Ushauri: Mama mkwe kaahidi kuniroga, kunifunga jela au kuniua

Ushauri: Mama mkwe kaahidi kuniroga, kunifunga jela au kuniua

maskio popo

Senior Member
Joined
Sep 3, 2015
Posts
158
Reaction score
31
Ndugu zangu,

Mimi nina tatizo na mama mkwe wangu kwa kifupi nimeishi na mtoto wake kwa miaka 15, sasa na tumepata watoto wawili lakini jambo la kushangaza ametoa kauli nzito kwangu akisema kuwa ataniua, kunifunga jela, au kuniroga.

Ugomvi wetu ni watoto wangu ambao niliondoka nyumbani kwenda Morogoro kutafuta maisha, mke wangu akabaki nyumbani kama miezi miwili akaja kunifuata.

Tumekaa kama miezi 6 akarudi nyumbani kuchukua watoto ambao aliwaacha kwa mama yake mzazi lakini mama akamnyima watoto na aliporudi tukajadiliana na kupata jibu kuwa niende. Mimi nikaondoka, lakini nilikutana na matusi mazito. Kwa hekima sikumjibu chochote nikaaga na kuondoka.

Ikapita miaka minne bila kuulizana chochote! Jambo la kushangaza mwanzo wa mwezi wa 8 tulikuja wote kwa ajili ya kusalimia na kuomba watoto lakini katamka wazi mbele ya mke wangu kuwa hanipendi na hataki nikanyage kwake niwe na mwanae.

Mke wangu alijua utani kumbe mama yake alikuwa hatanii. Sasa mimi nataka kuondoka nimuache mke wangu yeye hataki na anataka kujiua.
 
Nahisi ana matatizo ya akili huyo.
Jaribu kutafuta wazee na wenye hekima waongee naye ujue ni kwa nini anafanya hivyo na kwa nini anakuchukia na kukutamkia maneno yote hayo.
Hatua ya mwisho wachukue watoto wako kwa nguvu ili ajue ya kwamba wewe ni mwanaume na huna masihara katika hilo.
 
Nahisi ana matatizo ya akili huyo.
Jaribu kutafuta wazee na wenye hekima waongee naye ujue ni kwa nini anafanya hivyo na kwa nini anakuchukia na kukutamkia maneno yote hayo.
Hatua ya mwisho wachukue watoto wako kwa nguvu ili ajue ya kwamba wewe ni mwanaume na huna masihara katika hilo.

asante kwa ushauri mkuu ila nilituma wazee akawajibu mimi ni masikini na tangu nimchukue mwanae hatujafanikiwa kimaisha kwa hiyo nibora akae. nachukua ushauri wako wa kutumia nguvu
 
pole kaka angu hya ni maisha tu chamsingi chukua watoto wako kwa sababu ile ni damu yako na kama mke anakupenda chapeni lapa,kama anataka wakwe matajiri akae namwanae
 
Wazee wengine wachawi wanawafundisha wajukuu isije kuwa ni mmoja wao....(jokes)
 
asante kwa ushauri mkuu ila nilituma wazee akawajibu mimi ni masikini na tangu nimchukue mwanae hatujafanikiwa kimaisha kwa hiyo nibora akae. nachukua ushauri wako wa kutumia nguvu
mkuu mpigie kula lowassa hapo oct 25 ili tuondoe huu umasikini hopefully mama mkwe ataacha kukuchukia
 
Umwache mke kwa kosa gani,yy ndiye aliyekutukana na kusema hakupendi?acha mawazo hayo.
 
Duh! Majaribu mengine bana!!Ila cha muhimu ni kuhakikisha ukisha chukua Watoto wako uhamie Kanisani/msikitini na kuwa karibu sana na Mungu. Napia omba sana Mungu akupatanishe na huyo mkweo na ambadilishe la sivyo mtaanza kupigana vita vya kimwili na kiroho na mwishowe mmoja wenu au watoto watakuwa wahanga. Kumbuka akikushindwa wewe atawalogha watoto.
 
Jaribu kuchunguza kwa kina, kung'ang'ania wajukuu namna hiyo si jambo la kawaida, isije kawa watoto wanasubirishwa kufuzu ubebaji wa mkoba vizuri!
 
watoto wanahitaji malezi ya wazazi na sio ya bibi hapo wewe chukua wanao af mengine yatafuata....kuhusu vitisho hivyo neno 'USIOGOPE' limeandikwa mara 365 katika biblia means kila iitwapo leo hutakiwi kuogopa
 
Katoe taarifa polisi wamuweke kwenye watch list, kitakachokutokea chochote yeye ndo muhusika.
 
Umaskini huu utatupeleka pabaya sana. Mungu akusaidie sana ndg yangu maana hakuna jinsi tena, amini kwamba hawezi kukufanya kitu chochote
 
Pole kaka....haya ni mapito tu ya dunia ipo siku mungu atakunyoshea neema.
 
ndugu matishio ya vitisho vya uhai kwanza vinaripotiwa polisi.

sema huyo bi msdashi nahisi ni mwanga. au huenda tatizo lipo kwako pia
 
Back
Top Bottom