Biashara ya chakula ukitaka ife fukuza wafanyakazi ovyo

themagnificient

JF-Expert Member
Dec 13, 2016
988
3,318
Nadhani wengi humu mshawahi kushuhudia biashara zikifa baada ya Maboss kutopenda kutulia na wafanyakazi jambo dogo tu unakuta mtu anafukuza mfanyakazi kesho analeta ukipokea mwingine

Sasa moja ya Biashara ambayo unatakiwa kukaa vizuri na wafanyakazi ni Biashara ya Mgahawa maana skuizi kuna migahawa mikubwa ya kisasa, mtu anawekeza hadi milioni 30 kufungua, maana yake hela inatakiwa irudi

Biashara ya chakula uchawi wake mkubwa upo kwenye ladha nzuri ya chakula na usafi wa hali ya juu, yaani kuna wapishi ukiwapata huwa wanapika hadi wanakera kwa utam wa chakula sasa wewe jiloge kuwafukuza kazi hovyo bila sababu kesho usije ukaja kulia

Ukienda pale mwanza kuna Bar kubwa inasifika kwa kuchoma samaki watam sana , pale ishu sio Bar bali kuna mafundi wakuchoma samaki wapo pale Tajiri anaishi nao vizuri ndio maana kila kukicha wateja wa samaki watam hawakauki, ukijiloga kufukuza tu ukileta mchomaji hivyo wote utawafukuza

Pale temeke kuna msomali mmoja alifungua mgahawa kwenye frem za kishki mtaa wa yombo ,akamuajiri kijana mmoja mtaalam sana wa kupika chapati jamaa akawa anabeba kijiji kama chote, Msomali akaamka vibaya akamwambia kazi basi, jioni akaleta kijana mwingine , yule jamaa akafungua shem kwa mbele akawa anauza chapati mwenyewe

Alihama na kijiji chake yule msomali mgahawa ukaja kumshinda kwa ajili ya utata akaufunga
 
Kwenye mfano si ungetaja jina tukienda pande hizo tule samaki
 
Kama nafungua mgahawa mzuri nahakikisha nawaiba wapishi wanaopika aina aina ya vyakula vitamu yaani Chef sio cook
Na hao mshahara lazima uwe mwingi na kuwabembeleza juu ila wakianza dharau kwangu natimua tu
Heshima muhimu
 
Back
Top Bottom