Ushauri, Maoni na Msaada: Kwa wanaotaka kujilipua nje ya nchi kusaka maisha, kusoma na kuwekeza

Polisi wa South Africa wamethibitisha kuwakamata Washukiwa sita wa mauaji ya Rapper Kiernan Forbes maarufu AKA na kusema miongoni mwao ni ‘Mastermind’ aliyeandaa mpango mzima na kulipa wote Wauaji wote walioshiriki tukio hilo la February 10 2023.

Waziri anayehusika na Idara ya Polisi Bheki Cele amesema Watu hao sita watafikishwa Mahakamani Alhamisi hii February 29 ambapo mwenye umri mkubwa kati yao ana miaka 36, wa kwanza ni huyo Muandaaji Mkuu ‘Mastermind’, Watumia bunduki wawili, watoa taarifa wawili na mmoja wa mwisho ni aliyehusika kutafuta silaha na magari.

Waziri Cele amesema miongoni mwa waliokamatwa wamewahi kuhusishwa na mauaji ya kutisha ambapo walikimbilia Nchi jirani ya Eswatini ( zamani Swaziland) kujificha lakini tayari wamekamatwa na taratibu za kuwarejesha South Africa zilishaanza kufanyiwa kazi.

Pamoja na kwamba Polisi wamesema hawatozungumzia nia ya mauaji hayo, imefahamika kwamba Wauaji walianza kumfuatilia AKA kuanzia anawasili uwanja wa Ndege wa Durban hadi kwenye Mgahawa alikouawa.

South Africa ni moja ya Nchi zinazotajwa kuwa na mauaji mengi ya risasi yanayohusu visa vya kimaisha na wizi ambapo AKA sio Staa wa kwanza kuuawa kwa risasi kwani mwaka 2007 Staa wa muziki wa reggae Lucky Dube aliuawa kwa kupigwa risasi tatu na Majambazi baada ya kushindikana kwa jaribio la kumuibia gari lake ( Chrysler 300c) wakati akishusha Watoto wake kwa Ndugu.

Unaambiwa kwa mujibu wa rekodi zilizotolewa na Polisi mwezi uliopita, Taifa hilo lenye Mafundi wa amapiano lilirekodi vifo karibu 84 kila siku kuanzia October hadi December 2023. #MillardAyoUPDATES
FB_IMG_1709137295688.jpg
 
Ndugu zangu jaribuni watu wanaenda sana huko Uarabuni. Maisha yakikushinda bongo tafuta kwengine. Wenzetu wanaigeria na wakenya wametupiga hatua sana.

Nchi zao zinafaidika sana na vijana wao wanaofanya kazi nje ya nchi.

Kipindi cha nyuma kuna mdau humu alikuwa anataka mawasiliano na agents wa kazi nje ya nchi na mimi nilimpatia ninao wajua.

Bahati nzuri alipata kazi Qatar na sasa hv yupo huko nje ya nchi. So msikate tamaa pambaneni.
Ajira nje ya nchi.JPG
 
Ndugu zangu wana JF namshukuru Mungu sana kwa uhai.nilianza harakati za kutafuta nafasi ya masomo nje hasa nchi ya Canada.na Uzi huu ulinipa hamasa mno nimepitia changamoto nyingi mpaka kuja kufanikiwa.Nimejifunza penye nia pana njia nimepata VISA ya Canada naweza kuondoka muda wowote kuanzia sasa.Mliotupa hamasa nawashukuru na alieanzisha uzi pia maana nilijifunza mengi sana.Lengo nakwenda kusoma na kutafuta fursa za kimataifa.Asante
Asante kwa mrejesho, na wewe ukumbuke kusaidia wengine kupitia mkono wako.
 
Ndugu zangu wana JF namshukuru Mungu sana kwa uhai.nilianza harakati za kutafuta nafasi ya masomo nje hasa nchi ya Canada.na Uzi huu ulinipa hamasa mno nimepitia changamoto nyingi mpaka kuja kufanikiwa.Nimejifunza penye nia pana njia nimepata VISA ya Canada naweza kuondoka muda wowote kuanzia sasa.Mliotupa hamasa nawashukuru na alieanzisha uzi pia maana nilijifunza mengi sana.Lengo nakwenda kusoma na kutafuta fursa za kimataifa.Asante
kuomba ufadhili mnatumia njia gani na ni kitu gani cha msingi uwenacho wakati unaomba ufadhili
 
Ndugu zangu wana JF namshukuru Mungu sana kwa uhai.nilianza harakati za kutafuta nafasi ya masomo nje hasa nchi ya Canada.na Uzi huu ulinipa hamasa mno nimepitia changamoto nyingi mpaka kuja kufanikiwa.Nimejifunza penye nia pana njia nimepata VISA ya Canada naweza kuondoka muda wowote kuanzia sasa.Mliotupa hamasa nawashukuru na alieanzisha uzi pia maana nilijifunza mengi sana.Lengo nakwenda kusoma na kutafuta fursa za kimataifa.Asante

Hongera sana mkuu, vipi imekuchukua muda gani kupata visa yake, maana nimeambiwa za canada zinachelewa kweli
 
Mkuu hii ni thread maalumu kwa kupeana uzoefu wa majuu na namna ya kwenda. Ni maalumu kwa wenzetu wanaohitaji kwenda huko. Sio mimi ninayehitaji nimeweka kwa niaba ya wengine. Nimeshaishi USA for 8 years na Denmark.

So ili kupunguza wimbi la thread za ushauri ni vizuri tutiririke hapa ili wengine wajifunze.
Mkuu vipi kuhusu maisha ya UturukI, kuhusu uchumi wake, fursa na changamoto
 
Mimi sijaomba ufadhiri ila nilikopa hela ya kuonyesha obalozini.na kama unaweza kutumia njia ya kusoma kuna kampuni wanaijer na wahindi wanaitumia sana kupata ada inaitwa MPOWER na wameingia ubia na baadhi ya vyuo Canada wanakulipia ada na kila kitu unalipa baada ya kumaliza.Na uzuri wa canada unapata post graduate working permit ya kuanzia mwaka mmoja mpaka mitatu.
asante sana mkuu Mpower application zao unafanya Online au ata Tz wanaofisi
 
asante sana mkuu Mpower application zao unafanya Online au ata Tz wanaofisi
 
Ndugu zangu wana JF namshukuru Mungu sana kwa uhai.nilianza harakati za kutafuta nafasi ya masomo nje hasa nchi ya Canada.na Uzi huu ulinipa hamasa mno nimepitia changamoto nyingi mpaka kuja kufanikiwa.Nimejifunza penye nia pana njia nimepata VISA ya Canada naweza kuondoka muda wowote kuanzia sasa.Mliotupa hamasa nawashukuru na alieanzisha uzi pia maana nilijifunza mengi sana.Lengo nakwenda kusoma na kutafuta fursa za kimataifa.Asante
All the best, ukifanikiwa usioe mzungu, iko hivi ndoa ya mzungu mwanamke na mwafrika (mwanaume) hazidumu ni mateso lakin ndoa ya mwafrica mwanamke na mzungu (mwanamke) ni raha mseleleko.

Kaka zetu walio oa wazungu ndo wana majibu hiki nilichokwambia.wachache sana wana furaha.

Rafiki yangu yupo US katoka kunipigia muda sio mrefu anajuta kuoa mzungu pamoja na pesa alizo nazo bado hana furaha. Anakuja tz kutafuta mwanamke hata kama hajasoma.

N.b wadada walioshindwana na kaka zetu bongo tafuta mzungu hutojuta.
 
Kwa Japan, njia rahisi ni kwa ndoa. Watu hawaoani huku wala kuzaliana. Wanigeria wanaoa kila siku na Wajapani.

Kwa kusoma hapa, mpaka uletwe na serikali. Scholarship wanatoa kuanzia Ph.D level.

Unaweza kuja kwa kusoma Kijapani. Naifahamu shule moja ya lugha, gharama ni $1000 kwa mwezi. Wachina wanakuja hivo na kutafuta maisha wakiingia. Pia, viza hazina tabu za kuishi. Unaweza kusoma hapo kwa $500, na $500 unalipa chumba katika dorm yao. Pia, viza yako ya mwaka unaruhusiwa kufanya kazi na shule ina contact na makampuni. Baada ya hapo, akili kichwani.

Maisha ya Japan sio ghali kama unavyosoma katika magazeti. Unaweza kula kwa $10 kwa siku na kushiba. Kazi zipo nyingi tu, viwandani wanatafuta wafanyakazi, Wajapani hawazitaki na hawataki kuzaa. Kama ukitaka, nimeweka link ya vyumba vya kulala vya $500 kwa mwezi kutoka kwa agent. Unaishi kigeto, katika chumba kimoja, katikati ya jiji la Tokyo. Mgeni yoyote anakaribishwa.

Shule ya Kijapani: 東京近郊埼玉県さいたま市の日本語学校

Chumba Tokyo: www.realestate.co.jp
Mkuu Tokyo40 (au yeyote anayewekeza kunipa mwanga hapa) habari ya majukumu....

Nimeshindwa kuja PM, wacha nimwagike tu hapahapa.

Kuna scholarship za serikali ya Japan (MEXT) zimetangazwa na nimeamua kwamba na mimi mwaka hu niingize timu uwanjani (niombe).

Naomba input yako kwa uzoefu wako wa nchi ya Japan na hasa Jiji la Tokyo.

Pamoja na kwamba nahitaji elimu, exposure na connections, lengo kuu la mimi kuomba hizo scholarships ni kupata vijisenti.

MEXT wanatoa Japanese Yen 140,000 kama monthly allowance (wanaweza kuongeza yen 2,000 hapo kwa wale watakaosoma kwenye miji yenye gharama za juu za maisha).

Je, kwa huo "mzigo", kwa gharama za kawaida za mwanafunzi ambaye ameamua kujibana, na anasoma Jijini Tokyo, anaweza kutumia kiasi gani kwa mwezi ? (Nataka ku estimate, kiasi gani naweza nika sev).

2. Je, mwanafunzi anaruhusiwa kufanya kazi (hata vibarua) ili kujiongezea kipato ? (Je, fursa hizi zipo kwenye jiji kama la Tokyo, au hadi asogee "mikoani huko" kwenye mashamba ya njegere kuhesabu maboxi ?

Insight yako itanipa mwanga ili niweze kuamua vema, maana zipo possibilities za kuangazia fursa za scholarships toka maeneo mengine kama Ulaya, Amerika.

Maisha yamekua makali sana, inabidi "tutoke".

Naitafuta hii combination:
Nataka nifanye saving ya mshahara wa ajira yangu ya sasa (serikalini) + Saving ya kujibana kwenye stipend tajwa hapo juu + Saving ya kazi au vibarua nitakazofanya nikiwa huko Japan (kama ni possible).

NB; Swali langu ni Tokyo based kwa sababu (kama nitafanikiwa) kozi ninazotaka kuzisoma zinapatikana kwenye vyuo vikuu vya kilimo vilivyopo jijini Tokyo.

Ahsante.
 
Back
Top Bottom