Ushauri: Najuta kuingia kwenye mahusiano

Ushauri: Najuta kuingia kwenye mahusiano

"...hata mkeo alalaye kifuani kwako usimuambie siri."
 
ila na nyie kina dada muwe mnarudisha vijihela vyetu.
 
Mw?vuliana nguo kila siku afu mwakopeshana pesa, hii ingia akilin kweli???
 
Mw?vuliana nguo kila siku afu mwakopeshana pesa, hii inaingia akilini kweli????
 
Kama una akiri chukua hela yako teba leo. Hivi mpenzi anakopeshwa???
 
hivi laki nne nayo ni pesa ya kumkopesha mtu afu umkumbushie mara nyingi nyingi?

Wewe unaendana na yule mama(Pro) aliyesema 10 mil ni pesa ya mboga. Unafikiri watanzania wote wana kipato cha juu kama wewe ? Wengine hiyo laki nne ndo makusanyo ya mwaka kwa hiyo acha kauli za kejeli.
 
komaa akurudishie.....mwanamke haambiwi mipango endelevu.....anaambiwa ile mifupi mifupi tuuu....
 
Habarin za jioni wana MMU.

Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 24,nina kazi ambayo inaniingizia kipato changu kinachonikimu ktk maisha nipo kwenye mahusiano na binti mmoja kwa takribani mwaka mmoja sasa, ambaye pia ana kipato chake kizuri tu,tumekuwa tukisaidiana katika shida na raha, wiki moja iliyopita huyu binti, aliniambia kuwa amepatwa na shida ambayo inagharimu kiasi cha shiling laki nne na akaniahidi atanirudishia mwezi wa kwanza, hivo akaomba nimuazime.

Huyu binti namshirikisha kwenye mambo mengi sana, ikumbukwe nilishawahi kumshirikisha malengo yangu,na pia nikamjulisha kiaisi ambacho kinahitajika ili hayo malengo yaweze kutimia na pia isitoshe nikawa nmemjulisha kiasi ambacho nimefanikiwa kukikusanya na kukihifadhi katika account yangu ya akiba.Maana nlipanga kufikia 2016 mwezi wa 7 niweze kuanza kutekeleza hayo malengo yangu,vyote hvo nilimshirikisha.

Hivo alivyonifuata kuomba nimuazime hyo hela alijua kabisa siwezi kumnyima kiukweli kutoka moyoni sikupanga kabisa kuigusa hyo hela maana nafahamu madhara yake,nlikuwa nathubutu hata kujinyima mwenyewe kipindi nmekosa hela, niko tayari nitafute hela sehemu nyingine ili mrad tu saving account yang ibaki salama.

Baada ya yeye kuniahidi kuwa hyo hela itarudi mwezi wa kwanza kama ilivyo nkawa nmeamua kumkabidhi hyo laki nne.Juzi kati tar 20 siku ya ijumaa ya mwezi huu tukiwa tunachat akaniambia kuwa anashukuru kwa kumkabidhi hiyo pesa, mimi nkamuambia asijali ila nkamuomba anirudishie hyo pesa mwanzoni mwa huo mwezi wa kwanza.Hapo ndo ugomvi ulipoanzia, akaniambia kuwa mimi sina utu wala ubinadamu na nina roho ya kinyama,maana haiwezekani nimuazimishe pesa hata wiki mbili hazijapita naanza kumdai hivi wadau iko sawa kweli hii? Akawa amekasirika sana, siku ya jana usiku akanipigia tena akaongea tena maneno yaleyale kwa hasira sana, akasema kuwa amemuomba mtu amuazime hela ili anirudishie na hatothubutu tena kuniomba ama kuazma chochote kutoka kwangu.

Nimejaribu kumuomba sana na kumsihi kuwa mimi sikumaanisha anipe saivi ila nichosema ni kwamba anipe mwanzoni mwa huo mwezi wa kwanza.anasema kuwa lazima anirudishie ndani ya wiki hii maana mtu aliye muomba hawezi kumzuia asitume kwa madai ya kuwa anaogopa siku atakapo muomba tena ataonekana anamtania nipo njia kuu wadau yaani sijui nifanyaje,je nmemkosea nini? Maana tangu hiyo jana usiku hatujaongea wala hajanitafuta mpaka saivi simu hapokei, najiuliza je,ana mpango gani na mimi? Mbona ananifanyia vitimbwi vya ajabu hvi? Pia nafikia mahali najuta kumshirikisha huyu mtu mambo yangu,wenda asingefahamu nina kias gani cha pesa pia najiuliza kwa hayo yanayotokea nini hatima yake?

Samahani kwa thread ndefu wadau ila nna huzuni sana, maana sijui hatima ya huu uhusiano na pia sijui hatima ya pesa yangu maana simu hapokei, naomba mnishauri ndugu zangu, maana naiona dunia chungu.

Natanguliza shukurani kwenu nyote

Pliz take ur money back whetever it is pesa inauma ndugu asa na malengo yako hayo uliojiwekea kupitia saving

NB TAKE UR MONEY.BACK NASISITIZA HILO

Kama anakupenda basi ni baada ya kurudisha pesa zako ndo mambo mengine yatafuata

Sio kila jambo ni la kumwambia mwanamke hasa siri na malengo ya mafanikio unashindwaje kukumbuka kilichompata samsoni kwa delila daah hawa viumbe ni hawaeleweki ndo wapo ivo by nature

Wakitembea kama wanarud nyuma wakirud nyuma kama wanaenda mbele basi shagabaghala tu

Take ur money back and dont prove weakeness on it coz of love
 
Wanaume wakweli ndio hulizwa.
A woman is always treated like a kid. Promises, hopes, ndio maisha ya uchumba au mapenzi.
Ukweli upo lakini si kwa 100% , next time usifanye hovyo, hiyo hela hesabu umeliwa.!!
Mapenzi siku hizi mpaka account ioneshe inasoma, wallet imetuna, ndo utaitwa baby na majina mengine mazuri.
Jiulize kwa nini alikasirika?
Mwanamke hakopeshwi pesa bali hupewa!
Akiomba anatumia neno "nikopeshe" lakini humaanisha "naomba".
Read between the lines!
 
daah,nmeumia sana dada evelyn salt..yaan hapa nacho wazia ni nn hatma ya huu uhusiano.angalau hata pesa,siiwazii sana

Acha ujinga, chukua hela, kwanza nikuuze amekwambia malengo ya pesa? kwa nini hakuwa muwazi kwako, hata kama una uhusiano mwaka mmoja, it's doesn't means that she's yours, wanawake watu ajabu sana.

Usishangae mkuu akawa ana sharo wake mwengine kamuhadaa amuazime pesa, kachukua kwao kapeleka kwa mwengine, haya ndio wanayo fanya wanawake, sio wote lakini wanawake sio wa kuamini 100% akili zao za kuongozwa. Hata Mungu ametueleza hilo mwanamme ndio kiongozi wa mwanamke kwa sababu wako weak.

Ndugu yangu, wake up, tengeneza maisha yako, kwa family yako unayo tarajia huyo mwanamke hujaowa wakati wowote anaweza kuvunja Mawasiliano, so what will you benefit? So.lost your time and money, imagine hizo pesa umechukua muda gani ku save? Then unasema pesa hujali unajali penzi? What fu....!
Wake up brother.

Mpenzi wa kweli ni yule mwenye open mind, asie kuwa na siri, something going on to her, nakuambia.
 
Kweli apo umebugi man,najua kabisa mtu haswa mpenz wako ukifanya ajue kuwa humuamini na unathamini sana pesa kuliko yye,af ata mda hujapita, apo huyo dem wako ana haki ya kuvimba
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom