Ushauri: Mama mkwe kaahidi kuniroga, kunifunga jela au kuniua

Ushauri: Mama mkwe kaahidi kuniroga, kunifunga jela au kuniua

mkuu kusoma huwezi na picha pia huoni?!!! ukimwachia watoto unatumaga matumizi au kununua vyakula hivyo hii nayo inampunguzia makali ya maisha , sasa wewe unachukua mradi wake ili iweje halafu akuchekee!! ebooo

mkuu laki mbili kwa mwezi ndo pesa inayotakiwa kutuma kwa mama mkwe kweli uwezo umenishinda
 
mkuu laki mbili kwa mwezi ndo pesa inayotakiwa kutuma kwa mama mkwe kweli uwezo umenishinda


kumbe umekubali unatuma hela!! ujue mtu akikaa na mtoto then wamtumia hela anaponea hapohapo sasa unavyomchukua unategemea nini? kaona atapauka huyo nna experience yakuacha mtoto kwa mtu
 
Swala la Msingi hapo tafuta wazee, ikiwa wazee wa upande wako wako mbali na unahisi nivigumu kuja basi tafuta wazee wa upande wake. Pia hakikisha huyo mkeo nae awe msitari wa mbele kuwahitaji hao watoto, na kwa ndugu zake aende aweelezee hali halisi. Lakini nawe usisite kuchukua tahadhar ya hayo matamshi ya mkweo.
 
muda mwingi nilitumia wazee lakin waliambulia matusi na kejeli

kaka inakuwaje familia yako (watoto) walelewe na mtu mwingine mbona hicho kitu hakipo duniani mwenye haki na wajibu na mtoto ni wazazi waliomzaa. Vp ndugu yangu mbona sielewi hapa maana hata sheria za nchi ziko upande wako nenda kachukue watoto kwa nguvu ni haki yako ina maana unashindwa hata kuwavizia siku hayupo ukaenda kuwachukua au kuwafuata shuleni maana hata akikushitaki watamshangaa hamna mtu anayeiba watoto aliowazaa

Hiyo kurogwa na mengine ya kukutishia katoe taarifa polisi na serikali za mitaa na wape taarifa ndugu wa pande zote, Acha kuogopa mikwara mbuzi kama kukuroga angeshakuroga muda mrefu tu kama ni mrogaji kweli
 
Tafuta viongozi wa imani yenu, ili wakae wamshauri awaachie watoto wenu mpate kuendelea kuwalea ukizingatia watoto wanahitaji malezi na UPENDO wa wazazi.
 
wazazi wengin wanga kweli...yamahusu nini ya maisha yenu sijui umaskini au utajiri....kama vp ripoti polisiaaaaah no piga maombi tu
 
Soma sentence zake anazo tamba nazo eti atakuroga au atakupeleka ngome ( jela ). Mie kwa mahono yangu huyo bimkubwa anazo chembechembe za uchawi na hao wanao atakuwa anawatumia mida ya usiku mnene kuwarostisha raia. Pia baade akivuta wanao walisi mikoba ya bibi. Kwa ushauri kama mtu wa dini kama mie
nenda fasta kanisani au msikitini kaonane na wazee .kama sio mtu wa dini msera kama mie nenda kwa sangoma pande za simba wanga (songea) au T A (tanga ).hukifanya masihara kweli mjomba utakuwa crazy au utahenda ngome kweli.
 
ni kweli mkuu kwani kuombwa laki 2 nijambo la kawaida na nimekuwa nakataa kutoa hapo ndo neno masikini likaanza

Mambo kama yako wazi hivyo ni vema ukawaeleza waziwazi kwamba juhudi zote unazofanya ni kwa manufaa ya mkeo na watoto tu. Mtu mwingine atapata kwa ziada nafasi inaporuhusu. Wasikugeuze ATM. Future ya watoto ni bora zaidi kuliko mtu mwingine yoyote.
 
Swala la Msingi hapo tafuta wazee, ikiwa wazee wa upande wako wako mbali na unahisi nivigumu kuja basi tafuta wazee wa upande wake. Pia hakikisha huyo mkeo nae awe msitari wa mbele kuwahitaji hao watoto, na kwa ndugu zake aende aweelezee hali halisi. Lakini nawe usisite kuchukua tahadhar ya hayo matamshi ya mkweo.
Mke wake hawezi kuwa mstari wa mbele kuhitaji hao watoto wakati hilo ni dili amepanga na mm yake, wakati mumewe anasurubiwa mke anachekelea
 
Hii kessy ni nzito sana kwanza kuna udini kitu kibaya sana hiki alafu umembadilisha mwanae dini kiukweli tayari ushatengeneza chuki mwenyewe huyo mama sio mchawi na anakiki tumamu sasa cha kufanya chukuaa watoto kinguvuu kabla hujachelewa alafu mengine yatafata
 
Kweli aisee, tangu watoto wahamie kwake maisha yamekuwa mteremko akikumbuka ngumu za kabla lazima awe mbogo. Jamaa akachukue watoto wake. Uzuri ana support ya huyo mke wake.
mkuu kusoma huwezi na picha pia huoni?!!! ukimwachia watoto unatumaga matumizi au kununua vyakula hivyo hii nayo inampunguzia makali ya maisha , sasa wewe unachukua mradi wake ili iweje halafu akuchekee!! ebooo
 
Ndugu zangu,

Mimi nina tatizo na mama mkwe wangu kwa kifupi nimeishi na mtoto wake kwa miaka 15, sasa na tumepata watoto wawili lakini jambo la kushangaza ametoa kauli nzito kwangu akisema kuwa ataniua, kunifunga jela, au kuniroga.

Ugomvi wetu ni watoto wangu ambao niliondoka nyumbani kwenda Morogoro kutafuta maisha, mke wangu akabaki nyumbani kama miezi miwili akaja kunifuata.

Tumekaa kama miezi 6 akarudi nyumbani kuchukua watoto ambao aliwaacha kwa mama yake mzazi lakini mama akamnyima watoto na aliporudi tukajadiliana na kupata jibu kuwa niende. Mimi nikaondoka, lakini nilikutana na matusi mazito. Kwa hekima sikumjibu chochote nikaaga na kuondoka.

Ikapita miaka minne bila kuulizana chochote! Jambo la kushangaza mwanzo wa mwezi wa 8 tulikuja wote kwa ajili ya kusalimia na kuomba watoto lakini katamka wazi mbele ya mke wangu kuwa hanipendi na hataki nikanyage kwake niwe na mwanae.

Mke wangu alijua utani kumbe mama yake alikuwa hatanii. Sasa mimi nataka kuondoka nimuache mke wangu yeye hataki na anataka kujiua.
Pole sana mkuu, mtafute mshenga wako muongee pamoja na wakwe zako
 
wanawake nao dah anataka ajiue ili iweje sasa...hapo sasa watakiwa kuwa strong zaidi maana hili bado lingine laja....pole sanahizo roho chafu anazo....maombi pia kwa sana hapo pia mpetafu wife awe strong...muulize vizuri kuna nini na mama yake....af ukipata watoto wako tengana na hiyo ukaribu ukate kabisa ife ndio adilinao af watoto wako ni wako sio wa mama mkwe
 
Kama amekutishia kukuua muwahi polisi ukatoe taarifa.
 
Ndugu zangu,.

Wachukuwe watoto, hakuna kitu kinachoitwa kuroga/kuloga, ni upuuzi wetu ni imani zetu za kishirikina, zama za ujima, jaribu kuwa mtu wa kisasa na kuachana na imani potofu, mbona polisi wakiwakamata hao waganga na kusekwa ndani huwa hawatoroki kichawi?!
Chukuwa watoto wako na kama waona hauko salama kimaisha toa ripoti polisi kuwa umetishiwa maisha, ila usiseme mambo ya kichawi maana hayajulikani kisheria.
 
Back
Top Bottom