Ushauri kwa wale wa early 2000's na late 90's

100 others

JF-Expert Member
Aug 5, 2017
3,626
12,053
Wadogo zangu muziki ni sanaa, ni kama filamu, unapoingia kwenda kutazama filamu cinema au nyumbani unapomaliza unaiacha palepale. Kwenye filamu si kweli kuna uhalisia kwamba spiderman yupo au wale characters kwenye avengers wapo, hakuna uhalisia ile tunatazama kuburudika tu.

Hivyo hivyo jumbe zilizomo kwenye baadhi ya nyimbo si za kuchukua na kuzifanyia kazi, kundi hili la vijana kuanzia late 90's hadi mwanzoni mwa 2000 ndio wahanga wakubwa kwa sasa wa maudhui yanayokuwepo kwenye social medias na nyimbo.

Nimesoma habari kijana kajiua, kisa stress za mahusiano akaenda kusikiliza nyimbo ya dear x mara 60, baada ya hapo kaenda kujiua.

Sasa hivi kuna hizi nyimbo za amapiano mtu anaimba na kusifu pombe na malaya kwamba anakunywa hadi asubuhi, nyimbo za kusifu ngono, matusi na kila aina ya false message. Nipende kusema hakuna uhalisia, tena hawa wasanii wengine hata hizo pombe hawanywi.

Mwisho: Maisha ya hawa social media influencers, wakiwemo wasanii na wengine maarufu, jina lingine ni internet personality, personality na life style yake kwenye internet/medias sio kweli katika uhalisia, wengi wana fake, na ile ni ajira yake.
 
Hili tunalijua mkuu ila dunia nzima tuna furahia vibe kwa hiyo kama wasanii wenyewe hawanywi shauri zao sisi tukipata hela tuna kikao cha kumwagilia chini ya pua suala la kukesha kila mtu ashinde mechi zake na kila mtu aubebe msalaba wake mwenyewe ila vibe tuachie mkuu hata ikipigwa ya rose muhando kama inachezeka tunaruka nayo
 
Vijana wangu mnakunywa sana pombe, tena mkipigiwa na zile nyimbo za kusifu ulevi ndio basi unaweza malizia hapo mshahara.

Hebu nipe faida hata moja ya kunywa pombe?
 
Wadogo zangu muziki ni sanaa, ni kama filamu, unapoingia kwenda kutazama filamu cinema au nyumbani unapomaliza unaiacha palepale. Kwenye filamu si kweli kuna uhalisia kwamba spiderman yupo au wale characters kwenye avengers wapo, hakuna uhalisia ile tunatazama kuburudika tu.

Hivyo hivyo jumbe zilizomo kwenye baadhi ya nyimbo si za kuchukua na kuzifanyia kazi, kundi hili la vijana kuanzia late 90's hadi mwanzoni mwa 2000 ndio wahanga wakubwa kwa sasa wa maudhui yanayokuwepo kwenye social medias na nyimbo.

Nimesoma habari kijana kajiua, kisa stress za mahusiano akaenda kusikiliza nyimbo ya dear x mara 60, baada ya hapo kaenda kujiua.

Sasa hivi kuna hizi nyimbo za amapiano mtu anaimba na kusifu pombe na malaya kwamba anakunywa hadi asubuhi, nyimbo za kusifu ngono, matusi na kila aina ya false message. Nipende kusema hakuna uhalisia, tena hawa wasanii wengine hata hizo pombe hawanywi.

Mwisho: Maisha ya hawa social media influencers, wakiwemo wasanii na wengine maarufu, jina lingine ni internet personality, personality na life style yake kwenye internet/medias sio kweli katika uhalisia, wengi wana fake, na ile ni ajira yake.
Upo sahihi sana na barikiwa mno naamin wapo wachache watakuelewa

Ukweli hizi nyimbo zimekuwa too much kwenye uharibifu wa kizazi cha sasa, zinahitajika jitihada maalumu kunusuru vizaz vyetu
 
Hivyo hivyo jumbe zilizomo kwenye baadhi ya nyimbo si za kuchukua na kuzifanyia kazi, kundi hili la vijana kuanzia late 90's hadi mwanzoni mwa 2000 ndio wahanga wakubwa kwa sasa wa maudhui yanayokuwepo kwenye social medias na nyimbo
Mimi ni msikilizaji mzuri sana wa hizo nyimbo na kila weekend lazima niingie viwanja either Elements, SamakiSamaki au kitambaa cheupe na sivuti sigara, bangi wala sinywi pombe.

Anayewafwatisha wasanii na tabia za watu wa social media ni mjinga.
 
Si kwelii kiongozi, Labda unatak kuleta picha tofuati hapo. Lakini si kweli hilo usemalo
 
Safari hii vijana shughuli tunayo. Kila tunachogusa lazima itafutwe angle ya kutusimanga. Mbona kuna mafaza na mabroo kibao tu ni walevi mbwa. Anyway ushauri mzuri
Sio kwamba mnafuatiliwa maisha yenu, ni ile kukumbushana kwamba tupo katika nyakati mbaya, mtandao wa business insiders africa umetoa takwimu Tanzania ni nchi ya pili bara la Africa kwa kunywa pombe.

Hivyo lazima tunakumbushana, ukiona mtu anakuambia ujue anakupenda na kukutakia mema.
 
Back
Top Bottom