USHAURI: Mdogo Wangu Amechagupangiwa Kibiti Sec. Combination Ya PCB

bampami

JF-Expert Member
Nov 5, 2011
5,697
4,107
Kama kichwa kielezavyo, mdogo wangu amepangiwa kibiti combination ya PCB, Kwenye familia kumekuwa na ubishani mkubwa wengi wao wakipinga aisende huko kutokana na hali ya usalama, sisi wachache tumeonelea yeye kwenda kwani serikali inajitahidi kuweka usalama katika hali yake ya zamani...

Wapendwa Tumefikiria sana tumefika mwisho au ukomo wa kufikiria, Kwa Niaba ya familia naomba maoni yenu, najua tupo wengi wenye mawazo toauti zaidi ya haya yetu, dogo mwenyewe ndo tunamtegemea na tunaarajia ndiye atakayetutibu huko mbeleni tukiwa wazee kwa NEEMA YA MUNGU, Naombeni mawazo yenu..

Natanguliza shukrani!
bampami!
 
Mkuu, kibiti ni kubwa sana.. Yani ukienda kibit wananch wanafanya mambo yao kwa aman mpaka utashangaa.. Then hyo shule ipo mbali na mji wa kibiti lakn mita 50 kutoka highway ya dar-mtwara.. Mpeleken akasome, kuna aman tele na shule haiko porini.
 
Nilisoma hapo miaka iliyopita,mchepuo huo huo wa PCB,na mwaka huu nilienda kutembea kwa sababu Nina ndugu zangu wanaishi pale kibiti mjini,hakuna tatizo watu wanafanya shughuli zao kama kawaida za kiuchumi.pia IGP alipoenda kuongea na wazee ule mkutano alifanya kwenye shule hiyo hiyo ya kibiti.lile eneo ni salama,pia kibiti ni mji mkubwa,hata hayo matukio yanayotokea wanaamua kusema kuwa yanatokea kibiti kwa sababu kibiti ndo mji maarufu.lakini kibiti kama kibiti yenyewe hakuna tukio lilotokea la mauaji.hivyo mwacheni dogo akapige msuli.
 
Hakuna shida kwa wanafunzi mimi kila siku naenda kuchukua mihogo wanafunzi wana endelea na masomo bila shida
Kibiti ni kubwa pia,kibiti yenyewe kuna amani tupu.hayo matukio yanatokea,ikwiriri,bungu,jaribu,mkuranga,pagae ambapo juzi polisi iliua wahalifu wanne.hata hivyo vimji vinavyotokea hayo matukio watu wanafanya shughuli zao kama kawaida.Upo sahihi mkuu
 
Kama kichwa kielezavyo, mdogo wangu amepangiwa kibiti combination ya PCB, Kwenye familia kumekuwa na ubishani mkubwa wengi wao wakipinga aisende huko kutokana na hali ya usalama, sisi wachache tumeonelea yeye kwenda kwani serikali inajitahidi kuweka usalama katika hali yake ya zamani...

Wapendwa Tumefikiria sana tumefika mwisho au ukomo wa kufikiria, Kwa Niaba ya familia naomba maoni yenu, najua tupo wengi wenye mawazo toauti zaidi ya haya yetu, dogo mwenyewe ndo tunamtegemea na tunaarajia ndiye atakayetutibu huko mbeleni tukiwa wazee kwa NEEMA YA MUNGU, Naombeni mawazo yenu..

Natanguliza shukrani!
bampami!
Ivi kobiti na wanafunzi wanauwawa? Acheni zenu bana muacheni kijana aende shule, au kama hamuhitaji mpelekeni private school tu
 
Hivi wee jamaa una habari kama huko Syria kuna shule zinafanya kaz kama kawaida pamoja na kuwa huko kwao bomb ni kama pensel...
 
Back
Top Bottom