihi kuwa mimi sikumaanisha anipe saivi ila nichosema ni kwamba anipe mwanzoni mwa huo mwezi wa kwanza.anasema kuwa lazima anirudishie ndani ya wiki hii maana mtu aliye muomba hawezi kumzuia asitume kwa madai ya kuwa anaogopa siku atakapo muomba tena ataonekana anamtania nipo njia kuu wadau yaani sijui nifanyaje,je nmemkosea nini? Maana tangu hiyo jana usiku hatujaongea wala hajanitafuta mpaka saivi simu hapokei, najiuliza je,ana mpango gani na mimi? Mbona ananifanyia vitimbwi vya ajabu hvi? Pia nafikia mahali najuta kumshirikisha huyu mtu mambo yangu,wenda asingefahamu nina kias gani cha pesa pia najiuliza kwa hayo yanayotokea nini hatima yake?

Samahani kwa thread ndefu wadau ila nna huzuni sana, maana sijui hatima ya huu uhusiano na pia sijui hatima ya pesa yangu maana simu hapokei, naomba mnishauri ndugu zangu, maana naiona dunia chungu.

Natanguliza shukurani kwenu nyote


hawa wafuatao watakusaidia tatizo lako mkuu:
NIDHAMU KTK PESA
UVUMILIVU
NA BIDII KTK KAZI. Wasilikize sana watakusaidia...

hivyo yani, nikupe siri za wanawake wanavyotupima:
wanawake hutupima katika mambo yafuatayo:
PESA-Anataka kujua wewe ni mtoaji au bahili? Maana wanawake hawapendi wabahili, hiyo hukumkopesha ulipaswa kumpa ndiyo matarajio yake
MIMBA-Mwanamke anaweza kukusingizia mimba ili ajue msimamo wake, ukikataa anakujua kuwa huna future naye
CARE-Atakuambia ndugu yake anaumwa ajue unawajali ?

Sasa kwa kile ulichokifanya, akitokea mtu anayejitoa kwake kwa hali na mali, Kamwone dokta akupe Panadol......And for your information mwanamke ukimboa, kama kuna mtu anamsumbua ndiyo palepale on spot anampata na anamgonga..........I am talking with experience, Tena atakuchafua mpaka Basi...

Ushauri: Usimdai, Usimpigie Simu, Endelea na Maisha yako, kama anakupenda atakuja mwenyewe
 
Pole kaka kuwa mpole ili upate hela yako.
ukiwa mkali yy utamkosa pia na hela yako utaikosa
 
Kachukue pesa yako halafu umwache aendelee na wengine wanaotoa pesa za mkopo na kuzifanya za bure. Kama alitaka kuomba pesa angeomba bila kuomba mkopo.

Ila dunia ya siku hizi na pesa mhhhhhh.....wenzio enzi zetu za 1947 hatukuwahi kusikia wapenzi wanakopeshana au kusumbuliwa na mambo fweza!
 
Kitu mkipeana kwa deadline inakubidi kuwa na subira. Aliona unamfedhehesha.

Ongea naye.
 
Huyo kakuzidi kete ina wezekana wewe hujui yeye ana akiba ya sh. Ngp na hujui malengo yake ni yapi na inawezekana kapiga hesabu anakudai laki 4 kama malimbikizo ya huduma ya papuchi
piga moyo konde songa mbele akirudisha poa na asipo rudisha nisawa vile vile
 
Komaa arudishe pesa kwanza hayo mengine yatajiset baadae

Ukingagania bila kuangalia hali yake kifedha kama wakati huo anauwezo au la, kuna hatari ya wewe kupewa pesa iliotoka kwa mwanaume mwenzio ambae hana mkono wa birika.
 
Una miaka 24 inaonekana mpenzi wako anamiaka 20-23 kwa umri huo wasichana wengi hujiona bado wanalipa huyo anatafuta sababu tu,
kama amesema anakuletea pesa yako pokea halafu piga kimya
 
Hela ya Malengo ni kama uchi wa mtoto... ukiigusa tu ni miaka 30 jela. Sas we pambana upewe hela yako alafu... Alafu next tym ukimkopesha mtu dont be obssessed kumkumbusha siku ya kukulipa maaana si alikuahidi tayari honestly inakera in most cases maaana watu wengine wana mambo Yaki K. Kinyama kama huyo demu wako
 
Kosa kubwa ni kutoa siri zako za kipato kwa rafiki wa kike ukidhani umepata mke tayari.... Usipokuwa makini na kuonyesha mapenzi ya kitamthilia hilo salio lililobaki benki lipo hatiani maana kama umekutana na kundi la kifo lenye aina fulani ya wasichana lazima ukae.... Pia ulifanya kosa kuhoji marejesho leo wakati january bado iko mbali sana japo wakati mwingine imekurahisishia kujua una rafiki namna gani. Mwisho punguza munkari za kufanya malengo yako kwa kumshirikisha mungu ili imani ikupe amani zaidi maana unaweza fanikiwa yote lakini ukajikuta peke yako na pengine una vidonda vya tumbo kwa sababu ya ugumu.
 
Amekasirika unamkumbusha kumbusha kila saa utadhani hatakulipa, hata hivyo kama una malengo nae kaka kwanini laki 4 ikutoe roho? Hukuwa na haja kumkumbusha kumbusha hata wiki bado, hata angekudhulumu si ni wako bwana, kama umeweza kumpa moyo wako na mwili wako akaufanya atakacho laki 4 kitu gani bwana.

Umemkosea sana kumfanya kama hatakulipa!
 
Sasa haujui nn?uhusiano umekwisha,ilikuwa sababuu.
 
ulimuonesha sura ya udhaifu mapema na itakula kwako.....
 
umeonesha udhaifu sana kwa kumiminika kwake na ana take advantage....usiwe too good auusitake kuonekana good kwa huyo mdada
 
Hehehe! Pole kijana ndo ukubwa huoo!! We tuliaa ka anakupenda atakirudishaa,na akikupa pesa zako chukuaaa akigomaa sameheee tafuta zingine.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom