Ushauri, Maoni na Msaada: Kwa wanaotaka kujilipua nje ya nchi kusaka maisha, kusoma na kuwekeza

Mkuu Kaveli nakusalimu popote pale ulipo.

Bruh don't cry you gotta keep yo head...

afe9e745a0adcb1f055d364edb76f23e.jpg


Hahaha mkuu Lizarazu, naam. Ahsante kwa salaamu.

Nakusalimu pia. Natumai uko poa na mishe zinasonga.

Uzi huu umekuwa very useful. Nafurahi kuona wadau wanaendelea kushea fursa na kupeana madini.

Siredi hii idumu.

-Kaveli-
 
izzo kama umeona comment yangu hili suala nimeliongelea hapo juu. Tunaopewa ushauri tujitahidi tunayoambiwa tuyafanyie kazi la sivyo hizi zitakuwa stori kama za chit-chat.
Sipo perfect kuhusu hili ila jamani tunaoshauriwa ili washauri waendelee kutupigania lazima tuonyeshe efforts japo kidogo. Binafsi sikutaka kuexpose nilipofikia kwasasa ila kwa comment yako hii imenibidi japo nitaelezea kwa ufupi.

Kuna jamaa nilikutana naye na nafikiri nilimwelezea kule nyuma nikasema anayehitaji msaada wake anifuate ila sikuona reponse ya mtu yeyote. Huyu jamaa anadeal na visa za Canada na Europe anakutafutia visa then pia anakutafutia mbongo au mtu yeyote wa kukuhost kwa muda huku ukikamilisha mambo yako. Gharama yake ni usd 2000 ila ukiongea naye kikubwa inapungua.

So binafsi nimeamua kudeal naye ananishughulikia visa ya sweden a process zimeanza. Safari itakuwa before tareh 20 April. Kuhusu kurushwa jamaa sina mashaka naye japo binadamu sio wa kuwaamini.

Changamoto iliyopo kwake:
Ni namna ya kupata makaratasi maana napotoka huku nakuwa na schengen visa so bado nafanya mchakato wa namna ya kupata makaratasi na kuishi muda mrefu. Kuna watu nimekutana nao wananipa ramani ya kupata makaratasi lakini still michakato haijafikia hatua inayostahili ila shukrani kwao saana saana.

Gharama za jamaa ni nyingi maana hizo usd nilizotaja hapo sio kitoto.

Ombi langu kwenu kama kuna mtu anajua machimbo ya kupata papers nikishafika nishaurini ila nimeamua kujilipua April.
Msichoke kutushauri vijana wapo wanafutilia documents ila ni vizuri ndugu zangu muweke updates hapa tuwape moyo kina lusungo na izzo wanayofanya ni zaidi ya tuliyotarajia kuyapata.
MREJESHO...
Ulifikia wapi mkuu..!?
 
Do not seduce yourself to temporary person, as you may aware that people doesn't have much time to remember that feeling which you were shared nimejoin JF kukwambia tu mkuu you can take it or leave it.
We bwana mbona ulikuja kuwavurugia watu maisha..!?
Nini tatizo..!?
Bro stop na habari hii, utakuja kujishushia heshima huko ulipo trust me mimi yameshanikuta wabongo si watu utakuja juta kwa kile unachotaka kufanya ...
 
Mkuu Izzo kidogo nina idea kuhusu hizo issue ya za occupational health and safety coz nipo kwenye kampuni inayotarajia kupata ISO AND OH&S CERTIFICATION, so huwa nahudhuria mafunzo hayo pia nina degree.
Mkuu...
Toa idea yako tafadhali..!
 
Ndugu zangu Watanganyika ni muhimu kama huna degree coz kupata White - collar job kwanza ni ngumu kama bado ujapata PR so unaweza kuanza na kazi ndogo ndogo lakini zinalipa vizuri (pay is good) jifunzeni Construction Work , QS's, Carpenter, Painter, Plumber trust me hz kazi zipo nying sana na malipo ni mazuri sana

Kingine kuna hii kitu ambao wengi hawajui lakni ni bonge la dili inaitwa Occupational safety and health ni bonge la dili kwani unafanya kazi sehemu yeyote na kazi huwezi kukosa
Nitakuja kuwapa ujanja wa kusoma hii course online na chuo ambacho kipo chini ya U.S. Department of Labor (DOL) na kama ukimaliza hapo unasoma PROFESSIONAL TRAINING PROGRAMS ukitoka hapo course ni miezi 6 mpaka mwaka ukitoka hapo unapata kazi sehemu yeyote duniani kuanzia kwenye makampuni makubwa , viwanda,taasisi na kwenye sector ya mafuta na gesi watu wengi naona wanakwenda kusoma vitu ambayo watu wengi wanasoma siku ikitokea wametangaza ajira interview inafanyika uwanja wa taifa kwa jinsi mlivyo wengi tatizo tumefungwa ufahamu tumeshindwa kutumia milango sita ya ufahamu nyinyi mnafundishwa kuna milango 5 wenzenu wanafundiswa ni milango sita mpaka 9

Mpaka sasa hv chuo hiki kuna watu laki 3 ndio wamesoma hapa sasa jiulize duniani kuna makampuni mangapi,kuna viwanda vikubwa vingapi kuna nchi ngapi wanachimba gesi na mafuta hakuna kampuni yeyote utakayopeleka cheti cha chuo hiki ukakosa kazi duniani kwani wanafunzi wake wote wapo kwenye data base anachofanya ni kuingia kwenye data base na kuingiza namba zako tu anaona kila kitu so huwezi kufake hata kidogo

Taasisi hii ndio inasimamia maswala ya Safety na Health duniani makampuni na mashirika yote makubwa yanasimamiwa na taasisi hii ambayo iko chini ya U.S. Department of Labor (DOL)

kirikou1 kweupee Hary Jay Ndata Prishaz WiseLady Mrike wembeee talentboy Dr.adams faida Daby Tombstone Piledrive Padri Mcharo Shyshii lucley kui tagamwa binti kiziwi dangadunguri Tembo2 lusungo kweupee pius1021 Prof cognition Agogo Jr Chakochangu soul provider Mrike
Mkuu...
Mbona haukutoa muongozo hapa kuhusu hii kozi..!?
 
Wewe na mimi hatupishani. Kadegree kangu kamoja tu wategemezi kibao siishi kwa raha mjini kila saa simu za kuombwa hela tu. Nimeomba scholarship Norway China na Sweden. Zikigoma naenda kujisomesha. Mwaka jana nilipata chuo ila nikawa nategemea mpaka scholarship....sasa mwaka huu nikikosa scholarship naenda kujisomesha mwenyewe nauza ki mark x changu kisha naunganisha na mpunga mwingine huyoooo China kujisomesha nikifika huko mambo itajipa tu. Kuna jamaa yangu kaenda mwaka juzi kwa kujisimesha kajilipia ada semester ya kwanza tu ya pili akapata scholarship na sasa muda ambao hayupo darasani anafundisha vitoto vya kichinia Kiingereza anapiga mpunga wake safi wa kama mabank teller watanne kwa hapa Dar. Kaka tuondoke tupotee kama miaka mitano hivi kisha ndo turudi maana ndugu wa hapa bongo hatutaendelea
Afadhali ya nyie mnavyakuuza, wengine wapo matopeni na hizo simu za misaada ndio kama mafuriko. Mtu akifika tarehe 5 ya mwanzo wa mwezi amebakiza elfu 10 mfukoni.

Mungu hebu tusaidie manake moyo wakusaidia tunao lakini kipato hakitoshi na watu hawaelewi kabisa.
 
Asante sana mkuu tokyo mimi ni graduate wa education in science na napenda kuishi canada nimejaribu kuomba vyuo lakini gharama naona ni kubwa sana na scholsrship siqualify kwa sababu GPA yangu ni 3.4 lower second hivyo nimeoba option ni kupata training fupi hasa ya vocational jobs ambayo itaniwezesha kupata kazi canada au jyhapan au scandnavian countries ili nikisettle nisome medicine au nursing au lab science nikiwa nimepata uraia au permanent residence please naomba yeyote mwenye information anisaidie
Gpa sio shida sana kaka. Competition ni kubwa mno. Mm nina 3.6 second class upper division. Nshakosa mara kibao
 
Mkuu scholarship za Japan zinatolewa Kwa wenye advanced degree kutokana Na Tokyo40.Naomba kukosolewa kama nimekosea.Kuhusu "recommendation letter" unaipata toka kwa Mwalimu wako anaye kujua vizuri.Scholarship nyingi unaweza kujiandikisha Hata kama bado unasoma UDSM.
Kila la kheri mkuu
 
Me ninandugu yangu, ambae kwasasa ameshakuwa raia wa UK, na anafamilia kabisa kule.
Nimeshajaribu, kumshawishi anipe mbinu za kuingia kule lakini ni muoga balaa, yaan haishi kunikatisha tamaa. Mara utasikia oooh siku hizi Hali ni mbaya Sana.

Halafu inaonekana si mtu wakujichanganya kabisa yan hujui aanzie wapi ili kunirahisishia njia.

Wadau Hebu nipenni mbinu ili nimfundishe Huyu anko wangu maana amelala Sana.
hahahaaaaa
nimekudaka leoooooo
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Kwa Mara nyingine tena
Schoralship za kusoma nchini ufaransa zipo wazi kabisa kwa walio na sifa
Ni masters na PhD
Usizidi miaka 36
Nauli utapewa
Pesa Ya matumizi utapata
Mwisho wa maombi ni Tarehe 25/5/2017
Nikutuma tu kwa email
Tembelea tovuti ya ubalozi wa ufaransa hapa nchini
Tafadhali wenye sifa naomba zisikose mtu hizi nafasi...!!
Asanteni
 
Ukitegemea uende nje kwa Scholarships ni probability kabisa, tusiwe wavivu kutafutanjia nyingine, mfno mimi naomba kazi mbali mbali nje, cheti cha lugha kimekua kikwazo kwangu
 
Kwa Mara nyingine tena
Schoralship za kusoma nchini ufaransa zipo wazi kabisa kwa walio na sifa
Ni masters na PhD
Usizidi miaka 36
Nauli utapewa
Pesa Ya matumizi utapata
Mwisho wa maombi ni Tarehe 25/5/2017
Nikutuma tu kwa email
Tembelea tovuti ya ubalozi wa ufaransa hapa nchini
Tafadhali wenye sifa naomba zisikose mtu hizi nafasi...!!
Asanteni
Mkuu nimejaribu lakini

Sent from my TECNO H6 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom