Ushauri kwa Wazanzibari

Goodrich

JF-Expert Member
Jan 29, 2012
2,091
1,177
Nitaongea/kuandika kiimani zaidi.

Hekima imenifundisha kuwa kila jambo lina asili yake.

Zanzibar kuna tatizo, tatizo ni kuwa Wazanzibari wanajiona kuwa hawapo huru.
Wanajiona kuwa baada ya Sultani kuondoka sasa wanatawaliwa na Tanganyika. Kwamba they are not sovereign. Kwamba hawawezi kujiamulia mambo yao. Hata Rais wao wanapangiwa na Watanganyika.

Ni kweli hawapo huru.

Lakini Tatizo hili lina asili yake.

Asili yake ni laana ya kuficha ukweli wa historia ya Mapinduzi.
Wameficha au kufanya siri historia ya Mapinduzi na hivyo mapinduzi hayo yamekuwa kazi bure. Hayana Baraka zozote.

Hawatakuwa huru mpaka watakapopata fursa ya kujiuliza kwa kina kuwa kwa nini hawapo huru hata baada ya mapinduzi.

Hakuna sababu ya kuendelea kuficha ukweli kwa kuwa Sultani Jamshin Abdullah aliyetimuliwa yupo hai anaishi Uingereza, japo Shujaa John Okello alifariki miaka michache iliyopita Uganda lakini Waliohusika wengi tunao, Picha na Video za mapinduzi zipo, Nyaraka na Majengo yaliyotumiwa na Sultani yapo.

Jiondoeni kwenye kifungo hicho, wekeni wazi historia ya mapinduzi, tajeni mashujaa wa mapinduzi, tajeni waliopoteza maisha katika harakati hizo, mtakuwa huru.
 
Back
Top Bottom