Ushauri: Mke kamalizia kulipa gharama ya kiwanja ambacho mume wake alikuwa anamnunulia mchepuko

Dah! Mwenyekiti hili ni bomu kabisa. Lakini hakijaharibika kitu maana sidhani kama huyo mzee anajua kua kiwanja ni cha mchepuko. Hapo kuruka kiunzi jamaa avunge aende akasaini makaratasi lakini kwa jina la mtoto wake, iwe kama kamnunulia mtoto.

Alaf apeleke document nyumbani. Wife lazma atauliza, hapo ndipo msela amwambie alikutana na kiwanja kama zali akaona anunue. Pia ajitetee kuwa hakusema kwa sabab aliona kuna mambo mengi waliopanga kufanya kama familia so this was unnecessary cost ya ghafla so akaona aishi nayo kibingwa.

Kwa wewe mwenyekiti inabidi uvunge tu mpaka shemeji aje mwenyewe, akija na siasa kwamba kiwanja ni cha mchepukk, ruka futi mia. Useme tu kua umeambiwa u co sign kama shahidi lakini huez kuhoji maana hayo ni mambo ya familia.

Mwisho wa siku kama huyo mams alihack sim ya jamaa so anajua kila kitu, everything nilichoandika ni wastage of battery life. Kimeumana nje ndani!

Mwanaume hakosei, anaghafilika!
 
Kuna wanaume wapumbavu sana hapa duniani.

Si ajabu mdogo wake au shangazi yake kule kijijini kamuomba laki Tano ya mtaji tena kwa mkopo lakini man kachomoa kasema hana pesa na maneno ya kejeli mengi.

Mpumbavu huyo mwache achapiwe.

Usione huyo binti kakaa kimya ni kwamba ameamua kugawa uroda bure.

Na mke wako huenda kataarifiwa kila kitu na sasa wanalipiza kisasi
 
Hizi mada za michepuko zimekua nyingi mno.

Hii ni kwa sababu ndio jambo ambalo jamii kwa sasa inalifanya kwa kiasi kikubwa.

Nimezaliwa na kukulia kijiji moshi huko, niliwahi kushuhudia wazee kama wanne hivi wakiwa na wake wawili, kama ijulikanayo kule dini ya ukristo wa katoliki imeshamiri sana, wale wazee walikua wametengwa na kanisa kwa sababu hiyo.

Pamoja na kutengwa lakini walikua wamejenga nyumba kwa kila mwanamke na kwa kiasi chake wale wakina mama walikua wanaupendano.

Ni miaka mingi kidogo tokea nitoke huko lakini mpaka leo hii wale wazee wapo na wake zao wapo na hapo wako around miaka 80 mpaka 90 ila mmoja alishafatiki.

Kwetu kama jamii ya leo inaonekana ni kubwa na mke mwingine ni dhambi isio ya kawaida, hali hao wanawake walio olewa wa kwanza hawatimizi majukumu yao kwa ukamilifu.

Binafsi babu yangu alizaliwa kwa mke wa 3. So siku nikiona kuna ulazima wa kua na mke mwingine sita kua na mjadala na mtu maadam tu natimiza wajibu wangu kama baba.
 
Hahahahah ya leo kali!

Ina maana shemeji yako alishasanukia mchongo ila kaamua akamalize show kibingwa. Sasa hapo mtachagua kusuka au kunyoa maana hamna jinsi zaidi ya kupiga kimya ni kumfata mwenye kiwanja na kumchana live tu kuwa show ishakuwa kali.

Wife kalipia kiwanja cha mchepuko so wa assume tu kuwa hakuna kilichotokea wampe documaa shemeji yako. Ila kimsingi wote mshaonekana mafala tu.😅 Kaukeni hapo haina bobo!

Mwambie jamaa yako awe makini na simu yake na awe mtu wa kufuta meseji kila wakati. 100% meseji ndio zimemponza...Mie baada ya kugundua sms zinanichomaga mara nyingi nimetia pini whatsapp. Mama akishika simu anaombaga aangalie picha kisha anapekua pekua call logs na whatsapp.
🤣 🤣 🤣 🤣
 
Wakuu

MDA SI mrefu nmetoka kupigiwa Simu na rafiki yangu mmoja wa karibu Sana Ni DOKTA hospital moja ya wahindi hapa mjini,Na anamiliki duka moja la dawa za binadamu kubwa Kiasi ambalo suka ilo mkewe ndo muuzaji na msimamizi mkuu wa kila mara.
Sasa Jamaa kapigia akinipa taarifa nzito sana khs jambo moja.

Ni kwamba
kile kiwanja nilichosaini Kama shahidi wake kwa ajili ya manunuzi na kumjengea mchepuko wake nyumba tayar kaenda MKE wake na mil 2 cash pesa ilobaki ili kukimalizia kabisa.

Ni Hivi wakuu,
Katika harakati za hapa na pale, jamaa yangu uyu nilimshaur Bora amjengee TU mchepuko wake maana Kodi anakokaa anayomlipia kubwa Sana na inamuumiza (double ya nnayomlipia mchepuko wangu mimi).Jamaa kweli akakubali.

Kiwanja kimetafutwa kimepatikana na maafikiano yamefikiwa kilipiwe pesa mil. 8 cash ila iwe ni kwa installment 3 ndani ya miez 3 tu.
Yaani January tulipoenda wote kililipiwa mil 3 cash- Tukasainishana awamu ya kwanza tukaondoka.

February, - Jamaa akamuingizia TU mzee Ela mil.3 kwenye bank. Akanipa taarifa tu ila Hatukwenda kule saiti kusaini. Mzee akasema tutakuja kusainishana mwishoni kabisa tukimaliza biashara.

Jana anasema kapigiwa na mzee mwenye kiwanja kwamba mkataba uko tayar Mbona haji wakakabidhiane na viongozi wa serikali. Kila Siku anapiga kalenda.

Jamaa akajitetea mzee amvumilie kwanza mpk amalizane na TRA tar 30 March kwenye maswala ya Kodi ya mapato. Mzee akamjibu kwamba mbona ela iliyobaki tayar ishalipwa, ililetwa na mama (yaani mkewe).

Mzee Anasema Kuna mmama alimpigia akijitambulisha kwamba mme wake DOKTA flani kampa maelekezo pesa ilobaki mil.2 cash aje aimalizie, sasa wakutane wapi akabidhiwe?

Mzee kamjibu kwamba wakutane saiti maana Hakua mbali na pale. Akasema mama mwnyw alikuja na gari yake ile ile jamaa aliyokuja nayo siku ya mwanzo pale saiti kwake Akiwa Yuko na mtoto mdogo na binti mmoja kafunga nywele kwa juu kuja kumalizia Ela.

Na kuondoka zake kwamba mkataba watakuja jumapili ijayo.Jumapili imefika hawajaja Ndo ikabd ampigie jamaa. Sasa Jamaa akasema kwa maelezo yake akahisi labda mzee yule anamjaribu. Ila Kama ni gari Huenda iwe imetumika wikendi TU maana ndo humuachia mkewe apeleke Watoto wake kanisani, yeye ubaki nyumbani kupumzika.

Sasa Leo jion kaenda kumhoji binti wa kazi kama Kuna sehem yoyote alienda na mama ake, binti kweli kakiri Kuna mahali jumapili moja walienda na mama ake baada ya kutoka misa nje ya mji kidg.

Ila yeye alibaki kwenye gari mama akaenda kuongea na wazee flani, baadae mzee mmoja akawa anamsindikiza mpk kwny Gari wakasalimiana ila yeye akujua walienda kufanya Nini kule Maana mama akumwambia kilichompeleka mpk wanarudi.

Sasa Jamaa kachanganyikiwa apa kaniomba ushaur afanyeje kulimaliza hili.Nmemwambia nipe muda nitafakari Kwanza tunafanyaje.

Kiukweli
Mimi mwnyw hata Cha kumshaur sahii Ni kipi nmekosa.

Maana Kama kweli yule MAMA alijua nilikua shahidi tayar nishajijengea chuki kwamba nmehusika kwenye dhambi ya mmewe. Mimi na mmewe Ni wale wale.

Afu kibaya zaidi Mimi Ndo huwa msuluhishi wao kila Mara pale wanapogombana, shemej huja kushtakia kwangu Nawasuluhisha.

Sasa kwahili nashangaa shemej yangu hajaja kunambia chochote.

Yaan Shemej yangu uyu huwa ananiamini Sana kias kwamba ata jamaa akienda kwenye Mambo yake akimwambia TU kua Yuko namimi, mkewe anakua na amani KABISA mmewe Yuko sehem salama.

Kwenye ugomvi shemej anamshaur kila mara kufuata nyayo zangu jins nilivotulia na familia yangu bila mambo mengi ya michepuko michepuko.

Sasa
Nishaurini vema niweze kumshaur vizur uyu jamaa yangu ili kuokoa ndoa yake.

Pili nishaurini namuingia vipi uyu shemej yang Kama kweli akija kujua nmehusika kwny kile kiwanja kwenye dhambi ya mmewe. Napangua vipi mapigo.

NAWASILISHA

Ni nahisi huo ni mchepuko wa jamaa/na wewe unakula kwa pembeni.
 
Hahahahah ya leo kali!

Ina maana shemeji yako alishasanukia mchongo ila kaamua akamalize show kibingwa. Sasa hapo mtachagua kusuka au kunyoa maana hamna jinsi zaidi ya kupiga kimya ni kumfata mwenye kiwanja na kumchana live tu kuwa show ishakuwa kali.

Wife kalipia kiwanja cha mchepuko so wa assume tu kuwa hakuna kilichotokea wampe documaa shemeji yako. Ila kimsingi wote mshaonekana mafala tu. Kaukeni hapo haina bobo!

Mwambie jamaa yako awe makini na simu yake na awe mtu wa kufuta meseji kila wakati. 100% meseji ndio zimemponza...Mie baada ya kugundua sms zinanichomaga mara nyingi nimetia pini whatsapp. Mama akishika simu anaombaga aangalie picha kisha anapekua pekua call logs na whatsapp.
Jamaa sidhan km Ni sms au WhatsApp.
Kuna mtu kachoma picha Zima Maana HAIWEZEKANI ile namba ya mzee wa kiwanja kaipata wapi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom