Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 63,678
- 107,843
Mtakapotoka hadharani kabla kwanza ya kueleza malalamiko yenu na kutokuridhishwa kwa yanayotokea sasa ni vyema kwanza mkatubu na kuomba radhi wote walioteseka na wanaondelea kuuguza maumivu na vidonda kutokana na ukatili waliopitishwa katika awamu yenu.
Wahanga watafarijika sana wakisikia mnasema haikuwa sawa na sio vyema kuendelea na yale ambayo hayakuwa sawa yaliyowaumiza.
Viongozi kuomba radhi sio udhaifu bali ujasiri, kujitambua na kuonyesha kujali. Papa aliwahi kuomba radhi kwa masaibu ya unyanyasaji wa kingono yaliyofanywa na baadhi ya maaskofu na mapadri, aliwahi pia kuomba radhi kwa baadhi ya mapadri kushiriki katika mauaji ya kimbari ya Rwanda. Kaburu De Klerk rais wa mwisho wa makaburu aliomba radhi kwa niaba ya makaburu wenzake Africa Kusini kwa madhila yote waliyowapitisha watu weusi kwenye nchi hiyo katika utawala wa kibaguzi.
Nilisikitika sana Polepole alipodogosha na kupuuza madhila aliyopitia Tundu Lissu kipindi yeye akiwa kwenye mfumo, jambo hilo kwenye press yake ni kama lilikuwa jiwe au chuya kwenye wali mzuri.