Ushauri, Maoni, Mapendekezo na Pongezi kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda

Naunga mkono hoja

P
 
Ila Makonda ana mazuri yake Mengi kama hilo la kusaidia watoto wenye shida ya moyo, mapungufu machache kama kijana anao muda wa kujirekebisha
 
''Makonda utalaumiwa,utatukanwa,utafokewa,utapingwa,lakini kwa hili la kushughulikia elimu,huna mpinzani''-Dr Bashiru Kakurwa Ally KM-CCM
Sijawahi ona Dr.Bashiru akisifia binafsi kiongozi wa serikali zaidi ya Makonda
 
Asante mkuu kwa hoja yako tukufu juu ya mkuu wetu wa mkoa Mh. Paul Makonda.

Ilibaki kidogo nikupigie makofi ya kukushukuru kwa jitihada zako za kutoa maelezo matam ya kumpa sifa RC wetu Mh. Paul Makonda. Baada ya kuingalia kiundani ikabidi nisitishe ghafla tendo hilo.

Kwa mtazamo wangu nafikiri kuna kitu kimoja kikubwa sana kina kosekana katika hoja yako uliyo tuletea. Umesahau au umekosa kutambua au kutathmini kuwa Mh. Makonda kama RC anawajibu gani katika Mkoa wake.

RC Makonda kwa vile ana mwakilisha Rais wa Tanzania katika mkoa wetu basi itambulike kuwa yeye ni Rais wa mkoa wetu. Mambo yote yanayotendeka katika mkoa huu yakiwemo mambo ya kimaendeleo na usaalama yeye ndiyo commander in chief kama ilivyo kwa Rais Magufuli kwenye nchi.

Kwa hiyo mkuu ukiondoa hiyo mada inayo husu madawa ya kulevya hayo mengine yote uliyo ya eleza juu ya engagement yake katika kutafuta pesa kwa ajili ya matibabu ya watoto masikini wenye matatizo ya moyo na kadhalika hiyo ni charity work. Naomba ieleweke kuwa Charity Work ni party ya maisha yake kama mtawala lakini sio ya kuipa kipao mbele kikubwa sana, kwani kuna wizara na idara zinazo husika. Kipao mbele chake kikubwa kiwe kwenye maendeleo ya kimkakati ya mkoa wake.

Nachotaka kukuambia hapa ni kuwa RC Makonda anajukunu kubwa sana katika mkoa huu mbali na charity work. Huu mkoa una wakazi wengi sana kuliko mkoa wowote mwingine nchini, zaidi ya hayo huu mkoa ni Gateway la kutuunganisha sisi na Outside world. Kwa hali hiyo nguvu kubwa inatakiwa itumike kuufanya huu mkoa kama jiji kuwa dynamic.

Ukiangalia uwingi wa idadi ya wakazi wa huu mkoa ambao mpaka hivi sasa wako na wale ambao kila siku wanaongezeka kutoka mikoani na vijijini na hata nchi nyingine za ulimwengu, utaona kuwa the dynamism au kasi ya utekelezaji wa mipango na miradi mingi ya maendeleo ili kukidhi mahitaji na matakwa ya wakazi wa huu mkoa, haiendani, ni ndogo mno.

Charity activities za mkuu wa mkoa kwa uzito wa majukumu wa huu mkoa naona ni kaji tone tu cha maji kwenye mawe mengi kubwa,
ukilinganisha na speed la ongezeko la watu. Huu mkoa unahitaji nguvu kubwa sana ambayo mimi bado sijaiona kutoka kwa Mh. Makonda. Anahangaika na vitu ambavyo, ndiyo kwa upande mmoja unaweza sema kwamba ni muhimu, lakini sio kihivyo.

Ikumbukwe tu kuwa Dar es salaam hivi sasa kulingana na takwimu nilizo nazo kwa wastani ina wakazi wapatao zaidi ya milioni 5, mpaka kufikia 2030 tunaweza tukafika milioni 10. Je, tuna nini ambacho tumejiandaa mpaka sasa? Wakati mitaani vijana wasomi na wasio wasomi wamejaa kibao wakiwa hawana ajira.

Sikatai vipaji vyake vya kuwa attractive na talkative kwa watu na hasa vijana, wakina mama na wasanii, lakini hata hivyo ana ukosefu mkubwa wa Vision na innovation drive kama ya Rais Magufuli.

Kama ushauri wangu tu kwake na kwa wote wanao husika, Makonda anatakiwa ajishughulishe zaidi na maadalizi ya vijana wenye talents tofauti ambao ni potential ya watoa ajira ya leo na kesho kwa vijana wenzao kwa kuwa kusanya hao vijana wenye hizo talents na kuwajengea facilities na funds ambazo zita wawezesha ku improve hivyo vipaji vyao na kuona jinsi gani wanavyoweza kuusaidia mko wetu kiajira kwa vijana.
Mfano talent ya huyu kijana Moses Mbaga ambaye ameweza kutengeneza App yake;
Makonda anatakiwa katika kuwa hamasisha vijana hao wenye vipaji vya pekee kushirikiana na walimu, maprofessor, mawaziri na Rais mwenyewe.

Makonda anatakiwa ashirikiane na timu yake ya wataalam kutafuta na kubuni miradi midogo midogo na mikubwa ya maendeleo ambayo itawawezesha wananchi kutengeneza na kupata ajira. Asijikite sana na upande mmoja tu wa kukusanya pesa kwa ajili ya charity work na wasanii peke yake.

Kitu kingine ambacho ningependa kumshauri ni usimamizi wa miradi. Asipende sana kutumia njia za zamani ambazo hazija leta mafanikio yeyote kwetu ya kusimamia kazi kwa kila mara kuitisha mikutano kama kwenye hii clip;
Rais Magufuli kipindi cha awamu ya nnewakati akiwa waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano alifanikisha miradi mingi mikubwa ya barabara kwa sababu yeye mwenyewe alikuwa site na kujiona mwenyewe kitu gani kinaendelea.

Kwenye hiyo clip nasikitika kusema sijamwona akionyesha seriousness ya hilo onyo alilopewa kwa mara ya pili. Inaaminika kuwa yeye na RASI wake wamepoteza mda mwingi kuwakusanya watendaji wake kwenye kikao badala ya kuwaambia wakutane site. Hayo maandalizi da COCO Beach ameyaonabkwenye clip.

Yeye kama mkuu wa mkoa angeweza hata tumia Helikopter ya jeshi au polisi kama hana ya kwake mwenyewe, I mean ya mkoa, kurash kwenye hiyo sites za miradi mbali mbali badala ya kuitisha kikao na kupiga siasa za kuunda tume da usimamizi. Anaunda tume leo? Hilo alitakiwa alifanye mwezi wa tatu wakati alipo kutana nao na kuwapa maagizo.

Mkuu wa mko wa jiji hili kulingana na uzito na ukubwa wa majukumu anatakiwa permanently awe angani na helikopta kuangalia na kusimamia miradi mbali mbali inayo fanyika jijini. Haya mambo ya kwenda kuji show off kwenye matukio ya matatizo kama ya mafuriko na kadhalika na hatimaye hakuna kitu kinacho endelea baadae cha kutatua tatizo lisitokee tena, haina tija kubwa kwa wana Dar es salaam na imepitwa na wakati.

Hali hii ikiendelea hivi hivi, nakataa katakata kama itaweza kuwa na mafanikio chanya siku moja. Watanzania hasa wabongo tuna mind sana starehe za hanatha kuliko kuumiza vichwa katika kufanya kazi za maendeleo yetu. Tunataka pesa za haraka haraka ili tuende kwenye vimada vyetu na mkubali kusifia maendeleo ya wenzetu!
 
Umetoa ushauri murwa kabisa tatizo ni kama Bashite atazingatia.
 
Umetoa ushauri murwa kabisa tatizo ni kama Bashite atazingatia.
Asante mkuu. Hilo atalijibu mwenyewe Makonda. Rais Magufuli amesha sema "mesaage sent and delivered". Kitakacho mtokea next asimlaumu mtu.

Nafikiri bado haja realize umuhimu wa kuwa mkuu wa mkoa wa jiji kama jili la Dar es salaam.
 
Nashukuru kwa kutonipiga makofi.
Kwa maelezo yako, MAKONDA yumo humu na atachukua kama changamoto.
hii nchi ni yetu sote, tumsaidie huyu bwana mdogo kwenye utawala, aachana na "petty issues" ajielekeze kwenye mambo yenye maslahi na wengi mkoni.
note: amshauri baba yake kuzingatia sheria na katiba
 
Sifa ya kiongozi ni kuwa na ushirikiano kati ya sekta moja na nyingine majuzi nimemsikia akijitetea mbele ya raisi kuwa aliwa achia manispaa zijitawale kwa mujibu wa sheria kwa maelezo haya tu ilitosha kutumbuliwa maana kodi zetu zinafujwa na wahuni wachache chini ya usimamizi mbovu wa mkuu wa mkoa wa dar es salaam
Hii ina maanisha kuna maeneo ambayo makonda atakuwa anashiriki kiaina katika ulaji wa hela zetu ..Raisi hakutakiwa kuwafundisha nn cha kufanya katika miradi ya kimkakati ....
 
Ungeweka na namba zako za simu ili "mteuzi" akisoma hii thread akutunuku hicho cheo
 
Hapati usingizi tokea juzi anakesha kwa waganga wa kienyeji wapya walioletwa na na Le mutuz toka Africa ya kati na chad
 
Le mutuz kapiga pesa ndefu kipindi hiki kuliko vipindi vyote kwani kamtisha Bashite kuwa safari hii anakwenda na maji ndipo Bashite kamlipa pesa Ndefu kumletea waganga wapya
 
Pumbafu sana wewe
 
Es geht doch! So muss es sein.
Es lebe Präsident Magufuli! Es lebe RC Makonda!

It works! That's the way it has to be.
Long live President Magufuli! Long live RC Makonda!

Dar es salaam oooyeeeeeeeeeeeee!
 
Asante mkuu wetu wa mkoa. Unafanya kazi nzuri.

Ningeomba kukupa ushauri kidogo mheshimiwa wetu; Jitahidi ukiwa site kuhojiana na wataalam wa ujenzu ili kujua nini kinaendelea, japo kuwa najua basic yako ya kisayansi ni ndogo hata hivyo kabla hujaenda site mwambie mtaalam wako wa kitengo cha utaalam wa mkoa akuandae kidogo mambo ya kuuliza kama mkuu wa mkoa wa Tabora Mh. Mwanri na waziri wa Temisemi Mh. Suleiman Jafo wanavyo fanya.

Usipende sana kujionyesha kama figure isyoelewaka ukiwa site na kila wakati kumsifu Rais Magufuli. Kuwa wewe mwenyewe kama mtu unaye penda kujua nini unataka na kujiamini.

Usipende sana kila wakati kutumia neno Rais Magufuli na kumfanya yeye kama ni mungu. No, tumia sana serikali china uongozi wa ... ili kutuonyesha sisi kuwa na wewe pia ni party ya hiyo serikali.

Rais Magufuli asikupe shida yeye kazi zako ataziona na kukutunikia unachostahili mheshimiwa wetu. Wewe wabane tu kikamilifu hao wababaishaji. Sisi tunataka matokeo chanya na tuko pamoja na wewe kiongozi wetu.
 
RC Makonda unaona viongozi wanao tambua majukumu yao?

Msikilize Bashe vizuri, anaweka mambo clear anacho taka kifanyike. Humsikii kila wakati aki taja taja Magufuli bila sababu.

Hivi ndivyo kiongozi mwenye msimamo anavyo takiwa ku act. Yeye anajitambua kuwa kapewa madaraka na mamlaka ya kisheria kusimamia maendeleo katika wizara ya kilimo. Kwa hiyo ni wajibu wake kujua wapi kuna matatizo na kufanya mpango wa kuyatatua matatizo hayo. Ni wajibu wake. Full stop. Na sio Magufuli kasema hivi, oo tumpongeze Rais wetu and blaa blaa blaa!

Lakini wewe una luka luka weee, mpka Rais akikushtua ndiyo unaanza kulalamika, watendaji wangu walikuwa hivi, mala watendaji wangu wameniangusha and so on and so on! Yanini? Wewe umekabidhiwa hayo madaraka ni wajibu wako ku deal nao. Sisi tunacho taka ni matokeo.

Wewe unawajua jinsi watendaji wako walivyo wanyooshe sasa na sio kulalamika kwetu. Unatulalamikia sisi tuwafanye nini? Kama unaona hawa perform inavyo stahili mwambie Rais au waziri Mkuu watajua nini cha kufanya. Watonye tu kwao usiwaonee huruma. Hayo mamlaka RC Makonda uliyopewa ya kuongoza hili jiji ni makubwa!

Naibu waziri Bashe anapiga show lakini wakati huo huo anaweka msimamo. Hata wananchi wakimwona wana sema yes, huyu ndiyo kiongozi!

RC Makonda wewe ni kiongozi wa show off na mbwe mbwe nyingiii, lakini tukija kwenye out come it is almost ZERO!

Nakuomba radhi RC Makonda kama nitakuwa ninakukwaza. Najua wewe ni mzalendo kama mimi najaribu tu kukusaidia uuone wapi unakwama na ujirekebishe vipi.

Hili jiji Rais wetu alilo kupa ni kubwa sana na gumu sana kuli control. Kwa hali hiyo ina hitaji busara kubwa sana kutambua kuwa Rais amekuamini sana. Mwonyeshe Rais kuwa wewe utalikabili na kuliweka katika hali inayo takiwa. Katika uongozi usipende kupendwa na watu wote, wako watakao kubeza na kukurudisha nyuma. Usikubali mdogo wangu. Pigana pigana tu. Rais bado ana imani na wewe, usimwangushe!

Haya mambo ya wasanii na michezo mwachie Waziri Mwakyembe ana yaweza vizuri sana. Wewe deal na changamoto za Jiji letu kiasi kwamba ukitoka jina lako libaki for an eternity mdogo wangu.

Simamia miradi yote hata ile ya barabara za mitaa, masoko, majengo, shule, hospitali na miradi ya mazingira na kadhalika na washirikishe Mawaziri na Rais kwenye projects ambazo zitaleta ajira kwa vijana.

Komaa kijana wetu, komaa, sisi tuko pamoja na wewe. Mungu atakusaidia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…