milionea wa kesho
JF-Expert Member
- Dec 28, 2015
- 328
- 631
mabibi na mabwana habari za muda na wakati huu!
Nina mpango wa kuanzisha mgahawa wa hadhi ya kawaida maeneo ya stendi ya sabasaba jijini dodoma. Kwenye stendi ya daladala.
kichwani pangu nauona mgahawa upo namna hii:
Ni fremu tu ya kawaida tu nimeikodisha. kwa mbele kuna eneo la wazi nikaweka turubai za kisasa kwa juu na chini nikaweka kokoto ndogondogo kama zile za kwenye lami.
upande wa kushoto nimeweka sehemu ya chipsi ambapo zinaonekana vizuri kwenye kabati la kioo zikiwa zimeambatana na kuku, mishikaki na udambwiudambwi mwingine wote unaoujua kwa wauza chipsi. kwa wateja wanakula hapa hapa wanahudumiwa na kwa wale wa kubeba nafungasha kwenye take away.
upande wa kulia nimeweka sehemu ya matunda na juice sambamba na soda. juice za matunda yote zinapatikana hapa pamoja na matunda yote unayoyajua.
pia ile miwa ya kukata inapatikana. na maji ya aina zote yapo hata yale ya kandoro.
katikati nimeweka viti vingi pamoja na meza ambapo kuna vyakula kama wali ugali biriani n.k vinapatikana.
wahudumu ni watoto wa kike wote wazuri na wana shepu nzuri sana. hii ni kwa ajili ya wanaume wanaokuja kula chakula wanapata pia fursa ya kula kwa macho.
chakula cha hapa bei ni rahisi kidogo kulinganisha na bei za maeneo mengine ya jirani. Na ni chakula kizuri kweli kweli. mtu akila leo kesho lazima arudi.
hapa kuna wafanyabiashara wengi nakiwa nawapelekea oda za chakula. natafuta na vijana kadhaa wa kusambaza maji ya kandoro kwa wapanda daladala. maji nayaweka kwenye friji then nafunga kwenye vimfuko na kuuza 200/=.
wakuu naomba mchango wa mawazo yenu kama haya mawazo ni mazuri na yana tija.
1. kwa wazoefu na wasio wazoefu, mgahawa wa sampuli hii unaweza kugharimu starting capital kiasi gani?
2. Faida ya mgahawa inaweza kuwa kias.gani kwa mnaofanya mishe hii?
3. Ni mbinu gani naweza kutumia kuiboresha biashara hii?
Binafsi target yangu ni kuwa mwezi mmoja baada ya kuanza biashara hii niwe na uwezo wa kuingiza laki mbili kwa siku kama faida. Natarajia kuifungua mwezi ujao kama mambo yataenda vema. Mtaji wangu nafikiria niweke 1.5M.
Sent using Jamii Forums mobile app