Lusungo
JF-Expert Member
- Jan 4, 2014
- 27,534
- 40,670
Ndugu wana JF,
Kwa muda mrefu kumekuwa na masuala mbalimbali yahusuyo kujilipua (kwenda nje ya nchi) ambayo watu wanauliza mmoja mmoja kwa lemgo la kutaka msaada na ushauri namna ya kufika na jinsi ya kuanza maisha huko nje.
Kutokana na kutoa msaada kwa wengi (binafsi) kwa kutumia njia binafsi nimeona nifungue uzi huu ili kuweka mambo yote wazi kwa kadiri itakavyowezekana na kualika wengine pia waweze kutoka maoni yao.
Ndugu zangu nchi yetu ya Tanzania ki uwezo bado ni changa, fursa za kutoka ni chache na hata changamoto ni nyingi. Huko kwa wenzetu fursa ni nyingi ndio maana imekuwa chanzo cha kuvuta wahamiaji wengi sana toka mataifa masikini.
Nchi masikini wenzetu huko mbele raia wao wamejaa haswa kutokana na moyo wa kusaidiana na kuvutana.
Nimeamua nilete hoja hii kama ambavyo wenzetu hufanya huko Nairaland ya Nigeria ili kila mtu mwenye ujuzi au ufahamu juu ya namna ya kutoka (kujilipua) atoe msaada kwa wengine kwenda huko... si lazima wewe binafsi usaidie mtu binafsi NO, hata mbinu tu za jinsi ya kufika huko.
Kabla sijaingia kwenye kiini cha mada naomba nitoe faida na changamoto za kujilipua.
FAIDA
1. Fursa nzuri za kiuchumi na kujiinua hasa ukiwa na malengo.. Wakuu binafsi nimeishi Marekani kwa miaka nane. moja ya faida nilizopata huko ni kujiinua kiuchumi.... binafsi wakati naenda kusoma huko nilijiwekea malengo ya kujenga ghorofa nyumbani, kufungua mashine za kusaga na kukoboa nafaka pamoja na kumiliki fuso za mizigo.
Kipato cha mfanyakazi wa kule ni kikubwa mno kushinda hata cha baadhi ya maboss wetu hapa... hivyo nilijitahidi nilipokuwa kule malengo yangu yaimie... ni kweli baada ya muda huo nilifanikiwa kutimiza yote.
2. Huduma nzuri za afya, Elimu, Sheria, miundombinu.
CHANGAMOTO
1. Changamoto kubwa kwa kuwa kule ni upweke (ku feel home mara kwa mara japo wakati mwingine ukizoea hutoweka)
2. Xenophobia hii ni kwa baadhi ya nchi tu, sio zote.
USHAURI WA WAPI UENDE NA NAMNA GANI UENDE
Kwa wale wahitaji wa masuala ya maisha kujijenga na kuchuma nashauri nchi hizi, USA, UK, NORDIC COUNTRIES, NA WESTERN EUROPE COUNTRIES. kwa Afrika nashauri SA.
Jinsi gani utaenda namna ni nyingi. Naorodhesha baadhi hapo chini.
1. Kwenda kimasomo ambapo unaweza tafuta sponsors then ukapata scolarship itayokuwezesha kupata visa na kujilipua huko baada ya masomo.
2. Kutafuta mwenzi wa nje ambaye atakualika huko kisha mtaoana na kukuwezesha kupata resident permit na baadae uraia.
3. Kuhamisha mataji na biashara njia hii unakubaliwa popote alimradi uwe na biashara halali.
4. Kwenda kwa shughuli za utamaduni
Wenzetu wakenya na wanigeria wameunda mfumo wa kualikana wao kwa wao, kwamba mtu anakutumia barua ya mwaliko, then unakwenda ukifika huko anakutafutia mtu mnaoana kisheria tu ili upate karatasi kisha kila mtu anasika hamsini zake.
Wapendwa mambo ni mengi siwezi andika yote ndio maana nimeanziasha uzi huu tutaendelea kujuzana kwa kairi michango ya watu itakavyokuwa na maswali yatayojitokeza.
Nawakaribisha nyote. Na wote wenye maujuazi au mauzoefu ya huko mbele. Karibuni tusaidiane tujenge taifa letu. Tuwasaidie vijana wakasake fursa.